SI KWELI John Heche nikiteuliwa kuwa CAG nitashauri sekta zenye hasara kufanya kazi bila usimamizi

SI KWELI John Heche nikiteuliwa kuwa CAG nitashauri sekta zenye hasara kufanya kazi bila usimamizi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kumekuwepo na machapisho kadhaa yanayosambazwa kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii hususani facebook kufuatia kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, John Heche, alipozungumza na vyombo vya habari. Mojawapo ya machapisho hayo linadai kuwa amesema:

Heche CAG.jpg
Nukuu Heche 1.jpg
Nukuu Heche 2.jpg
Nukuu Heche 3.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na machapisho kadhaa yanayosambazwa kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii hususani facebook kufuatia kauli ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa-Bara, John Heche, alipozungumza na vyombo vya habari. Mojawapo ya machapisho hayo linadai kuwa amesema:

“Leo hii mimi nikiteuliwa kuwa CAG nitamshauri Mhe. Rais sekta zote zilizozosababisha hasara zisifanye kazi peke yake bila usimamizi. Ni vile itikadi za chama changu haziruhusu kuteuliwa japo mimi niko tayari kuwatumikia Watanzania.”

Dai hili limejiri mara baada ya makamu mwenye kiti wa CHADEMA kuzungumza na vyombo vya habari tarehe Aprili 06, 2026

Uhalisia wa Nukuu hiyo ni upi?

Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa kwa kutumia nyenzo za kidijitali ikiwemo Google Reverse Image Search na keyword search, umebaini kuwa kauli hiyo si ya kweli na haikutolewa na John Heche. Badala yake, imeundwa na kusambazwa kwa lengo la kupotosha umma kuhusu kile alichokisema wakati wa mahojiano yake na vyombo vya habari.

Aidha, katika maelezo yake halisi, John Heche hakugusia kabisa suala la yeye kuteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), wala kuzungumzia kuondoa au kupunguza usimamizi katika sekta za umma.

Katika wasilisho lake, alijikita zaidi kwenye masuala ya kiuchumi, hususan kupanda kwa bei ya mafuta nchini Tanzania hadi kufikia takribani shilingi 4,000 kwa lita. Alielezea athari za hali hiyo kwa maisha ya wananchi na uchumi kwa ujumla, akihusianisha na sera na mwelekeo wa uendeshaji wa nchi.

Hata ni wazi kuwa kauli inayosambazwa mitandaoni imepotoshwa na haiwakilishi maudhui halisi ya alichokisema John Heche. Ufuatialiaji zaidi umebaini kuwa grafiki hiyo pia haijachapishwa na CHADEMA katika ukurasa wake wowote wa kijamii ikiwemo X (Twitter) na Instagram.
Back
Top Bottom