Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Pale hakuna kitu kabisa!. Ili Chadema kisonge mbele, huwezi kuleta an empty shell at the top!, angalau ungesema Lissu!. Udhaifu mkubwa wa Lema is his intelect, hana reasoning power at all!, huyu ni mediocre ambaye anaweza kuwaingiza watu barabani ndani ya dakika sifuri!. Kitu ambacho nakikubali kwa Lema ni ndoto zake na baadhi ya kauli zake!, ile kauli yake kwa Sabaya, mpaka kesho ni very fresh in my mind!, huyu uenyekiti hawezi kabisa, he meeds to be more mature!.Kina nani wapo kwenye kakikundi sikutajii, mteule wao ni lema.
Ana uwezo au hana hiyo ni juu ya uwezo wangu kutambua.
Chadema ina tatizo kubwa sana la kukosa succession plan!. Hili nililizungumza ile siku nimeongea na Dr. Slaa Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa?
Nilisema
Japo ushauri huu ni wa miaka 10 iliyopita, ingekuwa Chadema wameufuata ushauri huu, saa hizi, zamani Chadema iko Magogoni!.Wanabodi,
Mara baada ya mazishi ya Mhe. Regia, (RIP), on route back to Dar, nilibahatika kukutana mahali na Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wibroad Slaa akiwa na wife wake, Fina, tuliendesha maongezi mafupi informally na sio mazungumzo rasmi
Hiyo siku nilipokaa na Dr. Slaa, nilimweleza reservations zangu kuhusu sio tuu mgombea urais wa Chadema, bali nilieleza kuhusu udhaifu mkubwa wa Chadema katika kuwapata viongozi wake na wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi wa ndani ya chama, na nje ya chama, kama serikali za mtaa, ubunge na udiwani.
Nilimshauri Dr, Chadema ianze kuwa na succession plan ya kuwatayarisha viongozi wake from the grass roots levels, kwenye kila posti kuanzia nafasi za uongozi ndani ya chama, hadi nafasi za kugombea serikali za mitaa, udiwani, ubunge hadi urais, badala ya kuwategemea wanaotemwa CCM na kuwadaka tuu. Yes japo wanaotemwa tayari ni mtaji, lakini lazima Chadema kiwe na timu yake, ili kufika mahali hao wanaotemwa CCM kupimwa streghts zao kwa kulinganisha na waliopo, kama aliyepo ni stronger kuliko aliyetemwa, huyo anayetemwa CCM, hapati nafasi kuwa mgombea wa Chadema.
Na ili kujenga Chadema imara, Chadema pia lazima kiwe na internal mechanism yake ya kutafuta wanachama wapya waaminifu na kufanya internal vetting kwa viongozi wake, vinginevyo inaweza kujikuta ina kundi kubwa la viongozi, kumbe wengi ni mamluki tuu na mapandikizi ya waliotemwa CCM na kuhama kwa hasira za ketemwa tuu CCM, lakini mapenzi yao yako bado yako CCM, hivyo wanakuja Chadema ili kupata tuu fursa za kugombea, na wakikosa, mtawashuhudia wengi wakirejea CCM!.
Pia ili kupata a dedicated team ya viongozi imara, Chadema ianzishe mfumo scouting from grass roots levels na kuanzisha succession plan, kuwatayarisha viongozi wake wa kesho by headhunting recruitment of committed leaders, iwafanyie grooming, iwapike, waive, ndipo ije iwape uongozi, mfano sasa hapo ilipo, tayari Freeman Mbowe ameisha overstay as Chairman, Chadema ianze maandalizi ya kutafuta atajayerithi mikoba ya Mbowe kwa kuwapika viongozi wake kwa nafasi ya uenyekiti hadi waive kwa kumuandaa nani atapokea Mbowe uenyekiti, ili kujenga succession plan bila makundi ili kujenga sustainability ya chama chochote sustainable kina succession plan.
Kwenye Chadema haijajipanga niliwaambia kuwa kuna baadhi ya maeneo, watu wameichoka CCM mpaka basi kiasi kwamba hata kama Chadema ingesimamisha jiwe, hilo jiwe lingepita!. Hii inamaanisha kama Chadema ingesimamisha wagombea kila jimbo, saa hizi mngekuwa na wabunge wengi zaidi ya hawa waliopo!.
