John Heche: Chadema itachapisha na kusambaza nakala za mkataba wa Samia na Dubai

Imalamawazo

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2021
Posts
1,343
Reaction score
3,269
Akihutumia maelfu ya wananchi wa Muleba 29.07.2023, mh Heche amesema Chadema itachapisha na kusambaza nakala za mkataba wa Samia na DP world hadi vijiweni.
My take: Ngoma inazidi kuwa tamu. Hakuna neno litakalo baki limestirika. Wanabaki uchi wa mnyama.
 
Kuuchapisha na kuusambaza ndio suluhisho? Mbona wao Chadema hawajawahi kuuchapisha na kuusambaza mgawanyo wa ruzuku wanazopokea Toka Serikalini?
 
Hili ni wazo nzuri ila utafsiriwe kwa kiswahili na ikiwezekana kwa kilugha.
Mfano; Kihaya, kinyakusa, kimasai, kiljaluo, kikurya, kisukuma, kimbulu, kichaga, kipare, kisafa na kadhalika.
Hahaaa, kabisa watu wote hata wamasai na wasukumu wajue content za mkataba. Siku wakiambia wanatakiwa wampishe mwarabu Ngorongoro wawe wanajua ni kifungu kipi cha mkataba kimetumika kuwaondoa.
 
hao vibaraka wakimaliza hizo pesa walizopewa watatulia. Mkataba umeshapita tunasubiri utekelezaji. Hao wananchi amewafundisha mpaka waweze kuuelewa wakati hata yeye mwenyewe ameshindwa kuuelewa. CHADEMA kweli imechoka, chama cha kudandia ajenda hawanaga ajenda zao. Leo wanamsifu Magufuli, wanafiki wakubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…