JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

JKT yasitisha Mikataba ya Vijana 854 waliofanya Uasi

Kugoma jeshini ni swala ambalo halikubaliki. Pili JKT siyo sehemu ya kwenda kuajiriwa unaenda kufundishwa stadi mbalimbali za maisha, ukakamavu na uzalendo.

Zipo OP kadhaa hapo nyuma wamerudishwa majumbani je mpaka sasa umeona vipi? Mpaka kufikia hatua unarudishwa ishafanywa tathimini kubwa sana. Walichokipata ni intro tu vitamu uanzia RTS na kuendelea.
 
Hayo ni mawazo yako lakini wengine tuna fikra kinyume kidogo na za kwako kwani huenda hao vijana wakajiajiri wenyewe, wengine wakawa watumishi wa nyumba za ibada wengine wakajitolea kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali hata kuanzisha kampuni binafsi za ulinzi hivyo ni lazima tuwe na dhana njema kwa wenzetu na sisi ndiyo inabidi tuwasihi wawe na maadili mema katika jamii, maisha yanataka ustahamilivu na tatizo la ajira ni tatizo sugu na kubwa nchini serikali na watu binafsi hawana budi kuliangalia kwa jicho la upekee hili tatizo lakini utovu wa nidhamu kwa kuandamana kushinikiza serikali na kwenda hadi ikulu lina tafsiri pana sana kuliko kuwapogopa hao magaidi.
Ukosefu wa ajira ,ajira ,ajira na kunyima haki,uonevu ni chanzo cha kuibuka kwa vikundi vya kigaidi duniani,Note my words
 
Vijana 800 ni wengi,je walivyotimuliwa kuna ndinga walikuwa wanapandishwa na kupelekwa kwao,maana kuwepo mjini kimakundi wanaweza kushawishika kufanya lolote maana sasa ataona maisha hayana maana,kama kudai ajira imekuwa nongwa basi wakajiunge na ISS ,hivi unadhani mawazo hayo hawana kwa makundi hayo yaliyopo mtaani,? Unless kama kila mtu alkuwa anarudishwa kwao mmoja mmoja

Mkuu unatakiwa kujua wao sio wakwanza kurudi nyumban afu hawa 800 ni wachache mnoo kama ulikuwa hujui hawa wamejifungia ajira za majeshi watakaa wazisikie tuu wamejitia doa. Haya mawazo ya kujiunga ISS wewe ndyo unawasemea ??
 
Sawa jiaminishe ivyoivyo watakapo anza kuchinja ovyo watu mtaani ndo utajua umuhimu Wa kuwaajiri hawa vijana.
Watu waliopitia mafunzo ya kijeshi ni wengi sana Tanzania, hao Iss tutawagawana kabla hata ya Mapolisi hawajaingilia kati

Tulivyopinda hivi halafu mtu aje na kilemba kutushurutisha,Magufuli mwenyewe kashindwa
 
Unajua wao wamepanic tuu kwa huu upepo wa saiz lazima wangeajiriwa tuu wamekosa subrah
Hukuna ajira za kutosha vijana wote hao.
Hao jamaa wamekua wakipigwa dana-dana na kufanyishwa makazi magumu kuanzia ujenzi wa ukuta wa mirerani na ahadi hewa kila kukicha.
 
Ni vyema jeshi wakaona haja ya kurecruit hao vijana pindi kunapokua na uhitaji kuliko kuwapa mafunzo na kuwapigisha mzigo for years bila kuwa na uhakika wa kuwapa hizo ajira.
Hao wanafundishwa stadi za maisha na siyo mafunzo ya kijeshi. Mafunzo ya kijeshi ni miezi 9, hao wanakaa zaidi ya mwaka
 
Hukuna ajira za kutosha vijana wote hao.
Hao jamaa wamekua wakipigwa dana-dana na kufanyishwa makazi magumu kuanzia ujenzi wa ukuta wa mirerani na ahadi hewa kila kukicha.

Ni kweli mkuu lakini unatakiwa kuelewa kuwa tawala zinabadilika Jakaya alikuwa anaajiri sana vijana ilifika hatua vijana wa jkt wanachagua jeshi la kujiunga
 
Back
Top Bottom