Pole kwa kadhia ya jiranyako.
Kwanza huo ukuta ni WA kwako ama wa kwenu?
Ukuta ni unakuwa WA kwako kama umejenga Kwa kuacha nafasi walau mita 2 kutoka jiwe la mpaka Ili na yeye ajenge wa kwake Kwa kuacha umbali huohu kutoka kjiwe lenu la mpaka.
Ukuta unakuwa wa kwenu wote kama mmekubaliana msiache kichochoro bali mjenge kufuata mpaka wa jiwe. Hapa haijalishi mmechangia ama amejenga mmoja wenu. Ilimradi hakuna nafasi iliyoachwa basi baina ya jiwe la mpaka basi huo ukuta unakuwa WA kwenu wote na kila mtu ana haki ya kuutumia.
Kama utataka jirani mkorofi asitumie ukuta wako, vunja huo na jenga mwingine Kwa kufuata Sheria.
Isije kuwa unamwonea wivu huyo jirani yako Kwa sababu unaona anakupiga gepu Kwa kumiliki mang'ombe, maana majirani hampendagi kupitwa.
Ngombe wake wako upande wake na wanachafua ukuta huo upande wake Sasa wewe shida Nini? Kama ukuta utaanguka ama kuharibika sehemu aliyojenga banda basi gharama za matengenezo ziatoka kwake.
Jirani punguza wivu, relax, ongea na jirani yako nawe jifunze ufugaji kutoka kwake baada ya hapo hutajuta kupata jirani mfugaji bali atakuwa baraka kwako