John Heche akamatwa akiwa Mahakama Kuu akijiandaa kuhudhuria kesi ya Tundu Lissu

John Heche akamatwa akiwa Mahakama Kuu akijiandaa kuhudhuria kesi ya Tundu Lissu

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Makamu Mwenyekiti Bara wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Heche mapema leo asubuhi amekamatwa na jeshi la Polisi Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam, alipofika kwa ajili ya kufuatilia shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu.

Pia soma

> John Heche amekamatwa na kuzuiliwa mpaka wa Sirari akiwa anaelekea Kenya kwenye mazishi ya Odinga
> Uhamiaji wadai Heche amevuka mpaka wa Sirari kinyume na sheria

Hechee.png




Video: Heche akiingizwa kwenye gari la Polisi


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika akizungumzia tukio la kukamatwa kwa makamu Mwenyekiti Bara wa chama hicho John Heche, leo Asubuhi Mahakamani alipofika kwa ajili ha kusikiliza shauri la uhaini linalomkabili Tundu Lissu.

UPDATE

Wakili wa CHADEMA, Gaston Shundo ameeeleza kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche ambaye amekamatwa leo Oktoba 22 akiwa katika viunga vya mahakama kuu kanda ya Dar es salaam akisubiri kusikiliza kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesafirisha leo kuelekea wilaya ya Tarime mkoa wa Mara

Soma Wakili Gaston Shundo: Polisi wamesema Heche hayupo DAR amesafirishwa kupelekwa Tarime
 
Makamu Mwenyekiti wa familia Mh John Heche amekamatwa kwenye lango la mahakama alipoenda kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu

Inasemekana amepelekwa kituo cha police cha kati
Police hawajaeleza sababu za kukamatwa kwake

Naona Serikali inatumika hila ili kuwaweka Kizuizini viongozi wakuu wa Chadema ili kupita uchaguzi wa utapeli wa kiini macho
1761115512230.jpg
 
Back
Top Bottom