Jirani anataka kujenga nyumba Yake Kwa kutumia fensi yangu

Wakuu habari zenu,

Nipo kwenye changamoto na jirani yangu hapa anayetaka kujenga nyumba Yake Kwa kutumia fensi yangu. Upande mmoja na cha kushangaza analazimisha na Ujenzi umeshafikia level ya fensi sasa kimbembe anataka aongeze kozi kadhaa za tofali kwenye fensi yangu ambayo ninataka iishie hpo ilipo na niweke zile electric wire au urembo wa fensi ninao utaka Mimi.

Hivyo ananiharibia plan za kutengeneza fensi ninayoitaka Mimi, mbya zaidi Niko mbali na nyumbani, kwani nyumba nimeijenga huko kanda ya ziwa na Mimi Niko hapa mjin Dar. Ninapomuambia asubiri nirudi ili nione anachotka kufanya anakuwa haelewi...

Kwa mazingira haya nashindwa kumuelewa kabisa kwani kama kiwanja anacho kikubwa kuliko Mimi. Hebu nishaurini maana ugomvi sipendi lakni naona ananichokoza to the maximum.
Mwache ajenge akimaliza, nenda kabomoe fensi yako umwambie unataka kujeng upya/kubadili design.
 
Issue ya uzio wa mpakani ni mapatano ya pande mbili, hasahasa upande wa maskini unatakiwa uwe mpole zaidi 😀

Kubalianeni zile mita 2 kwa kila mtu zisiwepo ila kuwe na uwiano wa 1:3 atakayejenga fensi apate eneo kubwa zaidi, ila kama wote mko njema mnapiga hesabu ya gharama ya uzio mnatafuta wastani mnashusha kitu

Kwa case yako huenda jamaa eneo lake ni dogo ndo maana akaamua kupunguza gharama ila madhara yake ni kwamba siku akimuuzia mtu mwingine nyumba yake ujue na umiliki wa fensi yako umeenda kwamaana akitaka kutoboa dirisha la upande wako utakua huna la kufanya nenda ardhi ita wataalam mlimalize
 
Aisee, nimepatwa na msongo wa mawazo ghafla baada ya kusoma komenti humu
Mimi nilishamkubalia mwenzangu pembeni, nikidhani ni ujirani mwema
Au labda kwa vile ni maeneo ya kishua, maana nyuma yangu naye kaomba hivyo na alikuwaga DC fulani, na kila mtu ana uwanja wa kutosha, lakini siku nikiona bati zinaelekezwa navunja ukuta
 
Kwaio unasubiri hadi uone bati zinaelekezwa,sasa unadhani atazielekeza wapi kama sio kwako!! mkataze sasa hivi hakuna cha ujirani mwema hapo ,hapana na kukatalia maeneo ya kishua hua hawajengi hivyo ,hata huyo jirani angekua wa kishua asingefanya uo ujinga wake!!😕
 
Wakuu habari zenu,

Nipo kwenye changamoto na jirani yangu hapa anayetaka kujenga nyumba Yake Kwa kutumia fensi yangu. Upande mmoja na cha kushangaza analazimisha na Ujenzi umeshafikia level ya fensi sasa kimbembe anataka aongeze kozi kadhaa za tofali kwenye fensi yangu ambayo ninataka iishie hpo ilipo na niweke zile electric wire au urembo wa fensi ninao utaka Mimi.

Hivyo ananiharibia plan za kutengeneza fensi ninayoitaka Mimi, mbya zaidi Niko mbali na nyumbani, kwani nyumba nimeijenga huko kanda ya ziwa na Mimi Niko hapa mjin Dar. Ninapomuambia asubiri nirudi ili nione anachotka kufanya anakuwa haelewi...

Kwa mazingira haya nashindwa kumuelewa kabisa kwani kama kiwanja anacho kikubwa kuliko Mimi. Hebu nishaurini maana ugomvi sipendi lakni naona ananichokoza to the maximum.
Kama uliingia kwake tutajuaje?
 
Mkuu fuata ushauri wangu mimi kama kijana wako.... Usitake malumbano nenda mkakubaliane tu na huyo jirani kwamba kama anahitaji slope ya kutumia uzio wako muelekeze ni jinsi gani umepangilia mipango yako na hivyo unataka ukuta wako uonekane aje na kama anataka kuongeza urefu basi aongeze pande zingine aache pale panapoungana.
Najua hamtoshindwa kuelewana.
 
Jiran yamefika huku Tena mbona mkeo tulikubaliana we ukiwa haupo...
Anyway maongez ua yanakuepo baina ya pande mbil pale mnapokubaliana mm jiran yangu alinruhusu kutumia ukuta wake kupandsha stoo.. Tuone picha ya jins jiran alvyojenga tukushaur ktu
 
Wakuu habari zenu,

Nipo kwenye changamoto na jirani yangu hapa anayetaka kujenga nyumba Yake Kwa kutumia fensi yangu. Upande mmoja na cha kushangaza analazimisha na Ujenzi umeshafikia level ya fensi sasa kimbembe anataka aongeze kozi kadhaa za tofali kwenye fensi yangu ambayo ninataka iishie hpo ilipo na niweke zile electric wire au urembo wa fensi ninao utaka Mimi.

