Job Ndugai: Sijawahi kumjulia hali Tundu Lissu kwani ananiona kama shetani | Mbowe asikimbilie Urais kuficha aibu ya kushindwa Ubunge

Job Ndugai: Sijawahi kumjulia hali Tundu Lissu kwani ananiona kama shetani | Mbowe asikimbilie Urais kuficha aibu ya kushindwa Ubunge

Sasa mtu mwenye marukanga toka lini akawa timamu,ndio spika kilaza kuwahi kutokea nchini.
Anashindia mbolea ndio aendelee kuishi
 
Hii Interview ya Leo 360 wamejua kuitendea haki. Ndugai anaulizwa maswali anajibu ambacho hakuulizwa.. Anakazana na Mbowe.. Mbowe na Kundi lake.

Hassana Ngoma mwishoni anamuuliza Bunge lake limekuwa kama linakandamizwa na Serikali na Bunge ni Mhimili unaojitegemea.. Anajibu eti kipindi chake cha Bunge wamefanikiwa kutengeneza kumbi za mikutano hapo hapo Bungeni na siyo kwenda UDOM au CBE Kama miaka ya nyuma.. Pia wameweka na lifti kwenda Ghorofa ya Nne..Swali analoulizwa na Majibu ni tofauti.. Hadi Aibu...

Sent using Jamii Forums mobile app
Aibu hii.
 
Kushindwa ubunge ni kuaibika? Si atabaki kuwa Mwenyekiti wa chama chake? Na hata yanayofanyika yanampa kisingizio kizuri cha kushindwa kwake. Mkurugenzi gani atakuwa na ubavu wa kumtangaza kuwa mshindi baada ya kupaniwa hivi?

Amandla...
NGAWETHU
 
Gongo ,banging,unga na mirungi ni haramu
Tatizo ni hiyo pombe nayo pia wangeamua iwe haramu ingekuwa poa sana tungepata wawakilishi safi sana#uleviwowoteharamu
 
Kafirisika kisiasa
Natazama 360 Clouds naona Hassan Ngoma anambana Spika maswali mpaka anajichanganya kuhusu suala la Mbowe.

Kuhusu sheria ya habari analalamika lalamika tu kuwa wapinzani wanapendelewa na mitandao ya kijamii na waandishi wa habari.

=====

Katika Mahojiano ya Spika Job Ndungai na Clouds Media, yaliyofanyika leo Nyumbani kwake Kisasa, Jijini Dodoma na Spika amesema haya;

“Tulifika mahali ambapo live camera ikaliharibu bunge, watu wakawa wanatukana, wanakuwa na tabia mbaya. Unakuta mmekubaliana kabisa kwenye kamati kila kitu, jambo lile lile likiingia bungeni inakuwa kama mchezo wa kuigiza” - Mhe Ndungai

“Hata kwa Mabunge ya nchi zilizoendelea kama Uingezereza si kweli kwamba ni live kihivyo, wanaicheleweshea kama dakika mbili au tatu kati ya kinachotokea live na kinachokuwa live wanajaribu ku-edit kidogo vitu ambavyo ni aibu kwa taifa” - Mhe Ndungai

“Ni ukweli usiopingika kwamba yako mambo Watanzania hawayajui na huwa hatupendi sana kusema ni kweli baadhi ya wabunge na hasa hao wenye fujo baadhi yao wanatumia madawa ya kulevya, wanatumia bangi, baadhi yao wanakunywa konyagi au gongo gani, wanakuja pale sio yeye” -Mhe Ndungai

“Tulifika mahali ambapo tumewafungia wabunge wengine mwaka mzima asirudi bungeni, mbunge mwingine mnampeleka kwenye kamati ya maadili anaenda anawaambia mimi nimefanya na nikipata nafasi narudia tena na msinisamehe na viadhabu vyenyewe kwenye vitabu ni vidogo” - Mhe Ndungai

“Nitumie nafasi hii kuwaomba vyombo vya habari, tumekuwa tukikuza watu wa hovyo, waropokaji ndio wanakuzwa kuonekana ni heroes. Bahati nzuri naamini wapiga kura watawachuja watu wengi katika hawa maana hamna walichokifanya jimboni” - Mhe Ndungai

“Hakuna ambalo sikufanya kumsaidia Tundu Lissu siku ya tukio nilikuwa Dar nilipotua Dodoma nikaenda Hospitali tuka-mobilize madaktari waliokuwepo Mhe Mbowe na wenzake wakasema si kweli kwamba hawaamini Muhimbili bali ili wapate amani ya moyo wanaomba wampeleke Nairobi”-Mhe Ndugai

“Sijawahi kuongea na Tundu Lissu kwa simu kwa sababu namjua namfahamu vizuri ni mtu ana imani zake fulani na mapambano, ana ruti yake anayoiendea ambayo yeye ndio anaweza kuielewa vizuri zaidi na anaona sisi wengine ni mashetani, mtu aina hiyo unampa amani, unamuacha”- Mhe Ndugai

“Bunge la 9 wakati wa kina Mzee Slaa palikuwa na wapinzani ambao walikuwa wakifanya kazi yao, walikuwa wanashusha hoja ambazo tukikaa pembeni kama CCM tunaambiana kuwa tunaharibiana” - Mhe Ndugai

 
Nasikia na kwao jimboni hawamtaki sasa asubiri kugombea kwenye jimbo la magogoni
Akimbana sana Jamaa ataishia tu kusema nilitoka familia Maskini saana,nilitembea Km 8 kwenda Shule na nilishinda njaa sana mimi.
 
Anajifedhehesha bure
Yani anafanya kumuattack tu mbowe kila swali analoulizwa, mara hakupigwa alianguka ni story nilizosikia yani anaongea naye hana uhakika. Mara alilewa chakali.
 
Back
Top Bottom