Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche akaanga vibaya OCD mbele ya umati wa wafuasi wa Chama hicho.
"Natamani ningekuwa na muda na hayo maelekezo unayopokea kwa Kihongosi, ningekuwa na muda ningepambana na wewe tuone ungenifanya nini mimi sio mke wako, huna cha kunifanya"
Lisu alimkaanga kabisa RPC mkutano wa hadhara kule Kusini Ruvuma walipotaka polisi kumkamata Lisu,Lisu akasema kwa jiamini hakamatwi mtu hapa Mthubutu muone cha mtema kuni nyie Polisi CCM
Polisi wakaingia kazini kumkamata Lisu ,Walinzi wa Lisu wakaingia mitini na wananchi wakatokomea gizani kusikojulikana wakamuacha Lisu apambane na hali yake
.Na Heche mwenyewe alikuwepo akamwacha Lisu akamatwe kama kuku wa Mdondo .Akaingia mitini
Kuna warriors wengi wa aina tofauti kuna keyboard warriors wakiandika waweza dhani serikali inapinduliwa kesho kumbe hewa tu
Kundi la pili ni la Mouth warriors akiwemo Lisu , Heche na Godbless Lema,manabii koko,maaskofu koko nk .Wakiongea ooh sisi hatuogopi polisi tuko tayari kupambana nao hao Polisi CCM division zero wakihutubia kupata makofi ya cheap popularity waweza dhani ooh polisi na nchi kesho wameisha na nchi inapinduliwa na huyu kidume asemaye haogopi RPC wala OCD wala polisi kwenye hotuba yake
Polisi wakitaka kuwakomalia kuwakamata au kuwatishia kidogo tu wanatorokea nje ya nchi,vyooni na kusikojukiana kujifungia na kelele kibao za ooh polisi wanataka kunikamata au kuniua anaita vyombo vya habari
Sasa mtu kama alisema haogopi polisi apambane nao? Mechi ya bifu ichezwe kati ya polisi na huyo asiyeogopa polisi tuone mshindi
Wananchi mara ingine wakitoa statement kams hiyo ya Heche wazoomeeni hao wanasiasa