Akilinjema
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 11,430
- 11,813
Wanasema alienda hapo akadai anataka akswali huko juu(alidanganya)
Msikiti upo ghorofa la juu kabisa 15,ye akapanda lift akaishia floor ya 7 wakamuona anaongea na simu mda mrefu ndo wakasikia kishindo mtu kaanguka.so alikua na nani huko kisa nini hawajui.
Jitahidi kutumia akili zaidi na kuzuia mihemko ya hisia zako.Karushwa na pengo
Joel hakuwa na madeni bali alipitia changamoto za kiafya.
Mkuu mbona mi naona kwenye ile video jamaa alivyodondokea tu kwenye tank moja kwa moja wakakimbilia kumtoa sidhan km waliona hatoki. Ile video mwili unasisimkaHakufa palepale alikimbizwa hospital. Huenda alifia njiani au hospital
Mbaya zaidi tukio lilikuwa linarushwa live na ITV wakakatisha matangazo. Yule njomba kut0ka Ntwara ilikuwa kazi yake michezo ya kupanda majengo marefu na kujirusha ndani ya tank za maji huku akiongozwa(guided) na kamba asidondokee nje ya tank.
Pale alifeli kukokotoa urefu wa jengo, uzito wake, na kina cha maji ili kutambua atakuwa submerged urefu gani ndani ya maji ili asiguze sakafu ya tank kwa mshindo mkubwa. Aliidharau Gravitional force (g). Alipotumbukia wanashangaa hatoki nje mwenyewe wakawahi kumtoa kavunjika viungo.
Angejiua vp sasa?Najua ni sababu ya haya maisha kujiua kwa kujirusha aseeh daah labda alirushwa bwana....
MkuuUnachozungumza ni kweli depression za namna hii zinanikumba saana na mpaka sasa mara nyingi wazo la bora nige lina nijia ila nikikumbuka watoto wangu ni wadogo na pia kujiua ni udhaifu na kumkosea Mungu nabaki kusema heri nisubiri wakati wangu nipumzike ila si kwakujiua mwenyewe
Mno. Tunajikaza tu lkn yaliyomo ndani ya mioyo yetu mazito wakati mwengine hayahimiliki...tunajikaza tuWatu wengi wako depressed.
Maisha yamekua na changamoto nyingi.
Sahih mkuu...anaefanya dhihaka hayajamkuta.Hakuna haja ya kufanya dhihaka haya mambo yana siri kubwa kuna issue ya depression huwezi kujuwa kuna wakati mtu haongei na mtu kuna kampeni kubwa duniani kuhusu haya mambo nakumbuka ile story ya Gary Speed mchezaji/Manager alikuwa na mafanikio makubwa tu lakini ghafla akakutwa kajinyonga garage na uchunguzi ulifanyika hakuna foul yoyote kumbe depression. Na hata hapa kwetu yapo sana sasa bila kuhitimisha nini kilimsibu ni vizuri tukasikia uchunguzi sababu issue kama hizi tumeona sana.
Mno. Tunajikaza tu lkn yaliyomo ndani ya mioyo yetu mazito wakati mwengine hayahimiliki...tunajikaza tu
Ulitaka mlinzi aanze kuhoji dini yake ?Halafu Mkristo lakini eti alimwambia mlinzi kuwa anaenda kuswali msikitini juu. [emoji848]
Hizi gorofa nyingi ukiingia unalizwa unaenda wapi ?
Jamaa kataja tu ili mradi si unajua tena mtu akiwa na lake.
Sina haja ya kumlaumu haya maisha acheni tu basi ..
Hahahaha jamaa lishiba ugaliHuyu Jamaa ndio Tushamsahau!!View attachment 2632363
Namshangaa huyo mbwa mbona amewahi kwenye tukio [emoji1] [emoji1787]Huyu Jamaa ndio Tushamsahau!!View attachment 2632363
Mmmh aseeJoel hakuwa na madeni bali alipitia changamoto za kiafya.
