John Heche anastahili kuvaa viatu vya Freeman Mbowe

Nimefuatilia michango yake tokea akiwa diwani huko Tarime mpaka kuwa Mbunge 2015, unaweza kubaliana na Mimi kuwa huyu ni msomi anayejitambua, anajua kujenga hoja, mzalendo haswaa, mtiifu, na misimamo isiyoyumba

Alipokuwa mwenyekiti BAVICHA ndipo tulishuhudia taasisi imara ya vijana iliyozaa wanasiasa wengi makini. Na tokea amalize muda wake Bavicha haikuwahi para mwenyekiti makini level ya Heche.

Ukifuatilia ziara yake Kanda ya kusini unaweza ona ushawishi na spirit aliyonayo kupigania maslahi ya wananchi maskini.

Kama mnavyofahamu Mhe Mbowe alitangaza atastaafu 2023, hivyo basi Mimi kama mwanachama hai wa Chadema naona Heche Sasa anafaa kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Ninaamini ataweza kufanikisha vision ya Mbowe na jamii nzima ya Chadema kufikia malengo yake.

Hata mimi namkubali
 
Kama ana huo uwezo wa kiuongozi atengeneze mazingira ya kumtoa Mbowe kidemokrasia na ayafanikishe. Mbowe ni over stayed mkt na hana mchango mpya wa kiuongozi uliobaki kwa cdm akiwa kama mkt. Abakie kuwa mshauri tu apishe damu mpya.
Mbowe Alishasema tokea 2020 kuwa atastaafu uchaguzi mkuu wa chama utakaofuata. So kufikia mwakani or 2024 kwenye mkutano mkuu atastaafu na kwenda kwenye bodi ya wadhamini/Baraza la wazee.
 
Bila Katiba Mpya, na hasa ile Rasimu ya Warioba, kubadili sura za watu ni kazi bure.

Lazima kwanza yatengenezwe mazingira yatakayowezesha huyo Heche kama akiwa kiongozi afanye majukumu yake kwa nafasi ili aweze kufikia malengo yake.

Lakini kinyume na hapo, akiingia madarakani akakutana na mazingira haya yaliyopo, kama zuio la mikutano ya siasa, hakuna cha maana atakacho achieve zaidi ya kuishia kulumbana na polisi kila siku, hivyo kuzuia uwezo wake wa kiutendaji kuonekana.

Mafanikio pekee chini ya uongozi mpya ambayo watayapata, ni kuongeza idadi ya viti vya ubunge majimboni, lakini lile lengo kuu la upinzani kushika dola, hilo halitakaa lifikiwe kwa Katiba hii iliyopo, licha ya uwepo wa uongozi wowote mpya Chadema.
 
Kama mnavyofahamu Mhe Mbowe alitangaza atastaafu 2023, hivyo basi Mimi kama mwanachama hai wa Chadema naona Heche Sasa anafaa kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Ninaamini ataweza kufanikisha vision ya Mbowe na jamii nzima ya Chadema kufikia malengo yake.
Ninakubaliana na maudhui ya mada nzima, isipokuwa katika haya maneno machache hapa:"Ninaamini ataweza kufanikisha vision ya Mbowe..."

Kama kiongozi, ninaamini ataweza kusimamia yote yanayoaminiwa na chama kwa ujumla, lakini pia kama kiongozi atabuni na kupigania yote anayoona yanafaa kwa taifa zima la Tanzania bila ya kufungwa na aliyoyaona Mbowe kama kiongozi.
 
Kina nani wapo kwenye kakikundi sikutajii, mteule wao ni lema.

Ana uwezo au hana hiyo ni juu ya uwezo wangu kutambua.
Lema kuwa Mwenyekiti? Are you joking? Najua hoja Yako ni ukabila eti wachagga wanataka mchagga mwenzao? Kwamba Chadema ni Cha wachagga?

Hivi ingekua kweli Lissu angepewa fomu ya Urais? Au Mnyika angekua Katibu mkuu Leo hii?

Kwa taarifa Yako tu Chadema Ina nguvu kule Mara kuliko hata huko Kilimanjaro!! Hizo propaganda za ukabila zishakufa tokea 2015 maana Dar, Mbeya, Songwe, Moro, Mara zilikua zimejaa Chadema ilihali sio kwa wachagga!!
 
Mbowe Alishasema tokea 2020 kuwa atastaafu uchaguzi mkuu wa chama utakaofuata. So kufikia mwakani or 2024 kwenye mkutano mkuu atastaafu na kwenda kwenye bodi ya wadhamini/Baraza la wazee.

Kwa aina ya viongozi wanaorudishwa kwenye chaguzi zinazoendelea ndani ya CCM. 2024 cdm watakuwa wamechelewa sana. Mbowe apishe damu mpya hata kesho.
 
