Depression nyingine huletwa na mashetani ambao huuvamia mwili wa mwanadamu na kuanza kumshawishi afanye mambo ya ajabu .Kwa ambaye hajapitia haya hawezi kuamini ila mi nishapitia hali hiyo!
Nilikuwa heavily depressed, muda mwingi najifungia ndani, sihitaji kuonana na mtu yeyote na vilevile hayo mawazo ya kujiua yalikuwa yakinijia sana, yaani unasikia kabisa vitu masikioni vikikushawishi ufanye uovu huo!!
Nikaja kuchukuliwa nyumbani kinguvu na wazazi wangu kwenda kutibiwa kwa sheikh kwa kisomo cha Ruqyah!!
Nilipofika tu kwake nikawa situlii, yaan kana mtu mwenye wasiwasi mzito, tumbo linajaa gas, napiga sana miayo n.k. Sheikh akaniangalia akasema ni signs za kuwa nina jini (shetani) baya limeuvaa mwili wangu.
Akanitibu kwa kunisomea Quran...ghafla nikaanza kupoteza uwezo wa kuona nikaanguka chini, akanisomea baadae nikarejea katika hali yangu ya kawaida baada ya lile shetani kunitoka. Na tokea hapo ile hali ya wasiwasi iliyopitiliza na depression ikanitoka.
So usimshangae jamaa huenda kichwani kwake alishavamiwa na mashetani na yalikuwa yakimpelekesha kumshawishi ajitupe ili aende akapumzike kuzimu huko.
Kama mmesoma biblia kuna story ya yesu anaposhawishiwa na shetani kwenda kujiua
MATHAYO 4
Kujaribiwa kwa Yesu
(Marko 1:12-13; Luka 4:1-13)
1Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.
2Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.
3Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
4Yesu akamjibu, “Imeandikwa:
‘Mtu haishi kwa mkate tu,
ila kwa kila neno asemalo Mungu.’”
5Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu, 6 akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa:
‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako;
watakuchukua mikononi mwao,
usije ukajikwaa kwenye jiwe.’”
7Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia:
‘Usimjaribu Bwana, Mungu wako.’”
8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,
9akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.”
10Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa:
‘Utamwabudu Bwana Mungu wako
na kumtumikia yeye peke yake.’”
11Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia."
Nb
hivyo Joel wakati anapanda juu ya ghorofa alikuwa chini ya ushawishi wa ibilisi (shetani). Ulikuwa ni mtihani kwake aweze kuushinda kwa kuyakataa mawazo maovu ya ibilisi but unfortunately alishindwa na kuamua kujitupa chini.
Njia pekee ya kuweza kuyashinda majaribu haya ni kuwa karibu na Mungu tu.