digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 8,926
- 17,880
Inasikitisha sana hawa wajuaji wetu wa jfKwani Kuna uwezekano wa kuwa nje ya hayo matatu mkuu!?..yaani unatabiri mechi itakua na mshindi au sare!!
Sasa ndio wajiue?.Nashauri Serikali iweke Somo la Stoicism Phillosophy kwenye mitaala yake ili kuwafundisha watu namna ya kuvumilia shida.Watu wengi wako depressed.
Maisha yamekua na changamoto nyingi.
🤣🤣🤣🤣🤣Nasikia siku hizi kwenye daladala watu wanakuna vichwa vya wenzao wakifikiri vyao kisa stress.
Hivi unawachukuliaje Wasukuma mzee?.Unaweza kudhani kajirusha kumbe ni msukuma alikua anashangaa shangaa akatokea dirishani bahati mbaya
Halafu mitaa hiyo wamejaa wale jamaa balaa. Wakina Derua wenyewe ni wana tai.Niki zoom Taasisi moja iloyo Jirani hapo na hili Tukio nalazimika Kuamini kuwa huyo Mtu hakijirusha bali alirushwa kwa sababu za Kumnyamazisha au alikuwa na Uadui na Mteuwaji Mkuu hivyo Watu wa Mfumo wameamua Kumuondoa kwa Mbinu hiyo.
Mtu ana drive ugumu wa maisha unatoka wapi?Ugumu wa maisha!Tanzania viongozi wanakula na kusaza.wananchi wamesahaulika
Wazungu wakisema hatuna akili tusikatae tangu saa 11 mpaka saa 2 mnauangalia tu? Hamna vituo vya polisi? hospital?
Majuha wa kutupwa.Sizani kama watu wa kitengo watakua majuha kiasi hiki, kati ya njia zote wamuondoe kwa style hii na sio nyingine ya kimya kimya
Pole Kwa mke wakePale Mwanga Tower, Makumbusho limetokea tukio la mtu asiyefamika kujirusha kutoka gorofani, ambapo inasemekana tukio hilo limetokea mapema leo majira ya saa kumi na moja asubuhi.
Mpaka majira ya saa mbili asubuhi bado mwili wa mtu huyo ulikuwa eneo hilo. Taarifa zaidi zitakujia kadri zitakavyopatikana.
View attachment 2632805
Joel Misesemo enzi za uhai wake
=====
Kijana asiyefahamika aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35 amefariki baada ya kujirusha kutoka gorofa ya 15 katika jengo la Derm lililopo Makumbusho, Dar es Salaam.
UPDATE: Polisi yathibitisha aliyejiua, kufanya uchunguzi
POLISI: KAMERA ZIMEONESHA JOEL MISESEMO AKIJIRUSHA MAKUSUDI KUTOKA GHOROFA YA 7
Kufuatia tukio la kifo cha Joel Misesemo mwenye umri kati ya miaka 35 hadi 40, Mkazi wa Mwananyamala, Jeshi la Polisi limesema chanzo cha awali ni mhusika kujirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kijitonyama.
Imeelezwa kuwa Joel alifika eneo hilo akiwa na gari aina ya Suzuki rangi ya silver (T142 DRM) na kuonekana katika jengo hilo Saa 11 Alfajiri ya Mei 23, 2023, akamwambia Mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye Msikiti uliopo ghorofa ya 15 ndani ya jengo hilo, muda mfupi baadaye alijirusha.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema kamera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya 7 kupitia dirishani na mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi Zaidi
4. stress za madeniHapo kuna mawili au matatu
1. Kajirusha
2. Karushwa
3. Kashurutishwa kujirusha
Wewe kila mtu ni classmate!!!!R.I.P classmate
Hiku marehemu akiwa kaachwa anadhalilika hapohapo pembeniHauwajui hata hao wazungu unaosema, wanaweza acha crime scene hata masaa 10 kwa ajili ya ku studu mazingira na ku collect evidence /samples
Fire ni kikosi cha uokozi, sio kuzima moto tu. Fire ina hadi ambulance.Sasa fire imeenda kufanya nini !!
Eti fire nayo imefika kwa wakati.
Anaweza kujitetea kuwa alitaka kujivunja miguu na sio kujiua.😄Inakua miguu imevunjika.
Ila kumbuka kutaka kujiua ni kosa la jinai.
Tunakunyanyapaa hadi ukome kujaribu kufaHivi ukijirusha ukapona halafu miguu ikavunjika inakuwaje hapo?
Hadi juzi alikuwepo DPC, alikuwepo ibadani jumapili.Joel nilimfahamu kupitia rafiki yangu, tulikua tunaonana kanisani DPC kinondoni, familia ya kina Joel wote walikua wanasali hapo na baba yao alikua mchungaji kama sikosei anaitwa Pastor Chizii..
Joel alikua mtu fulani humble na mcheshi mnoo, walikua wanaishi mwananyamala, nakumbuka badae Joel akaoa, akaenda na kusoma degree ya social work chuo cha ustawi pale..
Sijui nini kimemkuta kwa kweli hadi kufikia hatua ya kujifanyia ukatili huo..
Hiku marehemu akiwa kaachwa anadhalilika hapohapo pembeni
Si ndio?
Wenzetu wanakuja na ambulance wajaribu kuwahisha hospital huku polisi anaachwa anedelee na uchunguzi
kama wanaweza kukuokoa,ila sie tayari polisi wanahitimisha umekufa
Sasa kama ana mpaka Suzuki RAV4 huyo wa kijijini nae afanye nini? Tujifunze kuridhika kama ni kweli ugumu wa maisha ndio sababu yake..ila hao wengi huwa ni michakato yao ya utafutaji ndio huwafikisha hapo.Ugumu wa maisha!Tanzania viongozi wanakula na kusaza.wananchi wamesahaulika
Namba 3 ndiyo jibu, ... haya madeni yatatushurutisha wengi sana kufanya MAAMUZI YALIYOSHINDIKANA!Hapo kuna mawili au matatu
1. Kajirusha
2. Karushwa
3. Kashurutishwa kujirusha
Ikiwa confirmed kafa mfano mwili umeokotwa umeharibika ndo wanaweza kufanya kumfunika.ila tukio la mda mfupi ulopita mfano hilo la kujirusha huwa wanamoiga picha kisha wanachora alivyolala kwa spray nyeupe wanaachia ambulance wamchukue wao wanaendelea na mengine.Check ID extra, Azam TV number 200, haswa haswa anafunikwa, ila atashinda hapo mda mrefu sana, labda useme utepe, ila mwili wa Marehemu kwa Wazungu utapata tabu sana kwa sababu ya uchunguzi.