Mbowe Bado ana nguvu,

Na umri unavyozidi sogea BUSARA inazidi kuongezeka.

Mbowe ahakikishe CDM inashika DOLA akiwa mkt ndo ang'atuke.

Kwa sasa VIATU vya Mh Mbowe havivaliki.

Ameeeen.
 
Nimefuatilia michango yake tokea akiwa diwani huko Tarime mpaka kuwa Mbunge 2015, unaweza kubaliana na Mimi kuwa huyu ni msomi anayejitambua, anajua kujenga hoja, mzalendo haswaa, mtiifu, na misimamo isiyoyumba

Alipokuwa mwenyekiti BAVICHA ndipo tulishuhudia taasisi imara ya vijana iliyozaa wanasiasa wengi makini. Na tokea amalize muda wake Bavicha haikuwahi para mwenyekiti makini level ya Heche.

Ukifuatilia ziara yake Kanda ya kusini unaweza ona ushawishi na spirit aliyonayo kupigania maslahi ya wananchi maskini.

Kama mnavyofahamu Mhe Mbowe alitangaza atastaafu 2023, hivyo basi Mimi kama mwanachama hai wa Chadema naona Heche Sasa anafaa kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Ninaamini ataweza kufanikisha vision ya Mbowe na jamii nzima ya Chadema kufikia malengo yake.

MBOWE YUPO CHADEMA MILELE
 
Kwa taarifa Yako tu Chadema Ina nguvu kule Mara kuliko hata huko Kilimanjaro!! Hizo propaganda za ukabila zishakufa tokea 2015 maana Dar, Mbeya, Songwe, Moro, Mara zilikua zimejaa Chadema ilihali sio kwa wachagga!!
Hata wakati chacha wangwe anapigwa mizengwe chadema ilikuwa na nguvu Mara.

Au unaamini wangwe hakuwa na sifa za kuongoza chadema?!
 
Ninakubaliana na maudhui ya mada nzima, isipokuwa katika haya maneno machache hapa:"Ninaamini ataweza kufanikisha vision ya Mbowe..."

Kama kiongozi, ninaamini ataweza kusimamia yote yanayoaminiwa na chama kwa ujumla, lakini pia kama kiongozi atabuni na kupigania yote anayoona yanafaa kwa taifa zima la Tanzania bila ya kufungwa na aliyoyaona Mbowe kama kiongozi.
Kuna watu wanaamini Mbowe hawezi kutoka maana hajafikia vision yake ya kuifikisha Chadema ikulu so to solve that gap ndio na suggest kwamba ataifanikisha vision ya "Mbowe na familia nzima ya Chadema

Sijui kwanini umeikata hiyo sentensi ku fit ajenda Yako!!!
 
Hata wakati chacha wangwe anapigwa mizengwe chadema ilikuwa na nguvu Mara.

Au unaamini wangwe hakuwa na sifa za kuongoza chadema?!
Angekua mwenyekiti ila ilikua mapema sana, angemount challenge Ile 2014 angepata Uenyekiti same as Zitto. Maana Mbowe kaingia 2004 yaani miaka mitatu baadae tayari watu wanataka kumng'oa sidhani kama ilikua wise decision.
 
Kuna watu wanaamini Mbowe hawezi kutoka maana hajafikia vision yake ya kuifikisha Chadema ikulu so to solve that gap ndio na suggest kwamba ataifanikisha vision ya "Mbowe na familia nzima ya Chadema

Sijui kwanini umeikata hiyo sentensi ku fit ajenda Yako!!!
Actually, nilipata shida kidogo kuikata hiyo sentensi, nikijua nitakuwa nimetimiza lengo la niliyolenga kuyafikisha.

Nitakubaliana nawe, kama hiyo 'vision' ya Mbowe ni hilo la kuifikisha CHADEMA katika hatua hiyo.
Bila shaka kiongozi yeyote atakayechukua wadhifa baada ya Mbowe, lengo kuu litakuwa ni hilo hilo.
 
Angekua mwenyekiti ila ilikua mapema sana, angemount challenge Ile 2014 angepata Uenyekiti same as Zitto. Maana Mbowe kaingia 2004 yaani miaka mitatu baadae tayari watu wanataka kumng'oa sidhani kama ilikua wise decision.
Kulikuwa na ubaya gani kuwaachia wanachama wachague wanayeona anafaa kuwaongoza, si katiba inatamka uongozi ni miaka mitano baada ya hapo mnachaguana tena?

Zitto alizuiliwa kugombea 2010. Si jambo la afya kwa chama kinachojitambulisha kuwa cha kidemokrasia.
 
Heche anafaa kuwa kiongozi,ukimsikiliza akiongea unaonajinsi alivyo tulia na ana fact za kutosha.

Nimkosoaji mzuri,akiongea bidii ya kuelezea solution ya mambo anayo kosoa then he is 100% chairman material.
 
Back
Top Bottom