TANZIA GE2025 Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

TANZIA GE2025 Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
DODOMA: Spika Mstaafu na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia, leo Agosti 6, 2025, taarifa ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Dkt. Tulia Ackson imeeleza kuwa msiba umetokea Dodoma

Dkt. Tulia amesema Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Tuliwaambia hawakutaka kutusikiliza ngoja wawamalize Watanganyika ili nchi ibaki ya Wazanzibar pekee.
 
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki Dunia leo August 06,2025 akiwa anaendelea kupatiwa matibabu Hospitalini baada ya kuugua ghafla. Ndugai amekuwa Spika wa Bunge tangu November 17, 2015 hadi Januari 06, 2022 alipojiuzulu na kuendelea kuwa Mbunge wa Kongwa nafasi ambayo ameendelea kuitetea kwa kuchukua fomu tena mwaka huu ambapo ameshinda kwenye kura za maoni. Ndugai ambaye amezaliwa January 22,1960 alishinda kura za maoni za Ubunge wa Jimbo la Kongwa kwa kupata kura 569
View attachment 3434043
Bora katupunguzia gharama za matibabu yake. Maana akienda India anatutia hasara kweli.

Pia malipo yake ya uspika ilikuwa ni hasara tupu.
 
Kifo ni hakika isiyopingika. Ni safari ya mwisho ya kila kiumbe hai. Haijalishi uko wapi, una nini, au ni nani siku moja utakutana na mwisho wa maisha haya ya duniani.

Hili ni jambo ambalo linapaswa kutufanya tusimame na kutafakari: Tumejiandaa vipi kwa ajili ya kifo?
 
Back
Top Bottom