TANZIA Joel Misesemo afariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofani jengo la Derm eneo la Makumbusho, Dar

TANZIA Joel Misesemo afariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofani jengo la Derm eneo la Makumbusho, Dar

Niki zoom Taasisi moja iloyo Jirani hapo na hili Tukio nalazimika Kuamini kuwa huyo Mtu hakijirusha bali alirushwa kwa sababu za Kumnyamazisha au alikuwa na Uadui na Mteuwaji Mkuu hivyo Watu wa Mfumo wameamua Kumuondoa kwa Mbinu hiyo.
Halafu mitaa hiyo wamejaa wale jamaa balaa. Wakina Derua wenyewe ni wana tai.
 
Pale Mwanga Tower, Makumbusho limetokea tukio la mtu asiyefamika kujirusha kutoka gorofani, ambapo inasemekana tukio hilo limetokea mapema leo majira ya saa kumi na moja asubuhi.

Mpaka majira ya saa mbili asubuhi bado mwili wa mtu huyo ulikuwa eneo hilo. Taarifa zaidi zitakujia kadri zitakavyopatikana.

View attachment 2632805
Joel Misesemo enzi za uhai wake​

=====

Kijana asiyefahamika aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35 amefariki baada ya kujirusha kutoka gorofa ya 15 katika jengo la Derm lililopo Makumbusho, Dar es Salaam.


UPDATE: Polisi yathibitisha aliyejiua, kufanya uchunguzi


POLISI: KAMERA ZIMEONESHA JOEL MISESEMO AKIJIRUSHA MAKUSUDI KUTOKA GHOROFA YA 7
Kufuatia tukio la kifo cha Joel Misesemo mwenye umri kati ya miaka 35 hadi 40, Mkazi wa Mwananyamala, Jeshi la Polisi limesema chanzo cha awali ni mhusika kujirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kijitonyama.

Imeelezwa kuwa Joel alifika eneo hilo akiwa na gari aina ya Suzuki rangi ya silver (T142 DRM) na kuonekana katika jengo hilo Saa 11 Alfajiri ya Mei 23, 2023, akamwambia Mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye Msikiti uliopo ghorofa ya 15 ndani ya jengo hilo, muda mfupi baadaye alijirusha.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema kamera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya 7 kupitia dirishani na mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi Zaidi
Pole Kwa mke wake
 
Hauwajui hata hao wazungu unaosema, wanaweza acha crime scene hata masaa 10 kwa ajili ya ku studu mazingira na ku collect evidence /samples
Hiku marehemu akiwa kaachwa anadhalilika hapohapo pembeni

Si ndio?
Wenzetu wanakuja na ambulance wajaribu kuwahisha hospital huku polisi anaachwa anedelee na uchunguzi
kama wanaweza kukuokoa,ila sie tayari polisi wanahitimisha umekufa
 
Joel nilimfahamu kupitia rafiki yangu, tulikua tunaonana kanisani DPC kinondoni, familia ya kina Joel wote walikua wanasali hapo na baba yao alikua mchungaji kama sikosei anaitwa Pastor Chizii..

Joel alikua mtu fulani humble na mcheshi mnoo, walikua wanaishi mwananyamala, nakumbuka badae Joel akaoa, akaenda na kusoma degree ya social work chuo cha ustawi pale..
Sijui nini kimemkuta kwa kweli hadi kufikia hatua ya kujifanyia ukatili huo..
Hadi juzi alikuwepo DPC, alikuwepo ibadani jumapili.

Mzee wake hakuwa mchungaji bali mzee wa kanisa.
 
Hiku marehemu akiwa kaachwa anadhalilika hapohapo pembeni

Si ndio?
Wenzetu wanakuja na ambulance wajaribu kuwahisha hospital huku polisi anaachwa anedelee na uchunguzi
kama wanaweza kukuokoa,ila sie tayari polisi wanahitimisha umekufa

Check ID extra, Azam TV number 200, haswa haswa anafunikwa, ila atashinda hapo mda mrefu sana, labda useme utepe, ila mwili wa Marehemu kwa Wazungu utapata tabu sana kwa sababu ya uchunguzi.
 
Check ID extra, Azam TV number 200, haswa haswa anafunikwa, ila atashinda hapo mda mrefu sana, labda useme utepe, ila mwili wa Marehemu kwa Wazungu utapata tabu sana kwa sababu ya uchunguzi.
Ikiwa confirmed kafa mfano mwili umeokotwa umeharibika ndo wanaweza kufanya kumfunika.ila tukio la mda mfupi ulopita mfano hilo la kujirusha huwa wanamoiga picha kisha wanachora alivyolala kwa spray nyeupe wanaachia ambulance wamchukue wao wanaendelea na mengine.
Hata aliegongwa na gari wanachora anachukuliwa wao wanaendelea na kazi eneo la tukio
 
Back
Top Bottom