Pre GE2025 John Heche: Makonda anawahoji Polisi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM kwasababu anawaona kama green guard

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Anayewatetea polisi wa Tanzania wewe ni adui mkubwa wa raia wa Tanzania wasio na makosa. Kama hujawahi kuathiriwa na vitendo vya polisi utawatetea. Nimewahi kimfanyia kazi polisi aligoma kunilipa Tena Kwa dharau!
Mimi nilipenda style ya magufuri na Lugola dhidi ya mapolisi. Haijalishi ni polisi ahojiwe hadharani.
 
Kweli kabisa ndugu! Ila CHADEMA hawatakuelewa!
 
Police wanalinda chama na makonda ndie boss wa chama
 

Chama kinaiwajibisha serekali kupitia njia ya watendaji, madiwani na bungeni, na sio hadharani mwenezi kuleta maigizo. Kwenye vikao vya watendaji, madiwani na bungeni huko ndio chama kinapaswa kupewa majibu na serekali. Kama Makonda alitaka majibu toka kwa RPC sio hadharani maana huo ni usanii, angekaa na RC ama Waziri wa mambo ya ndani apewe majibu ya kiutendaji.

Kwa watu wajinga tu ndio wanaweza kuamini hayo maigizo kuwa ni kutaka kutatua matatizo ya wananchi. Na ukitaka kujua hakuna chochote Cha maana kitafanyika, hayo matatizo anayosema anatatua Makonda kesho yataendelea, na nchi nzima yataendelea kuwepo, maana sio uwajibikaji wa kitaasisi, Bali ni maigizo ya mjanjanja mmoja anayejifanya anasaka kura, wakati kiuhalisia hao hao polisi ndio watakaogizwa na ccm kusimama chaguzi za wizi.
 
Wewe mnywa mbege huwezi kumkubali Makonda wewe endelea Kushabikia mwenyekiti wenu Makengeza!
Makonda ndio nani? Bashite? Hilo jina la Makonda amelitoa wapi?

Mmekuwa mkitupigia kilele eti Bashite anatatua matatizo ya wananchi kwenye ziala zake.

Nimekuuliza swali dogo tu, tueleze tatizo moja tu la wananchi ambalo Bashite amelitatua ktk ziala zake. Naona unarukaruka tu

TUAMBIA MATATIZO YA WANANCHI AMBAYO BASHITE AMEYATATUA KTK ZIALA ZAKE
 
Ziala ndo nini wewe Mangi? Nenda kwanza shule ndo uje hapa kubishana na mimi!
 
Ziala ndo nini wewe Mangi? Nenda kwanza shule ndo uje hapa kubishana na mimi!
Mimi na Bashite kwenye elimu hatuchekani🤣🤣ila kwenye biashara nimemuacha mbali. Bro unaonekana wewe ni msomi sana. Chukua mauwa yako🌼🌷🌻💐🥀
 
Mimi na Bashite kwenye elimu hatuchekani🤣🤣ila kwenye biashara nimemuacha mbali. Bro unaonekana wewe ni msomi sana. Chukua mauwa yako🌼🌷🌻💐🥀
Wewe unabiashara kumzidi Makonda? Kanywe mbege kaka na kasimamie biashara za Makengeza!
 
Wewe ni mpumbavu namba mbili baada ya kiongozi wako Heche!
Hebu Chadema tuambieni kama sio nyinyi kila siku mnalalsmika humu mitandaoni kwamba Polisi haifuati PGO?
Kwamba jeshi la Polisi linawabambika kesi raia nk!
Sasa li- chama la hovyo kama hili limejaa chuki saa yote mnawaza ubunge tu!

Kisa Makonda kawapeleka puta na anazidi kujiongezea umaarufu kwenye jamii kila anakopita nyinyi shwine wa Mbowe mnazidi kumsakama.
Chadema hamjitambuwi!
 
Wewe ni CCM?
 
ChukuwaChakoMapema wamekamata Nchi! Mpaka wafe!
 
Huwa nashangaa sana watu wanavyohoji sana nguvu ya makonda

Kanuni ya utumishi wa umma mojawapo inasema "Utii kwa serikali"

Kwa sasa serikali inaongozwa na ccm
Hii ni chungu-tamu ila hamna namna
Kama mtumishi wa umma hutaki kelele acha kazi kaa pembeni
Makonda hautamsikia
No hard feeling but that is how it is 😪
 
Kumuelewa Heche inaitaji uwe na akili kubwa na timamu. Majoka wengi wa kijani akili hizo hamna
 
Pumba. Bashite hana cheo cha kiserikali. Yeye anatakiwa awawajibishe kwenye vikao vyao vya kichama tu basi.
 
Chadema ni wanafiki wakubwa. Ni viongozi wenye mwelekeo wa kimapinduzi tu ndani ya chama cha mapinduzi ndio wanaweza kufanikisha vita vya utawala bora nchini. Wananchi wameona na kushuhudia chini ya magufuli ufisadi na uzembe kupungua kwa kiwango kikubwa. Nyia ya kiliberali ya chadema imejaa unafiki mtupu. Wanasema eti utawala wa sheria wakijua mabwanyenye na fisadi wana uwezo wa kununua haki kwa wanasheria. Wananchi wanachohitaji ni utawala wa haki. Sheria ziko ila wanasheria wanageuza haki bidhaa chini ya sera za kiliberali ambazo hazitufai afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…