JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
“Tunasikitika kufuta mikataba ya vijana 854 wa JKT kutokana na kufanya vitendo vya uasi.”Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania - Jenerali Venance Mabey
----------



Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Mabeyo amesema wamefuta mikataba ya Vijana 854 wa JKT ambao ni miongoni mwa walioahidiwa kupewa ajira kwa kujenga Ikulu, Chamwino na hii ni kutokana na Vijana hao kufanya uasi kwa kugoma na kuandamana kwenda Ikulu.

My take; Gharama kubwa zilizotumika kuwaandaa hao vijana ili kuja kulitumikia taifa zinarejeshwa vipi?

Pia, soma:

1). Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi awasamehe waliofukuzwa JKT, watakiwa kurudi jeshini
 
Nimesoma habari moja kuwa JKT imesitisha mikataba na kuwafukuza vijana zaidi ya 800 baada ya kuandamana Ikulu wakinishinikiza kuajiriwa

Baada ya hao vijana kuja mtaani,wanajua kushika silaha na mafunzo ya awali ya kujihami,je hao vijana hawawezi kujiunga na vikundi vya kigaidi kama cha ISS huko Msumbiji?

Je serikali inawafuatilia hao vijana zaidi 800 mienendo yao mitaani kama sio rahisi kushawishika kujiunga na vikundi vya kigaidi kwa ukosefu wa ajira na kuleta majanga nchini?

Au unaweza ukawa mtego,wakashawishiwa kugoma wadai ajira ili watimuliwe wakajiunga na ISS huko Msumbiji


Serikali ibuni mikakati ya kuajiri vijana au kuwawezesha kupata mazingira rahisi kujiajiri ili kuepuka kushawishika kuvuka mpaka kule kusini na kujiunga na ISS

Narudia kuwatimua vijana 800 JKT ni hatari zaidi kwa usalama uliopo kusini mwa Afrika
 
Nimesoma habari moja kuwa JKT imesitisha mikataba na kuwafukuza vijana zaidi ya 800 baada ya kuandamana Ikulu wakinishinikiza kuajiriwa

Baada ya hao vijana kuja mtaani,wanajua kushika silaha na mafunzo ya awali ya kujihami,je hao vijana hawawezi kujiunga na vikundi vya kigaidi kama cha ISS huko Msumbiji?...
Boss kijeshi kugoma ni UASI hiyo haikuabariki askri anapogoma hizo ni ishara mbaya hata kwa usalama wako wewe binafsi na nnchi kwa ujumla jambo la pili wao kujiunga na iss sio rahisi kama unavyofikiria hyo organization wanaitoa wapi?

Kwani vijana wangap wanarudi toka huko jkt kwa sabab hawa sio wa kwanza hicho kitendo cha mgomo ni hatri hata mimi sijakiunga mkono.
 
Boss kijeshi kugoma ni UASI hiyo haikuabariki askri anapogoma hizo ni ishara mbaya hata kwa usalama wako wewe binafsi na nnchi kwa ujumla jambo la pili wao kujiunga na iss sio rahisi kama unavyofikiria hyo organization wanaitoa wapi? Kwani vijana wangap wanarudi toka huko jkt kwa sabab hawa sio wa kwanza hicho kitendo cha mgomo ni hatri hata mimi sijakiunga mkono
Vijana 800 ni wengi,je walivyotimuliwa kuna ndinga walikuwa wanapandishwa na kupelekwa kwao,maana kuwepo mjini kimakundi wanaweza kushawishika kufanya lolote maana sasa ataona maisha hayana maana,kama kudai ajira imekuwa nongwa basi wakajiunge na ISS ,hivi unadhani mawazo hayo hawana kwa makundi hayo yaliyopo mtaani,? Unless kama kila mtu alkuwa anarudishwa kwao mmoja mmoja
 
Ni vyema jeshi wakaona haja ya kurecruit hao vijana pindi kunapokua na uhitaji kuliko kuwapa mafunzo na kuwapigisha mzigo for years bila kuwa na uhakika wa kuwapa hizo ajira.
 
Hayo ni mawazo yako lakini wengine tuna fikra kinyume kidogo na za kwako kwani huenda hao vijana wakajiajiri wenyewe, wengine wakawa watumishi wa nyumba za ibada wengine wakajitolea kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali hata kuanzisha kampuni binafsi za ulinzi hivyo ni lazima tuwe na dhana njema kwa wenzetu na sisi ndiyo inabidi tuwasihi wawe na maadili mema katika jamii, maisha yanataka ustahamilivu na tatizo la ajira ni tatizo sugu na kubwa nchini serikali na watu binafsi hawana budi kuliangalia kwa jicho la upekee hili tatizo lakini utovu wa nidhamu kwa kuandamana kushinikiza serikali na kwenda hadi ikulu lina tafsiri pana sana kuliko kuwapogopa hao magaidi.
 
Vijana 800 ni wengi,je walivyotimuliwa kuna ndinga walikuwa wanapandishwa na kupelekwa kwao,maana kuwepo mjini kimakundi wanaweza kushawishika kufanya lolote maana sasa ataona maisha hayana maana,kama kudai ajira imekuwa nongwa basi wakajiunge na ISS ,hivi unadhani mawazo hayo hawana kwa makundi hayo yaliyopo mtaani,? Unless kama kila mtu alkuwa anarudishwa kwao mmoja mmoja
Jeshini hakunaga mgomo ilo ni kosa kubwa sana,
halafu hao 800 ni wachache sana jombaa, vijana wa jkt mbn wapo wengi sana mtaani
 
Back
Top Bottom