Hivyo ananiharibia plan za kutengeneza fensi ninayoitaka Mimi, mbya zaidi Niko mbali na nyumbani, kwani nyumba nimeijenga huko kanda ya ziwa na Mimi Niko hapa mjin Dar. Ninapomuambia asubiri nirudi ili nione anachotka kufanya anakuwa haelewi...

Kwa mazingira haya nashindwa kumuelewa kabisa kwani kama kiwanja anacho kikubwa kuliko Mimi. Hebu nishaurini maana ugomvi sipendi lakni naona ananichokoza to the maximum.
Kwa uo mlengo wako ni Bora kugawana mbao....

Namaanisha mwambie asijenge ukutani kwako bali ajenge Kwa kuacha nafasi ikiwezekana wewe bomoa na Kila mtu ajenge mwisho wa kiwanja chake....

Simple
 
Wakuu habari zenu,

Nipo kwenye changamoto na jirani yangu hapa anayetaka kujenga nyumba Yake Kwa kutumia fensi yangu. Upande mmoja na cha kushangaza analazimisha na Ujenzi umeshafikia level ya fensi sasa kimbembe anataka aongeze kozi kadhaa za tofali kwenye fensi yangu ambayo ninataka iishie hpo ilipo na niweke zile electric wire au urembo wa fensi ninao utaka Mimi.

Hivyo ananiharibia plan za kutengeneza fensi ninayoitaka Mimi, mbya zaidi Niko mbali na nyumbani, kwani nyumba nimeijenga huko kanda ya ziwa na Mimi Niko hapa mjin Dar. Ninapomuambia asubiri nirudi ili nione anachotka kufanya anakuwa haelewi...

Kwa mazingira haya nashindwa kumuelewa kabisa kwani kama kiwanja anacho kikubwa kuliko Mimi. Hebu nishaurini maana ugomvi sipendi lakni naona ananichokoza to the maximum.

Kaka pole Sana, haya yalishanikuta jirani alikuta tayari nimeshamaliza nyumba yangu safi na ukuta safi pande zote nne. Akajenga wa kwake na upande mmoja akatumia wa kwangu bure kabisa, sasa uwanja wangu hupo chini na kwake ni juu, kwa kweli nilijenga kozi za tofari zaidi ya 9 akasema niongeze eti kwake pafupi, nikaongeza kozi 2. Bado akawa anaomba niongeze tena. Nikamwambia wewe ni mtoto wa kiume au vipi unamwambiaje mwanaume mwenzako akujengee ukuta bure kabisa [emoji3][emoji3]
 
Jiran yamefika huku Tena mbona mkeo tulikubaliana we ukiwa haupo...
Anyway maongez ua yanakuepo baina ya pande mbil pale mnapokubaliana mm jiran yangu alinruhusu kutumia ukuta wake kupandsha stoo.. Tuone picha ya jins jiran alvyojenga tukushaur ktu
Mbeba Lawama una tabu[emoji23][emoji23]
 
Ushauri wa wengi humu ni kuchochea ugomvi, hakuna mwenye hekima ya suluhu.... kama ndo mawazo halisi haya majirani mnaishi kwa chuki sana.
 
kwaio unasubiri hadi uone bati zinaelekezwa,sasa unadhani atazielekeza wapi kama sio kwako!! mkataze sasa hivi hakuna cha ujirani mwema hapo ,hapana na kukatalia maeneo ya kishua hua hawajengi hivyo ,hata huyo jirani angekua wa kishua asingefanya uo ujinga wake!!😕
Aisee , ni hatari
Ni hivi mimi nilijenga msingi tu, akasema atapandisha uwe ukuta kwa upande wake, nikasema poa na ikanipa na mimi nguvu na nilamalizia ukuta wote kuzunguka, kwa hiyo alitumia tofali zake juu ya msingi wangu.
Ila huyu wa nyuma anasema ajenga kibanda cha kuhifadhi vifaa huku ujenzi ukiendelea, anasema ataondoa akimaliza ujenzi, bado hajaanza, mimi nikiona to bati zinachomokea kwangu nalianzisha, labda ajenge ya kibanda cha mabati
 
Kiwanja kimepimwa?
Kama kimepimwa je uliacha mita 1.5 kutoka kwenye jiwe la mpaka?
Kama uliacha hiyo mita 1.5 basi anakuingilia angalia sheria inasemaje. Iwapo viwanja havijapimwa pia je ulijenga fensi kwenye mpaka kabisa au ikoje?
Kujenga ukuta wa uzio uache mita 1.5?, mbona ni kubwa sana mkuu.
 
Wastani ni mita mbili kila upande, Sheria za ujenzi na ardhi zinataka hivyo. Malengo ya hili suala ni mengi ka vile kupata accessibility ya magari ya zimamoto wakati wa ajali za moto, way leave ya mtandao wa umeme, maji safi na maji taka, gas pipeline, kudhibiti kusambaa kwa ajali za moto kwa majirani, etc.
Tukumbuke kwamba viwanja huwa vinapitiwa na barabara mbele. Usikute hizo mita 2 ni kutoka mpaka wa kiwanja hadi jengo la nyumba linapoanzia na siyo ukuta wa uzio.
 
Back
Top Bottom