Nguvu ya umma kama ya yule Venancio Mondlane naona haipo kabisa, katika uhalisia nchini Tanzania.
Kabla ya mapinduzi ya kiuongozi ndani ya CHADEMA kupitia uchaguzi wa mfano wa kidemokrasia tuliamini sasa chama chetu kitakuwa na msukumo zaidi wa Nguvu ya Umma
Lakini inaonesha ni viongozi tu pekee yao ndiyo wana moto lakini kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wao hawajabadilika.
Viongozi watakata tamaa kuona umma wa waTanzania hautekelezi yale wanayodai kuwa walikuwa tayari wana moto wa manadiliko lakini walizuiwa na uongozi uliopita ndiyo maana wakafanya kila lililo katika nafasi zao uongozi mpya upatikane ndani ya CHADEMA .
Lakini ukweli umedhihiri waTanzania hawapo tayari kwa mabadiliko.
View attachment 3312708
Mwenyekiti Tundu Lissu alipigwa risasi 16 mwilini kesi ya waliohusika na shabulio hata faili halikufunguliwa, Tundu Lissu sasa yupo mahabusu kwa kesi ya Uhaini inayokwenda fasta fasta kiuchunguzi.
Makamu mwenyekit John Heche naye 'alitekwa' kwa muda wa masaa kadhaa na kuzungushwa hadi kiza kisha kutelekezwa barabarani usiku.
Freeman Mbowe naye kesi ya ugaidi aliwekwa mahabusu kwa miezi kibao kabla ya tuhuma kufutwa.
Uchaguzi wa TAMISEMI 2024 mamia ya viongozi wa CHADEMA ngazi za ubalozi, wenyekiti wa mitaa, vijijji walifanyiwa vitimbi kibao kukatwa, kuporwa matokeo n.k
Nguvu ya Umma imeshindwa kunyanyuka na kusema sasa basi kwa kuingia mitaani katika wilaya zote, mikoa ambapo viongozi wao wa ngazi zote walifanyiwa uhuni.
Tarehe 24 April 2025 Tundu Lissu anaweza kuwa hana wa kumuunga mkono zaidi ya viongozi wachache wa chama na jopo la mawakili nguli watetezi lakini Nguvu ya Umma haitakuwepo kuonesha umuhimu wao nje ya mifumo wa haki jinai, mfumo wa uchaguzi ambapo ingechukua dhana ya People's Power kusitisha vitiimbi vya watawala.