Jirani anajenga Msingi wa ukuta katikati ya jiwe la mpaka la manispaa, Sheria ya Ardhi inaruhusu hii?

Ramani inaonyesha kuna njia baina yako na jirani?
 
Yes amemsaidia upande mmoja..........Kuna wengine wana bahati anasaidiwa pande tatu zote yeye anabakiza kufunga mbele tu na kuweka geti....Ukinunua viwanja vya kupimwa ndio advantages zake hizo.
Hapana.Kuacha nafasi kati ya nyumba ya kiwanja kimoja na kiwanja kingine ni lazima kisheria za ujenzi.Na kuna vipimo vyake.Kila mmoja ataacha mita moja na nusu kutoka katika jiwe/bikoni yake.Akileta ubishi atabanwa kwa kuombwa yafuatayo kisheria za mipangomiji/halmashauri;-
1-Uhalali wa umiliki eneo(nyaraka halali),
2-kibali cha ujenzi kinachoenenda na muda(expire date)
3-Na kama amehamia/nyumba ipo,ataombwa leseni/kibali/ruhusa ya kisheria ya kuishi hapo,
4-Hana hivyo vitu;a,atapigwa faini kimojakimoja-b,atasimamishwa ujenzi-c,atavunja ukuta kwa muda atakaopewa kwa gharama zake-d,atapewa onyo kali aache ungedere.🙏🙏🙏😂😂😂😂
 
Kama anajenga ukuta ni sawa kaeni chini mchangie gharama ukuta uwe wenu wote.

Ila kama anajenga nyumba na ikiwa una nguvu kdg ya kifedha wala usimsemeshe atakapotoa kijiti chake weka chako jenga ukuta mrefu kupita makadirio ya pale atakapofungia lenta. Then kaa relax uone atapauaje?
 
Tanzania hii hii ya Samia au
 

Ukuta anaoujenga ataupaua. Maana mabanda ya kuku wake na mifugo mingine yanategemea huu ukuta.

Sasa akiupaua si itakuwa balaa
 

Hiyo si ni fensi mkuu? Kama ni fensi hapo yuko sahihi shukuru Mungu kakusaidia upande mmoja wa fensi.

Sali zaidi watokee na upande wa nyuma na pembeni.

Ila kama si fensi hapo sasa patakuwa na shida.
 
Yes amemsaidia upande mmoja..........Kuna wengine wana bahati anasaidiwa pande tatu zote yeye anabakiza kufunga mbele tu na kuweka geti....Ukinunua viwanja vya kupimwa ndio advantages zake hizo.
Sijawahi kubahatika hili zaidi nimewafaidisha majirani mara mbili sehemu tofauti.
Mimi naumia kujenga ukuta halafu wao wanakuja kuunganisha ukuta tu utafiiiri mimi baba yao
 
Ukuta anaoujenga ataupaua. Maana mabanda ya kuku wake na mifugo mingine yanategemea huu ukuta.

Sasa akiupaua si itakuwa balaa
Kama ni ukuta wa banda na si nyumba ya kuishi mfikishe kwenye uongozi mkubaliane kuwa utakapohitaji kujenga utautumia ukuta wake then unakuja unamalizia alipoishia unazungusha ukuta wako na upande huo unaotesha fensi ya maua ili kuziba madirisha yake asiwe anakupiga chabo ukiwa kwako
 
Sijawahi kubahatika hili zaidi nimewafaidisha majirani mara mbili sehemu tofauti.
Mimi naumia kujenga ukuta halafu wao wanakuja kuunganisha ukuta tu
Ikiwa najenga ukuta lazima ni mshirikishe jirani gharama kutegemeana na hali yake ya kimaisha ili tuutumie wote na ikiwa atakuwa mkorofi na ninaona kbs uwezo anao na kiwanja changu ni kikubwa upande wake naotesha fensi then hatua moja kuja kwangu najenga ukuta
 
Yes amemsaidia upande mmoja..........Kuna wengine wana bahati anasaidiwa pande tatu zote yeye anabakiza kufunga mbele tu na kuweka geti....Ukinunua viwanja vya kupimwa ndio advantages zake hizo
Kapata mseleleko hana gharama tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…