TANZIA Joel Misesemo afariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofani jengo la Derm eneo la Makumbusho, Dar

TANZIA Joel Misesemo afariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofani jengo la Derm eneo la Makumbusho, Dar

Dah [emoji22] ninaamini pasi na shaka yoyote kuwa huu ni wakati sahihi kabisa wa kuzungungumza wanaume wenyewe kwa wenyewe kuwa ni sawa kutokuwa sawa, its really ok not to be ok! Tukae chini wenyewe kwa wenyewe men to men TUONGEE YETU YOTE dah [emoji17] RIP brother Joel [emoji120]

Posted @withregram • @millardayo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema linachunguza tukio la kifo cha Mtu aitwae Joel Misesemo Chizi anayekadiriwa kuwa miaka kati ya 35 hadi 40, Mkazi wa Mwananyamala ambaye alijirusha kutoka ghorofani kwenye jengo la Derm Plaza lililopo Makumbusho Kijitonyama na kufariki.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Marehemu alionekana katika jengo hilo leo tarehe 23, Mei 2023 majira ya saa kumi na moja alifajiri na alimwambia Mlinzi wa zamu kuwa anaenda kufanya ibada kwenye Msikiti uliopo ghorofa ya 15 dani ya jengo hilo lakini muda mfupi baadaye alijirusha.

Taarifa ya Polisi imesema camera za jengo hilo zimemuonesha akijirusha kwa makusudi kutoka ghorofa ya saba kupitia dirishani na kufariki ambapo tayari mwili wake umepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.

Jeshi la Polisi limepata gari la Marehemu aina ya Suzuki rangi ya silver lenye namba za usajili T142 DRM lililokuwa limeegeshwa kwenye maegesho ya magari katika eneo hilo na sasa limehifadhiwa Kituo cha Polisi Oysterbay.
Sasa gari lake linahusiano gani na kifo chake police wetu nao wanacomplicate mambo sana.
 
DUSTBINCANE12L_02_600x.jpg
 
Tanzania sidhani kama inaweka msisitizo juu ya ufahamu kuhusu magonjwa ya akili ambayo yanaongozwa na ugonjwa wa msongo wa mawazo (aka depression).

Watu wengi sana wanasumbuka na hili tatizo kwa kujua ama kutokujua.
 
Mwl?

Ingia bank acha uoga wa pesa mkuu utakufa masikini,

Ingia bank omba mkopo fanya biashara ya faida

Tafuta hata laki nne tu, nenda kijijini kwenu kanunue ng'ombe mmoja tu au wawili wa laki mbili mbili, uwalishe pumba muda wa miezi miwili tu kwa uaminifu kabisa, ninauhakika mara baada ya miezi miwili hiyo, kila ng'ombe mmoja atakupa faida ya ng'ombe mwingine mmoja!
watu wengine mnawazaga ng'ombe tu. wasukuma bwana.
 
Yaani pole Joel kwa uliyopitia mpaka kujitoa uhai kwa njia ngumu kiasi hicho. Jina lake la mwisho ni Chizi. Yaani kuna majina ukikuta ulipewa udogoni na hayafai ni Bora kuyafuta rasmi kwa deep poll ili kuepuka mikosi kabisa. Majina na maneno huwa yanaumba Sana.
 
Back
Top Bottom