PreGE2025 John Heche: Polisi waliotukamata wamezunguka na sisi kwenye magari yao kisha kututelekeza barabarani

PreGE2025 John Heche: Polisi waliotukamata wamezunguka na sisi kwenye magari yao kisha kututelekeza barabarani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Matibabu dhidi ya Stockholm Sydrome ni pamoja na matibabu ya kisaikolojia
Kabla ya uchaguzi tulilaumu uongozi wetu uliokuwapo CHADEMA kuwa ulituzuia na kuvuta mashati yetu tusiende hatua ya juu ya kudai mabadiliko.

Tundu Lissu, John Heche na viongozi wengine tuliowachagua tukawapa moyo kuwa sasa ni sasa.

("tiba ya mazungumzo") na dawa ikiwa inahitajika kwa wataka mabadiliko
Sasa kumbe jibu unalo hapa, sasa kinachokutia wasiwasi ni kitu gani? Unataka dawa ifanye kazi kwa dozi moja tu? Uliona wapi matibabu ya aina hiyo!
 
Ni mfano wa makosa ya vuguvugu la mabadiliko kupewa mtu mmoja au viongozi wachache badala ya Nguvu ya Umma kuanzia kwao umma mpana, kisha Tundu Lissu akitoka jela anakwenda kwenye mazungumzo na watawala huku nyuma yake anaungwa mkono na kazi waliyokwishafanya nguvu ya umma.
Hata sielewi mawazo ya aina hii wewe umeyasikia wapi?
Umma wa wapi unaojiotea tu kama uyoga bila ya uongozi wowote ukaleta mabadiliko? Hayo uliyaona au kuyasikia wapi?
Unachoeleza wewe hata hakieleweki.
 
Ila maoni yangu Chadema wafanye movement zote lakini na busara iwaongoze.

Sehemu kama Kariakoo kiukweli kupeleka mikutano hapo ni kuleta usufumbu tu kwa watu, kama hauna jicho la kibiashara huwezi kuelewa logic ya kariakoo paachwe kama palivyo, njia za kuwafikishia ujumbe watu zipo nyingi.
Mbona Majaliwa kesha fanya hapo mara nyingi tu.
 
ndivyo inavyofaa kuwafanya vibaka na matapeli waropokaji wa kisiasa gentleman 🐒
Sister hiyo Mimba ukijaaliwa kujifungua salama, nakushauri huyo Mtoto mpe jina la CHADEMA, make kichefu chefu cha hiyo mimba isikiapo neno Chadema sio cha Sayari hii! 😁😁
 
Sister hiyo Mimba ukijaaliwa kujifungua salama, nakushauri huyo Mtoto mpe jina la CHADEMA, make kichefu chefu cha hiyo mimba isikiapo neno Chadema sio cha Sayari hii! 😁😁
calm down ndugu mropokaji,
jifunze kupokea ukweli bila mihemko :NoGodNo:
 
Kwa wenzetu wa Ulaya mambo kama haya yalifanyika karne ya 15 na 16. Sisi tunafanya karne hii ya kidigitali, Kiongozi unamkamata unatembea naye wee kisha unawachia njiani.

Aisee!!
 
Kwa wenzetu wa Ulaya mambo kama haya yalifanyika karne ya 15 na 16. Sisi tunafanya karne hii ya kidigitali, Kiongozi unamkamata unatembea naye wee kisha unawachia njiani.

Aisee!!
Mafuta yanapotea bure wanakula perdiem zao.
 
No Reforms No Election yetu inachezewa kama mwanasesere kwa kuwa ipo kwa viongozi 10,000 tu wa CHADEMA nchini kote ila sisi Nguvu ya Umma hii No Reforms No Election tumewaachia Tundu Lissu, Heche, Kamati Kuu ya CHADEMA na viongozi 10,000 walioenguliwa.

Kama nilivyosema inatakiwa Nguvu ya Umma ijitwike hii No Reforms No Election kwa maandamano makubwa nchi nzima tukidai pia Tundu Lissu aachiwe n.k

Hili la malaki ya wanachama na waTanzania kuwaachia viongozi 10,000 tu ncjini kote ndiyo walibebe ndiyo maana dola na watawala wanaona ni madai 'hewa' yasiyo na mashiko.

