Misri haiwezi wapokea Wapalestina wa Gaza sababu Hamas ilianzishwa na Muslin Brotherhood ambao wana msimamo mkali. Angalau ingeweza kuwapokea kama wangetoka West Bank.
Muslim Brotherhood imepigwa marufuku Misri na Saudi Arabia, ni kama kundi la kigaidi na Rais pekee kutoka kundi hilo pale Misri akipinduliwa na El-Sisi wa sasa, akafia jera kwa kesi za kusingiziwa.
Serikali ya Misri lazima iwaogope wasije lipiza kisasi. Wapalestina ndio walimuua Anwar Sadat aliposaini mkataba wa amani na Israel. Walitaka aendelee kupigana vita aumize nchi yake kisa wao, hawakuona kwamba Misri uwezekano wa kuishinda Israel haupo wao wanalazimisha ijitoe mhanga.
Kule Jordan walitaka kumuua King Hussein mara mbili. Wakamuua Waziri Mkuu wake. Wakawa wanatembea na silaha barabarani na wanazozana na jeshi. Wakapiga marufuku polisi au jeshi kufanya patrol kwenye kambi zao, wakati ziko Jordan. Wakaanza mashambulizi ya kigaidi na kuteka Wayahudi wakiwa Jordan.
Nchi ikaanza kumshinda King Hussein alipoamua kuwashambulia ikatokea Syrian Army imekuja kuivamia Jordan kuwatetea. Jordan ikapiga Syrian Army sababu haikuwa na cover ya Air Force mkuu wake alikataa kwenye mzozo wa ama waende ama wasiende, mkuu wa Air Force pale Syria alikuwa Hafez al Assad akaipindua serikali kwenye harakati za mgogoro huo. Ona sasa Wapalestina wakasababisha mapinduzi Syria.
Iraq ilitaka kupeleka jeshi kusaidia Wapalestina wapigane na Jordan. Waziri wa Ulinzi akakataa (third in command kwa serikali ile). Saddam Hussein alikuwa na wivu na anataka apande vyeo baadae afanye mapinduzi. Akamuua yule Waziri kisa Wapalestina, akawa ndiye third in command baadae akaipindua serikali. Hajawahi leta kiherehere kwao tena akawa busy kupigana na Iran. Ona hapo Wapalestina walisababisha Waziri auwawe na serikali ipinduliwe pale Iraq.
Kule Jordan wakatimuliwa wakaenda Lebanon. Wakaanzisha vita, nchi ikawa maskini mpaka leo tabu tupu. Wakati Lebanon ilikuwa nchi ya Kiarabu yenye Ufaransa flani ndani yake. Wakristo na Waislamu wanaishi vizuri sana. Leo nchi imekufa kisa Wapalestina.
Hapohapo Palestina mwaka 2007 walikuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Fatah na Hamas. Fatah na Mahmoud Abbas ikabaki West Bank, Hamas na Haniyeh ikabaki Gaza. Hamna Mwarabu mwendawazimu atawapokea, wacha waende kwenye kisingizio cha "wabaki uko ili Israel isichukue ardhi yao".