John Heche amwambia Ndugai kesho anaingia bungeni na hakuna wa kumzuia

John Heche amwambia Ndugai kesho anaingia bungeni na hakuna wa kumzuia

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011


Baadhi ya Wabunge wa Chama Kikuu cha Upinzani (CHADEMA) wamepinga vikali maamuzi ya Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai ya kuwataka Wabunge hao kutorejea bungeni hadi pale watakapopimwa na kuthibitika kuwa hawana Corona.

Aidha, inaelezwa kuwa Wabunge hao wa Chadema wamejiweka Karantini ya hiyari kwa wiki mbili baada ya Wabunge wengine watatu kufariki dunia katika siku za hivi karibuni.

Aidha, Mh. John Heche amepinga amri hiyo ya Spika wa Bunge ya kuwazuia kwenda Bungeni kwa sababu anadai kuwa hakuna kanuni yoyote waliyoivunja.

Heche, anafafanua kuwa hata Spika alipohojiwa na vyombo vya Habari alikiri kuwa Wabunge wa Chadema hawajavunja kanuni yoyote.

katika kudadavua suala hili Mh. John Heche amaesema "Tupo tayari kupima na sisi ndio wa mwanzo tuliotaka kupima lakini hatutaki kupimwa kibaguzi, tunataka kama Spika anataka Wabunge wote wapimwe hata wa CCM."

Zaidi ya hayo, Heche ameeleza kuwa sio Wabunge wa Chadema pekee ambao wamejitenga hata Wabunge wengine wa CCM wapo makwao na wakitaka kurejea Bungeni wanarejea bila bughudha yoyote.

ZAIDI SOMA
- Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2

- Wabunge wa CHADEMA kurejea Bungeni kuanzia leo
 
Wakubwa wa dunia wanapumulia mipira.
Kenya Hali tete
Zambia Hali tete
Kiboko TANZANIA [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]..
Calculator imetolewa alama ya +.
Screenshot_20200514-233852.jpg
Screenshot_20200514-233953.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom