Jirani anajenga Msingi wa ukuta katikati ya jiwe la mpaka la manispaa, Sheria ya Ardhi inaruhusu hii?

Jirani anajenga Msingi wa ukuta katikati ya jiwe la mpaka la manispaa, Sheria ya Ardhi inaruhusu hii?

Hili nalo Mwanangu Ridhiwan na timu yako muende mkalitizame!
 
Amekengeuka.Kuna umbali maalum/kipimo katika mita alipaswa kuingia kwa upande wake ndiyo ajenge.Hiyo ni ili aache nafasi kati yake na jirani.Pia aache uchochoro/nafasi kwa ajili ya huduma za jamii kama maji,umeme na hata njia ya kupita.Mumuwahi kabla hajaziba kabisa eneo kwa kuwapa taarifa viongozi wa mtaa au Mipangomiji/Ardhi wilayani waje wampe elimu.
Kama haupo eneo husika ni mwepesi kutoa ushauri

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Habari wadau,

Nina kiwanja changu kimepimwa na manispaa ya Ubungo.

Jirani yangu naepakana nae ameamua kujenga msingi wa ukuta wake kati kati ya jiwe linalotutenganisha..

Je, yupo sahihi? Sheria ya Ardhi inaruhusu hili kutokea?

Wataalamu na wazoefu naombeni ushauri

Tazama picha. Kiwanja changu ni upande wa kushoto na cha jirani ni upande wa kulia wa beacon

Beacon iliyowekwa na manispaa ndiyo hiyo pembeni ya mti (mti ameuweka ndani ya upande wa kiwanja changu) na hayo nyuma ndio matofali ya jirani

View attachment 2371564
Ni makosa hapo,Hilo jiwe Inatakiwa liwe nje ya ukuta, nenda serikali ya mtaa katoe taarifa, au ukiona vipi potezea
 
Siyo kuombwa.Uchochoro kati ya nyumba na nyumba ni lazima uachwe kwa vipimo vyake kitaalamu.Ujenzi holela,ubishiubishi na maroho machafu huwa yanazua balaa.Mkalisheni chini mumueleze huyo mshari.Laa sivyo mbeleni atawasumbua zaidi.Wa wapi huyo jirani yako?
Siku hizi mambo hayo yakuacha uchochoro hayapo

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Amekengeuka.Kuna umbali maalum/kipimo katika mita alipaswa kuingia kwa upande wake ndiyo ajenge.Hiyo ni ili aache nafasi kati yake na jirani.Pia aache uchochoro/nafasi kwa ajili ya huduma za jamii kama maji,umeme na hata njia ya kupita.Mumuwahi kabla hajaziba kabisa eneo kwa kuwapa taarifa viongozi wa mtaa au Mipangomiji/Ardhi wilayani waje wampe elimu.
Uchochoro haupaswi kuwa kila sehemu, kuna barabara za mitaaa
 
Huu ukuta ni wa kishari shari ndio maana nauogopa.. maana viwanja vyetu ni vya mtaa wa mwisho. Nyuma yetu kuna majirani waliojenga kienyeji enyeji..

Hao watu wote watategemea mimi ndio niwaachie njia kubwa.. maana walikuja kuomba na tukaongea na jirani wote tuingie ndani mita chache ili wa nyuma wapate njia.

Sasa ghafla jirani kaanza jenga ukuta nyuma ya beacon kabisa
Ooh,huo ukuta atauvunja tu,amekosea huyo, ni mchaga huyo au? Mimi hao nawapendaga nikipakana nao, sisi Wengine machizi freshi
 
...Sasa tukupe Ushauri Gani Hapo. Wee Sema ulitaka TU kutujulisha kwamba una kiwanja!
Nikuulize wewe swali la kawaida Hapo la kutumia TU Akili... Jirani akamua kujenga Hapo, Maji ya Mvua ya Bati lake yataangukia Wapi???[emoji35]
We inaonekana Ni fukara hata makazi huna, ndiomaana una roho ya kwann
 
Jirani yetu ni mchaga naye alitufanyiaga mambo meusi kama haya, sina chuki na kabila lolote ila maeneo mengi ukipakana kiwanja na mchaga kuwa macho
Mnawapa kichwa hao mandezi, dawa nikumfanyia umafia jirani mpuuzi Kama huyo
 
Binafsi ninaishi kwenye nyumba ambayo ujenzi wa ukuta unaendelea. Na tumejenga ukuta katikati ya "uchochoro" - katikati ya beacon ya Halmashauri.

Hatujengi kwa shari, bali tunafuata maelekezo ya Idara ya ardhi. Idara ilituelekeza kuwa Sheria hazikatazi kujenga ukuta(fence) katikati ya ya beacon. Mita 1.5 ambayo watu wanazungumzia ni lazima uiache unapoanza kujenga nyumba (sio fence). Na chochoro zinazoachwa huwa wanasema zinaachwa kwaajili ya huduma za jamii n.k. lakini kwa mujibu wa idara ya ardhi - hakuna kitu kama hicho endapo viwanja vimepimwa na kuna barabara upande wa mbele wa kila block. Mara ya kwanza tulipeleka ramani ya fence ambayo inaacha mita 1.5 za uchochoro - wakagoma kui-approve, wakauliza hizi mita 1.5 mmeacha za nini?

