John Heche anastahili kuvaa viatu vya Freeman Mbowe

Okay ni wazo zuri
 
Kama ana huo uwezo wa kiuongozi atengeneze mazingira ya kumtoa Mbowe kidemokrasia na ayafanikishe. Mbowe ni over stayed mkt na hana mchango mpya wa kiuongozi uliobaki kwa cdm akiwa kama mkt. Abakie kuwa mshauri tu apishe damu mpya.
Kinachonishangaza tu ni kuoa Kuondoka kwa mbowe wanaofurahia sana ni wanaccm.

Hii inanipa mawazo sana🤣
 
Dah, Zitto tena?
Wakati huu CHADEMA ingekuwa ni historia!
 
Japo mimi sio Chadema, lakini naunga mkono hoja, Ili tuwe na CCM imara, tunahitaji opposition imara, Heche ataijenga Chadema imara kuliko hata Chadema hii ya sasa ambayo kiukweli....

P
Naona hamumtakii mema Heche! kwa kauli zenu hizi muda si mrefu Heche ataingia matatizoni huko CHADEMA! Mtanikumbuka.
Naamini Wakurya si wasaliti ila CHADEMA inapenda wasaliti!
 
Wewe utamfanya Heche ya mkute kama yaliyo mkuta Zitto.
 
Nipe sababu niondoe imani niliyonayo kwa Zitto.
Unataka huu nao uwe mjadali mwingine pembeni?
Huna kumbukumbu kabisa ya yaliyokuwa yakitokea wakati Zitto anapambana kumwondoa Mbowe kwenye uongozi, na kuishia kujisalimisha kwa Kikwete, hujui chochote kabisa juu ya mkasa huo?

Sawa, hata kama hayo hukuyaamini, na bado unataka watu watoe "sababu" za wewe kuondoa ""imani kwa zitto", kana kwamba hata ACT-Wazalendo hujawahi kuisikia?

Basi, ninakusihi uweke imani yako kwa Zitto aliyepo ACT-Wazalendo, kuliko kwa Zitto ambaye angebaki na kuimaliza CHADEMA.
 
Propaganda zilizoasisiwa na waoga ndani ya chama.

Sitoshangaa propaganda kama hizo zikilengwa kwa heche in near future.
 
Propaganda zilizoasisiwa na waoga ndani ya chama.

Sitoshangaa propaganda kama hizo zikilengwa kwa heche in near future.
LOooo!

'Propaganda' tena? Hivi unanichukulia mimi kuwa kiwango hicho cha kulishwa propaganda?
Umenidhalilisha mkuu 'Gagnija', sijui kwa nini umeamua kufanya hivyo!

Basi, na yaishe, wewe endelea na "imani" yako kwa kiongozi ambaye mimi sioni namna ninayoweza kumwekea imani kama yako katika kusimamia maslahi ya taifa hili.
 
John mrema sijawahi kumkubali kabisa, anafaa kwenye kitengo chake Cha foreign affairs ila sio kwenye active political post!! Hana ushawishi wa kisiasa kabisa otherwise hao wengine uliowataja ni potential sana
 
Kinachonishangaza tu ni kuoa Kuondoka kwa mbowe wanaofurahia sana ni wanaccm.

Hii inanipa mawazo sana🤣

Ilikuwa hivyo enzi zile kabla ya ile sera ya kubadili gia angani na matokeo yake yaliyo iondoa cdm kwenye reli hadi hivi tunavyo andika hapa.

Lakini mambo si hivyo tena, kinacho itesa CCM ni je Mbowe na baadhi ya wanaoongoza naye cdm leo wakiondoka wataokakuja tutaweza kuweka cdm mfukoni chini ya uongozi mpya? CCM maombi yao ni Mbowe na genge lake waendelee kuwa viongozi cdm kuliko cdm kupata uongozi mpya wa Kitaifa ambao hautasimikwa na CCM.

Kama Dr Bashiru kasema kidogo tu kutofautiana na agenda kuu ya CCM ametikisa. Vipi kutakapo kuwa na cdm angalau ikawa kama ile ya Dr Slaa kipindi kile inayo vuna hoja zenye nguvu za Watanzania na kuzichukua na kuzifanyia kazi?
 
Daah! Kweli Kila mtu anaona tofauti!... Hivi kweli unaweza ukamlinganisha Heche na Wenje, John Mrema au Hata huyu Mnyika aliyepoa siku hizi... Heche level yake pale Chadema ni Lissu na Mbowe. Huyu mtu anajua kupanga hoja aisee, labda kama Huwa humfuatilii..
 
✔️
 
Naunga Mkono Hoja

Heche alimakazia Jiwe alivyoenda Tarime
Hatetereki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…