TANZIA Joel Misesemo afariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofani jengo la Derm eneo la Makumbusho, Dar

TANZIA Joel Misesemo afariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofani jengo la Derm eneo la Makumbusho, Dar

Wanasema alienda hapo akadai anataka akswali huko juu(alidanganya)
Msikiti upo ghorofa la juu kabisa 15,ye akapanda lift akaishia floor ya 7 wakamuona anaongea na simu mda mrefu ndo wakasikia kishindo mtu kaanguka.so alikua na nani huko kisa nini hawajui.



TCRA waangalie alokuwa akiongea nao mwishoni kwa muda mrefu na walikuwa wanaongea nini?
 
Hakufa palepale alikimbizwa hospital. Huenda alifia njiani au hospital
Mbaya zaidi tukio lilikuwa linarushwa live na ITV wakakatisha matangazo. Yule njomba kut0ka Ntwara ilikuwa kazi yake michezo ya kupanda majengo marefu na kujirusha ndani ya tank za maji huku akiongozwa(guided) na kamba asidondokee nje ya tank.
Pale alifeli kukokotoa urefu wa jengo, uzito wake, na kina cha maji ili kutambua atakuwa submerged urefu gani ndani ya maji ili asiguze sakafu ya tank kwa mshindo mkubwa. Aliidharau Gravitional force (g). Alipotumbukia wanashangaa hatoki nje mwenyewe wakawahi kumtoa kavunjika viungo.
Mkuu mbona mi naona kwenye ile video jamaa alivyodondokea tu kwenye tank moja kwa moja wakakimbilia kumtoa sidhan km waliona hatoki. Ile video mwili unasisimka
 
Hakuna haja ya kufanya dhihaka haya mambo yana siri kubwa kuna issue ya depression huwezi kujuwa kuna wakati mtu haongei na mtu kuna kampeni kubwa duniani kuhusu haya mambo nakumbuka ile story ya Gary Speed mchezaji/Manager alikuwa na mafanikio makubwa tu lakini ghafla akakutwa kajinyonga garage na uchunguzi ulifanyika hakuna foul yoyote kumbe depression. Na hata hapa kwetu yapo sana sasa bila kuhitimisha nini kilimsibu ni vizuri tukasikia uchunguzi sababu issue kama hizi tumeona sana.
Sahih mkuu...anaefanya dhihaka hayajamkuta.
Muhimu kusema Mungu Atunusuru
 
Mno. Tunajikaza tu lkn yaliyomo ndani ya mioyo yetu mazito wakati mwengine hayahimiliki...tunajikaza tu
FB_IMG_1684917349724.jpg
 
Depression nyingine huletwa na mashetani ambao huuvamia mwili wa mwanadamu na kuanza kumshawishi afanye mambo ya ajabu .Kwa ambaye hajapitia haya hawezi kuamini ila mi nishapitia hali hiyo!

Nilikuwa heavily depressed, muda mwingi najifungia ndani, sihitaji kuonana na mtu yeyote na vilevile hayo mawazo ya kujiua yalikuwa yakinijia sana, yaani unasikia kabisa vitu masikioni vikikushawishi ufanye uovu huo!!

Nikaja kuchukuliwa nyumbani kinguvu na wazazi wangu kwenda kutibiwa kwa sheikh kwa kisomo cha Ruqyah!!

Nilipofika tu kwake nikawa situlii, yaan kana mtu mwenye wasiwasi mzito, tumbo linajaa gas, napiga sana miayo n.k. Sheikh akaniangalia akasema ni signs za kuwa nina jini (shetani) baya limeuvaa mwili wangu.

Akanitibu kwa kunisomea Quran...ghafla nikaanza kupoteza uwezo wa kuona nikaanguka chini, akanisomea baadae nikarejea katika hali yangu ya kawaida baada ya lile shetani kunitoka. Na tokea hapo ile hali ya wasiwasi iliyopitiliza na depression ikanitoka.

So usimshangae jamaa huenda kichwani kwake alishavamiwa na mashetani na yalikuwa yakimpelekesha kumshawishi ajitupe ili aende akapumzike kuzimu huko.

Kama mmesoma biblia kuna story ya yesu anaposhawishiwa na shetani kwenda kujiua




MATHAYO 4​

Kujaribiwa kwa Yesu
(Marko 1:12-13; Luka 4:1-13)

1Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.
2Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.

3Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”

4Yesu akamjibu, “Imeandikwa:
‘Mtu haishi kwa mkate tu,
ila kwa kila neno asemalo Mungu.’”

5Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu, 6 akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa:
‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako;
watakuchukua mikononi mwao,
usije ukajikwaa kwenye jiwe.’”

7Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia:
‘Usimjaribu Bwana, Mungu wako.’”

8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,

9akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.”

10Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa:
‘Utamwabudu Bwana Mungu wako
na kumtumikia yeye peke yake.’”

11Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia."

Nb
hivyo Joel wakati anapanda juu ya ghorofa alikuwa chini ya ushawishi wa ibilisi (shetani). Ulikuwa ni mtihani kwake aweze kuushinda kwa kuyakataa mawazo maovu ya ibilisi but unfortunately alishindwa na kuamua kujitupa chini.

Njia pekee ya kuweza kuyashinda majaribu haya ni kuwa karibu na Mungu tu.
Hukuwa na majini wala mashetani, hizo zilikuwa ni nyege tu za balehe
 
Hayajakukuta
وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَمَنْ قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِفْ فِي الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنْصُورًا
Israa 33
Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.
 
Mimi nimesoma na marehemu joel pale taasisi ya ustawi wa jamii, kwa tuliomfahamu joel alikuwa ni mtu mwenye furaha muda wote kiasi kwamba hata baadhi yetu walikuwa wanamfata kuomba ushauri kuhusu mambo ya chuo na maisha nje ya shule. Na kwa taaluma ya psychology aliyoipata pale kwenye taasisi ni jambo la kushangaza sana kwanini alichukua maamuzi magumu na kuamua kupinzana na ujuzi wake taaluma ya ustawi
Yakikufika hapa, taaluma inakaa pembeni uhalisia unachukua nafasi.
 
Back
Top Bottom