tweenty4seven
JF-Expert Member
- Sep 21, 2013
- 15,863
- 19,626
Sasa mtu mwenye marukanga toka lini akawa timamu,ndio spika kilaza kuwahi kutokea nchini.
Anashindia mbolea ndio aendelee kuishi
Anashindia mbolea ndio aendelee kuishi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Cd4 hamna angalia uso umemvimba kama churaSpika anaharibu. Anaongea kwa chuki. Hajui kwamba anaharibu! Anaulizwa kwa nini Naibu Spika asitoke upinzani, yeye anamuongelea Mbowe! Shame! Shame!
Kastaafu na marukanga yake,uso umevimba kwa kubugia mboleaSema Spika mstaafu!
Aibu hii.Hii Interview ya Leo 360 wamejua kuitendea haki. Ndugai anaulizwa maswali anajibu ambacho hakuulizwa.. Anakazana na Mbowe.. Mbowe na Kundi lake.
Hassana Ngoma mwishoni anamuuliza Bunge lake limekuwa kama linakandamizwa na Serikali na Bunge ni Mhimili unaojitegemea.. Anajibu eti kipindi chake cha Bunge wamefanikiwa kutengeneza kumbi za mikutano hapo hapo Bungeni na siyo kwenda UDOM au CBE Kama miaka ya nyuma.. Pia wameweka na lifti kwenda Ghorofa ya Nne..Swali analoulizwa na Majibu ni tofauti.. Hadi Aibu...
Sent using Jamii Forums mobile app
Ubinafsi huo ndio umeua mataifa mengi.Hata ukimchukia haisaidii chochote sana Sana itakuzeesha na kukusabsbishia makunyanzi usoni. Raha jipe mwenyewe
NGAWETHUKushindwa ubunge ni kuaibika? Si atabaki kuwa Mwenyekiti wa chama chake? Na hata yanayofanyika yanampa kisingizio kizuri cha kushindwa kwake. Mkurugenzi gani atakuwa na ubavu wa kumtangaza kuwa mshindi baada ya kupaniwa hivi?
Amandla...
Hata wakiendelea. Hawawezi kuacha kuimba pambio: "Alilewa chakali".Hivi polisi si bado wanaendelea na uchunguzi mbona Job kakomaa alianguka sababu ya ulevi!
Spika anaharibu. Anaongea kwa chuki. Hajui kwamba anaharibu! Anaulizwa kwa nini Naibu Spika asitoke upinzani, yeye anamuongelea Mbowe! Shame! Shame!
Clip ipi?Spika anaharibu. Anaongea kwa chuki. Hajui kwamba anaharibu! Anaulizwa kwa nini Naibu Spika asitoke upinzani, yeye anamuongelea Mbowe! Shame! Shame!
Huyo tangu atoke india hana tena weledi alio kuwa nao wakati akimsaidia mama MakindaSpika anaharibu. Anaongea kwa chuki. Hajui kwamba anaharibu! Anaulizwa kwa nini Naibu Spika asitoke upinzani, yeye anamuongelea Mbowe! Shame! Shame!
Natazama 360 Clouds naona Hassan Ngoma anambana Spika maswali mpaka anajichanganya kuhusu suala la Mbowe.
Kuhusu sheria ya habari analalamika lalamika tu kuwa wapinzani wanapendelewa na mitandao ya kijamii na waandishi wa habari.
=====
Katika Mahojiano ya Spika Job Ndungai na Clouds Media, yaliyofanyika leo Nyumbani kwake Kisasa, Jijini Dodoma na Spika amesema haya;
“Tulifika mahali ambapo live camera ikaliharibu bunge, watu wakawa wanatukana, wanakuwa na tabia mbaya. Unakuta mmekubaliana kabisa kwenye kamati kila kitu, jambo lile lile likiingia bungeni inakuwa kama mchezo wa kuigiza” - Mhe Ndungai
“Hata kwa Mabunge ya nchi zilizoendelea kama Uingezereza si kweli kwamba ni live kihivyo, wanaicheleweshea kama dakika mbili au tatu kati ya kinachotokea live na kinachokuwa live wanajaribu ku-edit kidogo vitu ambavyo ni aibu kwa taifa” - Mhe Ndungai
“Ni ukweli usiopingika kwamba yako mambo Watanzania hawayajui na huwa hatupendi sana kusema ni kweli baadhi ya wabunge na hasa hao wenye fujo baadhi yao wanatumia madawa ya kulevya, wanatumia bangi, baadhi yao wanakunywa konyagi au gongo gani, wanakuja pale sio yeye” -Mhe Ndungai
“Tulifika mahali ambapo tumewafungia wabunge wengine mwaka mzima asirudi bungeni, mbunge mwingine mnampeleka kwenye kamati ya maadili anaenda anawaambia mimi nimefanya na nikipata nafasi narudia tena na msinisamehe na viadhabu vyenyewe kwenye vitabu ni vidogo” - Mhe Ndungai
“Nitumie nafasi hii kuwaomba vyombo vya habari, tumekuwa tukikuza watu wa hovyo, waropokaji ndio wanakuzwa kuonekana ni heroes. Bahati nzuri naamini wapiga kura watawachuja watu wengi katika hawa maana hamna walichokifanya jimboni” - Mhe Ndungai
“Hakuna ambalo sikufanya kumsaidia Tundu Lissu siku ya tukio nilikuwa Dar nilipotua Dodoma nikaenda Hospitali tuka-mobilize madaktari waliokuwepo Mhe Mbowe na wenzake wakasema si kweli kwamba hawaamini Muhimbili bali ili wapate amani ya moyo wanaomba wampeleke Nairobi”-Mhe Ndugai
“Sijawahi kuongea na Tundu Lissu kwa simu kwa sababu namjua namfahamu vizuri ni mtu ana imani zake fulani na mapambano, ana ruti yake anayoiendea ambayo yeye ndio anaweza kuielewa vizuri zaidi na anaona sisi wengine ni mashetani, mtu aina hiyo unampa amani, unamuacha”- Mhe Ndugai
“Bunge la 9 wakati wa kina Mzee Slaa palikuwa na wapinzani ambao walikuwa wakifanya kazi yao, walikuwa wanashusha hoja ambazo tukikaa pembeni kama CCM tunaambiana kuwa tunaharibiana” - Mhe Ndugai
Nipo Mkuu nami pia apa natazaman naona wanamuuliza swali la Tundu Lissu hapa?
Akimbana sana Jamaa ataishia tu kusema nilitoka familia Maskini saana,nilitembea Km 8 kwenda Shule na nilishinda njaa sana mimi.
Yani anafanya kumuattack tu mbowe kila swali analoulizwa, mara hakupigwa alianguka ni story nilizosikia yani anaongea naye hana uhakika. Mara alilewa chakali.