Jirani anajenga Msingi wa ukuta katikati ya jiwe la mpaka la manispaa, Sheria ya Ardhi inaruhusu hii?

FRESHMAN Inategemea na muundo wa block yenu. Kama ipo kama hii picha ilivyo kwa maana kwamba viwanja vyenu vipo "mkabala", basi jirani yupo sahihi na kakusaidia kujenga fence.View attachment 2371604
Wengi ni wabishi wasio elewa mambo yapoje bila kutaka kujielimisha

Et ktk hizo plots uache chocholo ya 1.5 kushoto na kulia

Kuna watu wana hitaji elimu haswa
 
Nafasi inaachwa mita 1 kutoka katika jengo la makazi na boundary ya kiwanja ili kuzuia maji ya mvua yasimdondokee jirani.
Fence inajengwa kufuata mchoro wa halmashauri na kwa jinsi picha inavyoonyesha hapo huyo jirani yupo sahihi. Ila napata mashaka kama kweli ni kiwanja chako
 
Huo ndio ushauri! Hapo juu, jamaa hawajui chochote, badala ya kupiga kimya, wao wameamua kujivua nguo!
Tafuta shule ya mipango miji ukasome Au ingia wizara ya ardhi Au ktk bodi ya mipango miji kajielimishe

Elimu haina mipaka ndugu

Ukiuliza kwa nini zenji tuna weza zalisha viwanja vya kumi kwa kumi lakini huku bara haiwezekani na hizo setbacks za 1.5 zina tofautiana kwa upande na upande sasa jiulize yale mabanda yenu mnayo yajenga ukutani/fensi huwa mnajenga kwa sheria Au taratibu zipi?

Huyo atakaye enda kumshitaki ataonekana kituko pale ofisi ya ardhi na watapata fursa ya kumpga sababu ni layman
 
Sio kweli
Hakuna njia hapo baina ya viwanja viwili vinavyopeana ubavu
Huyo jamaa ni mbishi anataka Kiwanja kiwe kisiwa Au kiwe na double access wakati kitu kimoja wapo ktk mipango miji ni kuondoa hilo
 
Hivi mnatoa wapi hizi stori?
Ununue kiwanja cha 20*20 afu uje na mbwembwe za mita mbili kila upande?
Mnazalisha mapito ya vibaka

Wkt barabara kwny ramani zinaonekana
Wajinga na wajuaji ni wengi hivyo serikali ina kazi kubwa sana kupambana na hawa watu wa aina hii wasio jua taratibu zipoje na wana nunua viwanja wamemaliza
 
Habari wadau,

Nina kiwanja changu kimepimwa na manispaa ya Ubungo.

Jirani yangu naepakana nae ameamua kujenga msingi wa ukuta wake kati kati ya jiwe linalotutenganisha..

Je, yupo sahihi? Sheria ya Ardhi inaruhusu hili kutokea?

Wataalamu na wazoefu naombeni ushauri

Tazama picha. Kiwanja changu ni upande wa kushoto na cha jirani ni upande wa kulia wa beacon

Beacon iliyowekwa na manispaa ndiyo hiyo pembeni ya mti (mti ameuweka ndani ya upande wa kiwanja changu) na hayo nyuma ndio matofali ya jirani

View attachment 2371564
Naona kaamua kumega eneo lako kama mrusi anavyoimega ukraine.
 
Uliwahi kujenga Kate?Au ulijenga tu kwa sababu hakuna aliyekughasi ukaona upo sawa?Jielimishe "dugu yangu"?Unajua hata kuhamia kwenye nyumba yako uliyoijenga kunahitaji leseni?Uliwahi kudodosa au kuiona mkuu?
Unacho zungumzia wala ukijui

Setbacks kila upande

Kulia kutoka ktk fensi/ukuta Au mpaka wa kiwanja 1.5m
Kushoto kutoka ktk ukuta/fensi Au mpaka wa kiwanja 1.5m
Nyuma kutoka ktk ukuta Au fensi mpaka wa kiwanja 1m
Mbele kutoka ktk ukuta/fensi Au mpaka wa kiwanja ni 2.5m

Kwann tuna takiwa kuacha hivi?

Kwa uchache eneo litakalo bakia baada ya kutoa hizo mita ndio jengo au nyumba ijengwe, nyumba isijengwe mpkani ila fensi ndio mpaka

Sasa hizi setbacks zinawekwa kusaidia
-kupitisha miundombinu kama system za maji safi na taka,
  • umeme
  • kujenga chemba
  • kusaidia wakati wa majanga (mf. Moto usiweze sambaa kwa majilani na kusababisha mahafa zaidi, uweze zibitiwa haraka)
-parking/Open space/assembly area (ukienda sehemu kama za mabenk sheli vyuo nk wameonesha matumizi yake)

Hivyo tuelewe tujifunze tusipotoshe kama hatujui jambo
 
hapa ndiyo umejibu ki-GT

huko juu ulikua unabwatuka tu
 
Naomba maoni yako anachokifanya jirani kujenga kati kati ya beacon yupo sahihi ama hayupo sahihi?

Tazama vizuri picha inayoonesha jiwe la manispaa na matofali ya ukuta yake.

Nitashukuru ukinipa maoni juu ya hili swali langu
 
Attachments

  • 20220929_142623.jpg
    20220929_142623.jpg
    1.7 MB · Views: 17
Naomba maoni yako anachokifanya jirani kujenga kati kati ya beacon yupo sahihi ama hayupo sahihi?

Tazama vizuri picha inayoonesha jiwe la manispaa na matofali ya ukuta yake.

Nitashukuru ukinipa maoni juu ya hili swali langu
Yupo sahihi kama haja ingia eneo la mwingine
 
Mi naona amekula kiwanja chako kidogo, mlitakiwa muigawane beacon nusu nusu.
 
Acheni kudanganyana nyie yaani uache uchocjoro kwa ajili ya kibaka kuja kukuibia? ukizingatia viwanja ni 20x20m apo nikiacha uchochoro pande zote3 kiwanja kinabikia na ukubwa upu??
 
Unacho zungumzia wala ukijui

Setbacks kila upande

Kulia kutoka ktk fensi/ukuta Au mpaka wa kiwanja 1.5m
Kushoto kutoka ktk ukuta/fensi Au mpaka wa kiwanja 1.5m
Nyuma kutoka ktk ukuta Au fensi mpaka wa kiwanja 1m
Mbele kutoka ktk ukuta/fensi Au mpaka wa kiwanja ni 2.5m

Kwann tuna takiwa kuacha hivi?

Kwa uchache eneo litakalo bakia baada ya kutoa hizo mita ndio jengo au nyumba ijengwe, nyumba isijengwe mpkani ila fensi ndio mpaka

Sasa hizi setbacks zinawekwa kusaidia
-kupitisha miundombinu kama system za maji safi na taka,
  • umeme
  • kujenga chemba
  • kusaidia wakati wa majanga (mf. Moto usiweze sambaa kwa majilani na kusababisha mahafa zaidi, uweze zibitiwa haraka)
-parking/Open space/assembly area (ukienda sehemu kama za mabenk sheli vyuo nk wameonesha matumizi yake)

Hivyo tuelewe tujifunze tusipotoshe kama hatujui jambo
Unasikitisha.Umesoma komenti zangu zote au umeiona hiyo tu?Usiwe na kijiakili cha hivyo.Fuata komenti mojamoja utaona.
 
Back
Top Bottom