Gari la zimamoto halipiti uchochoroni, ni mazoea tu kusema uchochoro ni kwaajili ya gari la fire au gari la wagonjwa. Septic tanks unatakiwa kujenga ndani ya kiwanja chako sio katikati ya beacon. Zaidi ya hayo, unapolipia kiwanja ramani haioneshi uchochoro: kwahiyo unalipia kiwanja chako chote bila kuacha hata hatua moja. Kwa maana hiyo, unaruhusiwa kukitumia chote bila kuacha hata hatua moja. Isipokuwa kuna taratibu zake kila unapotaka kuanza ujenzi ili upate vibali vya kujenga either fence au nyumba. Na kwasababu taratibu zinaanzia katika Serikali za mitaa, kibinadamu na ili kuepuka migogoro - basi huwa wanashauri kama unajenga ukuta katikati ya beacon zungumza na unayepakana nae ili mkubaliane na ikiwezekana mchangiane gharama.

Lakini ukijenga ndani ya beacon, si lazima umshirikishe jirani kwasababu unajenga NDANI ya kiwanja unacholipia.

Nyumba ninayozumgumzia ipo ndani ya Halmashauri ya Mji mmoja hapa nchini. Na wakati tunaanza kujenga ukuta majirani waliandamana, kesi ikafika mpaka kwa Mkuu wa idara ya ardhi. Akafika eneo la ujenzi na akasisitiza kwamba: kisheria fence haijakosewa, ila kibinadamu hayo ni maamuzi ya majirani kukaa chini ya kuyajenga ili kesho na keshokutwa yasije kutokea maafa ya visasi. Lakini nilichokiona ni kuwa sheria yenyewe haifahamiki na watu, kwahiyo tunaenda kimazoea zaidi kuliko kisheria.

NB: Hata mimi nasimamia huu ujenzi lakini Sheria yenyewe siijui, nafuata tu maelekezo ya Halmashauri ambayo wameyaweka kwenye kibali walichonipa.

Walichosisitiza ni kwamba; wanaruhusu kujenga ukuta katikati ya beacon kwasababu ukuta sio "permanent structure", inaweza kubomolewa kirahisi kama kukiwa na ulazima wa kufanya hivyo. Mwisho wa siku Serikali ndio inamiliki ardhi yote, yenyewe ndo inaweza kuja saa yeyote ikakwambia uondoe ukuta. Na Serikali inapozungumza, unapaswa kutii!
 
Habari wadau,

Nina kiwanja changu kimepimwa na manispaa ya Ubungo.

Jirani yangu naepakana nae ameamua kujenga msingi wa ukuta wake kati kati ya jiwe linalotutenganisha..

Je, yupo sahihi? Sheria ya Ardhi inaruhusu hili kutokea?

Wataalamu na wazoefu naombeni ushauri

Tazama picha. Kiwanja changu ni upande wa kushoto na cha jirani ni upande wa kulia wa beacon

Beacon iliyowekwa na manispaa ndiyo hiyo pembeni ya mti (mti ameuweka ndani ya upande wa kiwanja changu) na hayo nyuma ndio matofali ya jirani

View attachment 2371564
hii siyo sawa hata kidogo, anatakiwa aache jiwe pembeni
 
Yes amemsaidia upande mmoja..........Kuna wengine wana bahati anasaidiwa pande tatu zote yeye anabakiza kufunga mbele tu na kuweka geti....Ukinunua viwanja vya kupimwa ndio advantages zake hizo.
Kweli mkuu, kuishi karibu na matajiri unanufaika na vingi mi mmojawapo wa mnufaika wa hilo,

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Bado upo kulekule.Inategemea mchoro wa ugawaji viwanja na aina ya ujenzi unaotakiwa.Kumbuka:Jamaa wapo squatter area.Usiwe mwepesi wa kufikia mwisho ukaacha kiini.
Shida yako maelezo yako yamekaa kilayman kishamba, hujui vitu una lazimisha kujua

Tuna kuelekeza lakini wapi ubishi mwingi... wewe ndio chanzo cha migogoro... watu wa aina yako ndio chanzo cha migogoro...
 
Hapo ni sawa ama unataka ajenge ukuta ndani ya kiwanja chake na wewe ujenge ndani ya kiwanja chako ili kuwe na kichochoro katikati? Hii style ndio tunatumia mtaani kwetu aliyeanza kujenga ukuta anaongea na jirani yake ukuta unapita katikati ya mpaka.
 
Huu ukuta ni wa kishari shari ndio maana nauogopa.. maana viwanja vyetu ni vya mtaa wa mwisho. Nyuma yetu kuna majirani waliojenga kienyeji enyeji..

Hao watu wote watategemea mimi ndio niwaachie njia kubwa.. maana walikuja kuomba na tukaongea na jirani wote tuingie ndani mita chache ili wa nyuma wapate njia.

Sasa ghafla jirani kaanza jenga ukuta nyuma ya beacon kabisa
Wahi wamepa itakuumiza baadaye kuna watu wengine akili zao hutumika kuanzia miguuni kwenda kichwani
 
Back
Top Bottom