Miongoni mwa ushauri wangu kwa Dr. Slaa, Chadema isishobokee wagombea maarufu wala kusubiria makapi ya CCM!, good leaders are made and not born!. Nikashauri, Chadema ifanye incouragement kwa wanachama wake wenye uwezo na nia mbalimbali za kugombea, wajitanabaishe tangu sasa ili wapimwe, wawe groomed kuja kugombea mara wakati utakapo wadia na sio kusubiria kipenga cha NEC kipulizwe, by the time kipenga kinapulizwa, the time left will be too little too late!.
Nikatolea mfano wa jimbo la Kinondoni, linashikiliwa na CCM miaka nenda, miaka rudi. Mgombea wa CCM tayari anajulikana, weaknesess zake zinajulikana, kama mimi ni mwana Chadema na nina nia ya kugombea Kinondoni come 2015, nitasema sasa na wote wenye nia wajitangaze sasa ili miongoni mwetu, sote tujue nani ni best kutuletea ushindi, ndipo tumgroom tayari kwa kuiteka Kinondoni na sio kusubiri hadi 2015 na kusubiri CCM itamsimamisha nani!.
Mfano kwa Mwaka 2015, Jimbo Ubungo, kwa vile jimbo limeshikwa na upinzani, CCM huenda itampeleka mtu very strong ili kulikomboa, Jimbo la Kawe, CCM itamrudisha Kippi, na majimbo yote yanayoshikiliwa na wapinzani, CCM itapeleka watu makini, au wenye fedha na very strong, ili kuyagomboa, hivyo kama mimi ni mwana Chadema, najijua uwezo wangu kuiletea Chadema ushindi kwa jimbo fulani ni mkubwa kuliko mbunge aliyepo, mfano jimbo la Kawe ni mkubwa kuliko uwezo wa Halima Mdee kulitetea jimbo la Kawe, nitaonyesha nia sasa kwa kujenga mtandao wa mazingira ya ushindi. Muda kuchukua fomu ukifika, mimi nitachukua fomu kwa jimbo la Kawe, na Halima Mdee nae atachukua fomu, Ben Saanane nae atajaza na Mzee Mwanakijiji pia atajaza, Chadema kitatupima wote, ni nani mwenye uwezo zaidi na chances kubwa za ushindi, kinampitisha kupeperusha bendera ya Chadema, kama sio Halima, then Halima Mdee anakuwa ndio mhamasishaji mkuu wa mgombea mpya wa Chadema Kawe. Baada ya kumuengua Charles Mwera Tarime, niliwaambia makosa yenu na jimbo mlilitoa sadaka bure kabisa kwa kukosa busara!.
Kwa sisi wapenzi wa demokrasia ya kweli ambao japo tuna vyama vyetu, tunaamini hakuna mwana Chadema yoyote, mwenye hakimiliki ya kuhodhi nafasi yoyote ya uongozi kuanzia chini hadi uenyekiti. Nafasi zote za uongozi ndani ya chama na nje ya chama, ni haki ya kila mwanachama mwenye sifa, vigezo na uwezo!. Kama Zitto anazo sifa, vigezo na uwezo, kwanini azuiliwe asigombee?!.
Kwa vile nilishasema toka juzi, jana, leo na kesho nitasema tena, na tena, mimi Pasco wa jf, nina chama na sio Chadema na kiukweli, CCM ndicho chama tawala kilichoko madarakani, namfagilia sana EL kama atakuwa ndie mgombea wa CCM, na nikasema kama afya yake ni mgogoro kuhimili pilika pilika za uchaguzi wa 2015, then the second best candidate kwa CCM awe ni John Pombe Magufuli!, sio nawafangilie ili washinde, bali CCM iwasimamishe wagombea wa aina hii ili muwatumie kama pace makers wenu, ili Chadema mteue wagombea makini wa kuwaletea ushindi na sio kuendelea kuteua wasindikizaji tuu wa mgombea wa CCM !.
Mwenye masikio na asikie!.
Pasco.
12:24 am
P