HayajakukutaNi upumbavu tu kujiuwa
Hukuwa na majini wala mashetani, hizo zilikuwa ni nyege tu za baleheDepression nyingine huletwa na mashetani ambao huuvamia mwili wa mwanadamu na kuanza kumshawishi afanye mambo ya ajabu .Kwa ambaye hajapitia haya hawezi kuamini ila mi nishapitia hali hiyo!
Nilikuwa heavily depressed, muda mwingi najifungia ndani, sihitaji kuonana na mtu yeyote na vilevile hayo mawazo ya kujiua yalikuwa yakinijia sana, yaani unasikia kabisa vitu masikioni vikikushawishi ufanye uovu huo!!
Nikaja kuchukuliwa nyumbani kinguvu na wazazi wangu kwenda kutibiwa kwa sheikh kwa kisomo cha Ruqyah!!
Nilipofika tu kwake nikawa situlii, yaan kana mtu mwenye wasiwasi mzito, tumbo linajaa gas, napiga sana miayo n.k. Sheikh akaniangalia akasema ni signs za kuwa nina jini (shetani) baya limeuvaa mwili wangu.
Akanitibu kwa kunisomea Quran...ghafla nikaanza kupoteza uwezo wa kuona nikaanguka chini, akanisomea baadae nikarejea katika hali yangu ya kawaida baada ya lile shetani kunitoka. Na tokea hapo ile hali ya wasiwasi iliyopitiliza na depression ikanitoka.
So usimshangae jamaa huenda kichwani kwake alishavamiwa na mashetani na yalikuwa yakimpelekesha kumshawishi ajitupe ili aende akapumzike kuzimu huko.
Kama mmesoma biblia kuna story ya yesu anaposhawishiwa na shetani kwenda kujiua
MATHAYO 4
Kujaribiwa kwa Yesu
(Marko 1:12-13; Luka 4:1-13)
1Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.
2Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.
3Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
4Yesu akamjibu, “Imeandikwa:
‘Mtu haishi kwa mkate tu,
ila kwa kila neno asemalo Mungu.’”
5Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu, 6 akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa:
‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako;
watakuchukua mikononi mwao,
usije ukajikwaa kwenye jiwe.’”
7Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia:
‘Usimjaribu Bwana, Mungu wako.’”
8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
9akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.”
10Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa:
‘Utamwabudu Bwana Mungu wako
na kumtumikia yeye peke yake.’”
11Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia."
Nb
hivyo Joel wakati anapanda juu ya ghorofa alikuwa chini ya ushawishi wa ibilisi (shetani). Ulikuwa ni mtihani kwake aweze kuushinda kwa kuyakataa mawazo maovu ya ibilisi but unfortunately alishindwa na kuamua kujitupa chini.
Njia pekee ya kuweza kuyashinda majaribu haya ni kuwa karibu na Mungu tu.
Nahisi alishangaa mtu anajitumbukizaje ndani ya tank la maji 🐶Namshangaa huyo mbwa mbona amewahi kwenye tukio [emoji1] [emoji1787]
وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَمَنْ قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِفْ فِي الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنْصُورًاHayajakukuta
Yakikufika hapa, taaluma inakaa pembeni uhalisia unachukua nafasi.Mimi nimesoma na marehemu joel pale taasisi ya ustawi wa jamii, kwa tuliomfahamu joel alikuwa ni mtu mwenye furaha muda wote kiasi kwamba hata baadhi yetu walikuwa wanamfata kuomba ushauri kuhusu mambo ya chuo na maisha nje ya shule. Na kwa taaluma ya psychology aliyoipata pale kwenye taasisi ni jambo la kushangaza sana kwanini alichukua maamuzi magumu na kuamua kupinzana na ujuzi wake taaluma ya ustawi
Hayajamfika huyo dada nakuambia.Kuna mdada alishawahi niambia Kujiua ni "Lack of Life Skills"...