Jirani anajenga Msingi wa ukuta katikati ya jiwe la mpaka la manispaa, Sheria ya Ardhi inaruhusu hii?

Hebu weka site plan au ramani ya kiwanja ili tukusaidie.
 
Shida yako maelezo yako yamekaa kilayman kishamba, hujui vitu una lazimisha kujua

Tuna kuelekeza lakini wapi ubishi mwingi... wewe ndio chanzo cha migogoro... watu wa aina yako ndio chanzo cha migogoro...
Huwa mnajidai mnajuuuuuaaa!Mkifika eneo mnajijambia tu ushuzi wa ngomani.Twende site tukafanye kazi ujue hujui.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hakuna kitu sikipendi duniani kama ugomvi wa Ardhi uwa haumaliziki salama.
 
sio lazima kila baada ya kiwanja kunakuwa na uchochoro au barabara viwanja vingi tu uzio wa nyumba unakutana, suala la njia ni suala la mipango miji , kama wamepima kuna sehemu maalumu wanaacha njia , tambua kwamba sio kila baada ya kiwanja kilichopimwa wanaweka njia au barabara
 
Uchochoro haupaswi kuwa kila sehemu, kuna barabara za mitaaa
kabisa kiongozi huyo jamaa inaelekea hajatembeea maeneo yaiyopangwa vizuri kama mikocheni au masaki, kungekuwa kuna njia au uchochoro kila baada ya nyumba sijui kungekuwaje , sanasana ingeleta shida kwenye suala la ulinzi
 
upo sahihi sana na ndivyo ilivyo, honera kwa mchango wako mzuri na wa ukweli
 
Kama jiwe limewekwa na manispaa maana yake njia wataweka haohao manispaa, hivyo hapo hapapaswi kuwa na njia yoyote. Infact, sijaona kosa la jirani yako. Ukuta unaojengwa ndio mpaka wenu. Hakuna sababu ya kuja kuwa na kuta mbili kisa kuacha jiwe wazi.
 
Viwanja vilivyopimwa huwa havina huo utaratibu ndugu. Hicho unachoongea ni taratibu za kimila lkn taratibu za ardhi iliyopimwa hazina hicho unachoongea kwasababu ardhi iliyopimwa huzingatia barabara hadi miundombinu mingine kama maji na umeme
 
Uliwahi kujenga Kate?Au ulijenga tu kwa sababu hakuna aliyekughasi ukaona upo sawa?Jielimishe "dugu yangu"?Unajua hata kuhamia kwenye nyumba yako uliyoijenga kunahitaji leseni?Uliwahi kudodosa au kuiona mkuu?
Vibali vya ujenzi huwa havioneshi hivyo vichochoro unavyosema wewe labda kama umeenda kujenga maeneo yasiyopimwa ndio vichochoro ni lazima kuacha. Maeneo yaliyopimwa yanazo barabara zake. Sisi tunaojenga maeneo yaliyopimwa tunafahamu
 
Kwan ile sheria ya kuacha nusu mita sijui mita moja kutoka kwenye mpaka wako unapo taka kujenge fensi imebadirika au mazaea mabaya?

Na wewe lounge hapo hapo kaishakusaidia ukuta wa upande mmoja
Sheria za zamani sana izo, huku nchi za watu ni ukuta kwa ukuta, hivyo vichochoro bongo mnavyovitengeneza vya kuacha mita mojamoja katikati ya mpaka wabongo mko na project gani mnayotaka kuileta au anzishavna hivyo vichochoro
 
Lazma uunge ndio
Master plan inaonyesha kichochoro?
Kama hamna we unaitoa wapi?
Inaonekana hawa jamaa wanajenga sehemu zisizo rasmi ambako hakuna mipango miji ndio maana wanaongea habari za kuacha hatua. Kwa tuliojenga maeneo rasmi tunajua kuwa hakuna utaratibu wa kuacha hata hatua moja
 
Haya ndo majibu ya msomi. Wengine porojo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…