1745488659728.jpeg
 
Anaandika Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kupitia ukurasa wake wa X

"Ninawashukuru Watanzania wote, kwa mshikamono wenu wa kupiga vita udikteta katika Nchi yetu.Polisi waliotukamata wamezunguka na sisi kwenye magari yao kisha kututelekeza barabarani.Kesho saa saba mchana baada ya kikao cha viongozi wakuu wa chama tutazungumza na vyombo vya habari.Msiogope hata kidogo, tutashinda vita hii"
Soma Pia: John Heche akamatwa na Polisi Kariakoo


Ulitaka upelekwe polisi mwenyewe unajiona mwanamapinduuuuzi. CHADEMA wapuuzi sana😁😁
 
Ila maoni yangu Chadema wafanye movement zote lakini na busara iwaongoze.

Sehemu kama Kariakoo kiukweli kupeleka mikutano hapo ni kuleta usufumbu tu kwa watu, kama hauna jicho la kibiashara huwezi kuelewa logic ya kariakoo paachwe kama palivyo, njia za kuwafikishia ujumbe watu zipo nyingi.
Ccm huwa wanafanya mikutano kariakoo,nawenyewe hawana busara?
Mkutano sio vurugu,kazi ya polisi ni kulinda amani ikiwemo kwenye mikutano
 
Mambo yameiva ile cocktail mchanyato wa kuzindua Nguvu ya Umma ndani ya waTanzania wapole imefika, Historia ya Sharpville kule kwa watawala ya Ubaguzi kusini huenda sasa ikalipuka Tanzania

KUMBUKUMBU YA UASI DHIDI YA WATAWALA SHARPVILLE
CIC Julius Malema Addresses Sharpville Massacre Rally, 21 March 2025


View: https://m.youtube.com/watch?v=pxD24Vwdd4c
 
Haraka ya nini mkuu Bagamoyo!
Mambo haya hayaendi kwa pupa.
Wape waTanzania nafasi, watafanya kweli. Vuta subira mkuu!

Mkuu kwa hali iliyotokea leo 24 Aprili 2025 viongozi wetu ambao wanazidi 10,000 na kidogo baadhi ya kupigwa, kudhalilishwa huku wengine wakiwa mahabusu bado sisi Umma Mpana People's Power tujizuie au tujitokeze kuwa front kwa maandano nchini nzima yasiyo na kikomo.

Katika uzi huu nilichambua kisayansi haiba ya wadhalimu wetu kuwa walitaka kututenganisha na dhana ya No Reforms No Election kuwa ni ya watu wachache Tundu Lissu pamoja na viongozi wetu 10,000 walioenguliwa nchi nzima 27 November 2024 uchaguzi wa TAMISEMI.

Uchambuzi wangu umedhihiri leo wamewashambulia viongozi wetu na kuwatupa nje barabarani na nje ya mji.

Tungejitokeza hapa Dar es Salaam watu 50,000 hadi 100,000 wadhalimu hawa wasingeweza kututupa nje ya mji.

Lakini tumewabebesha msalaba viongozi wetu wachache 10,000 nchini kote, sisi kwa mamilioni tumekuwa watazamaji.


View: https://m.youtube.com/watch?v=8KuIoOKTNkM
 
Tungejitokeza hapa Dar es Salaam watu 50,000 hadi 100,000 wadhalimu hawa wasingeweza kututupa nje ya mji.

Lakini tumewabebesha msalaba viongozi wetu wachache 10,000 nchini kote, sisi kwa mamilioni tumekuwa watazamaji.
Madhila haya mazito kwa viongozi wetu hadi lini ?
1745507516717.jpeg
 
Katika uzi huu nilichambua kisayansi haiba ya wadhalimu wetu kuwa walitaka kutugenganisha na dhana ya No Reforms No Election kuwa ni ya watu wachache Tundu Lissu pamoja na viongozi wetu 10,000 walioenguliwa nchi nzima 27 November 2024 uchaguzi wa TAMISEMI.

Wadhalimu watesema kuwa ni nguvu ya nje ya nchi kama ya Martha Karua n.k ndiyo inataka mabadiliko pamoja na viongozi 10,000 wa CHADEMA huku sisi mamilioni ya raia tumejificha na kushindwa kujitokeza kufanya maandamano ya maelfu ya raia bila kikomo kudai No Reforms No Election

1745507739282.jpeg
 
Back
Top Bottom