Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema kuwa chama hicho hakiogopi vitisho, ukandamizaji wala hila dhidi ya wapinzani, na kitaendelea kusimama kidete kutetea haki, uhuru na maisha ya Watanzania wote
Akizungumza Julai 23, 2025, wakati wa kutoa salamu za chama katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arumeru, Albert Elias Mollel, huko Ngaramtoni mkoani Arusha, Heche amesema kuwa taifa haliwezi kuendelea kwa viongozi wa umma kutumia mabavu kuwanyamazisha wanaowakosoa
Aidha Heche ametoa matumaini kwa wanachama wa CHADEMA na Watanzania wote waliopoteza imani, akisema kuwa ushindi wa mabadiliko ni suala la muda tu
Na kwanini serikali iliyoko madarakani itumie nguvu kujibu hoja za upinzani? Nimekuwa nikijiuliza sana kwanini nchi za Africa pekee ndio wang'ang'ania madaraka kuliko nchi zilizoendelea