Job Ndugai akutana na Rais Samia Ikulu Dodoma
Chief Hangaya baada ya Kutoka Kwao Zanzibar amekutana na kuzungumza na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) aliyefika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Chief Hangaya kesho ana Kikao na Mawaziri na Manaibu Mawaziri Ikulu Chamwino.

Pia soma;


====

RAIS SAMIA AKUTANA NA JOB MDUGAI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai (Mb) Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo January 12,2022
View attachment 2078328
Ukiangalia "body language" hasa ya Job Ndugai, ni dhahiri hiyo picha imelazimishwa, Kwa hiyo hata hayo mazungumzo yalikuwa ya kulazimisha.
 
MHE. RAIS SAMIA AKUTANA NA NDUGAI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Leo Jumatano Januari 12, 2022 amekutana na kuzungumza na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) aliyefika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

#NyukiWaMama

View attachment 2078404
Tutamsikia Rais Samia, akitueleza kuwa hata yeye Ndugai, atampa Kazi maalum!

Nimeamini kuwa CCM kweli ina wenyewe, ambao ndiyo wanaostahili kupewa vyeo ndani ya nchi hii, hata wakiharibu namna gani, hao hawataguswa!
 
Siujui kwanini nilisita kulisema hili hapa JF kwani lilinijia kichwani tangu jana kuwa linaweza kutokea

Nilichotaka kusema ni uwezekano wa Ndugai kuitwa Ikulu kwa lengo la kupozwa na kupigwa picha ya pamoja kama hii ili kuonyesha umma kuwa Mama na Spika wako pamoja.

Nilipanga pia kumuonya Mama kuwa Ndugai ataitikio wito kwa heshima ya Raisi tu ila moyoni teyari ana kinyongo.

Ndugai hawezi kumuunga mkono huyu Mama ingawa kwenye public anaweza kuongea kuonyesha hana kinyongo nae.

Under certain circumstances, it is very easy to foresee or predict negative things that our politicians are like to do or say. But under the same or different circumstances, it is very difficult to predict or foresee positive things that our politicians are likely to do or say.
Picha yenyewe inajitosheleza jamaa kanunaa.
 
Kama habari za Tundu Lisu ni za kweli basi Ndugai alienda kuenjoi Ikulu. Tundu Lisu anatuhabarisha kwamba Ndugai anadai kwa mujibu wa sheria gari jipya, mafuta lita 70 kwa wiki mpaka anakufa, dereva anayelipwa na serikali mpaka kufa, kiinua mgongo, gharama za kufungasha virago, gharama za service ya gari mpaka anakufa n.k
 
Naona hujui pictorial interpretation.

Binafsi ukiangalia hii picha kama mama ana hofu na soni kumtazama Job..Huku Job akiwa na ham sana ya kumshika mkono mama ila mama naye hana "Time" naye kabisa .


Ni kama kuna juhudi za kuwaunganisha pamoja ila wote wanaonekana wamelazimuahwa.

Hakuna inner willing ya wahusika kumaliza tofauti zao.

Nawaza tu kuliingana na picha!!


Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
NDUGAI kakoseewa sna na adabu uwezi nichamba vile alfu utake tupige picha public kbsa aisee hata mm ningenuna tu cwez kenua meno kwa. Mtu alikwisha niudhi na kunidhalilisha
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Kweli jamaa atakuw hana vidole, hiyo simamia yake hiyo,
Sio
 
Back
Top Bottom