Binafsi ninaishi kwenye nyumba ambayo ujenzi wa ukuta unaendelea. Na tumejenga ukuta katikati ya "uchochoro" - katikati ya beacon ya Halmashauri.
Hatujengi kwa shari, bali tunafuata maelekezo ya Idara ya ardhi. Idara ilituelekeza kuwa Sheria hazikatazi kujenga ukuta(fence) katikati ya ya beacon. Mita 1.5 ambayo watu wanazungumzia ni lazima uiache unapoanza kujenga nyumba (sio fence). Na chochoro zinazoachwa huwa wanasema zinaachwa kwaajili ya huduma za jamii n.k. lakini kwa mujibu wa idara ya ardhi - hakuna kitu kama hicho endapo viwanja vimepimwa na kuna barabara upande wa mbele wa kila block. Mara ya kwanza tulipeleka ramani ya fence ambayo inaacha mita 1.5 za uchochoro - wakagoma kui-approve, wakauliza hizi mita 1.5 mmeacha za nini?
Gari la zimamoto halipiti uchochoroni, ni mazoea tu kusema uchochoro ni kwaajili ya gari la fire au gari la wagonjwa. Septic tanks unatakiwa kujenga ndani ya kiwanja chako sio katikati ya beacon. Zaidi ya hayo, unapolipia kiwanja ramani haioneshi uchochoro: kwahiyo unalipia kiwanja chako chote bila kuacha hata hatua moja. Kwa maana hiyo, unaruhusiwa kukitumia chote bila kuacha hata hatua moja. Isipokuwa kuna taratibu zake kila unapotaka kuanza ujenzi ili upate vibali vya kujenga either fence au nyumba. Na kwasababu taratibu zinaanzia katika Serikali za mitaa, kibinadamu na ili kuepuka migogoro - basi huwa wanashauri kama unajenga ukuta katikati ya beacon zungumza na unayepakana nae ili mkubaliane na ikiwezekana mchangiane gharama.
Lakini ukijenga ndani ya beacon, si lazima umshirikishe jirani kwasababu unajenga NDANI ya kiwanja unacholipia.
Nyumba ninayozumgumzia ipo ndani ya Halmashauri ya Mji mmoja hapa nchini. Na wakati tunaanza kujenga ukuta majirani waliandamana, kesi ikafika mpaka kwa Mkuu wa idara ya ardhi. Akafika eneo la ujenzi na akasisitiza kwamba: kisheria fence haijakosewa, ila kibinadamu hayo ni maamuzi ya majirani kukaa chini ya kuyajenga ili kesho na keshokutwa yasije kutokea maafa ya visasi. Lakini nilichokiona ni kuwa sheria yenyewe haifahamiki na watu, kwahiyo tunaenda kimazoea zaidi kuliko kisheria.
NB: Hata mimi nasimamia huu ujenzi lakini Sheria yenyewe siijui, nafuata tu maelekezo ya Halmashauri ambayo wameyaweka kwenye kibali walichonipa.
Walichosisitiza ni kwamba; wanaruhusu kujenga ukuta katikati ya beacon kwasababu ukuta sio "permanent structure", inaweza kubomolewa kirahisi kama kukiwa na ulazima wa kufanya hivyo. Mwisho wa siku Serikali ndio inamiliki ardhi yote, yenyewe ndo inaweza kuja saa yeyote ikakwambia uondoe ukuta. Na Serikali inapozungumza, unapaswa kutii!