1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,802
- 10,307
Anaandika Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kupitia ukurasa wake wa X
"Ninawashukuru Watanzania wote, kwa mshikamono wenu wa kupiga vita udikteta katika Nchi yetu.Polisi waliotukamata wamezunguka na sisi kwenye magari yao kisha kututelekeza barabarani.Kesho saa saba mchana baada ya kikao cha viongozi wakuu wa chama tutazungumza na vyombo vya habari.Msiogope hata kidogo, tutashinda vita hii"
Soma Pia: John Heche akamatwa na Polisi Kariakoo
Kuna kitu naliona hakipo sawa ndani ya Chadema .
Ama wawafukize G55 au waitishe kikao cha dharura kisha kura zipigwe kupinga ama kukubaliana na maoni ya G55 .
Wakishindwa kwanye kura basi wakubali kuwa maamuzi ya wengi ndiyo Demokrasia.
No Reform No Election ilikua ni ya Mbowe lakini Mrema kwa makusudi ameamua kuunda Genge ndani ya Chama na kutumia media mara kwa mara kueneza uongo na chuki kuliko hata CCM.
Mrema ni Kati ya wachaga wabinafsi na wenye Roho Mbaya kuliko Mtanzania yeyote .
Haiwezekani Mtu aliyefanya mambo makubwa ndani ya Chama kama Lisu mpaka akachaguliwa kugombea Urais akiwa Hospitalini Ubelgiji baada ya kupigwa risasi 16 , hakuwahi kuomba kugombea urais wala umakamu wa Mwenyekiti wakati huo zaidi ya kuteuliwa na chama halafu leo yupo tena Gerezani kwa kesi ya uhaini wakati anakipigania Chama akiwa na ulemavu na risasi Mwilini ; John Mrema kwa roho yake Mbaya anaitisha tena vyombo vya habari na kuendeleza harakati za kuua chama na ili kujifurahisha CCM halafu arudi CCM kugombea kama anavyoahidiwa .
Nilifikiri anaitisha vyombo vya habari kutoa msimamo wa kulaani Kitendo cha Mwenyekiti kukamatwa na kufunguliwa kesi ya Uhaini badala yake anasema uchaguzi utakua wa haki na huru utakaoinua ndoto za watu ndani ya Chadema .
Yaani wanawaza kupata viti maalumu vya bure kwa wanawake zao ili wawapelekee mil.2 kila mwezi . Wanataka mfumo ule ule wa kupeleka watu wao kinyemela eti ndizo ndoto za Watanzania .
Pumbavu kabisa .
Yaani anawaza kufa kwa ndoto za wake zake lakini hawazi kufa na kutekwa kwa vijana mamia wakati wa uchaguzi . Huyu hajui kuwa CCM wanajifanya wema kwa sababu wanaona Chadema hawajaeleweka. Leo hii Chadema wakisema wanashiriki kwa sheria azilizopo na tume yake ndipo vita inapoonekana .
Ushauri wangu . Mrema Afukuzwe kwanza yeye peke yake .
Vyama vyote duniani vinakosoana lakini sio kuunda chama ndani ya Chama .
Mpaka sasa G 55 ni Chama kamili ndani ya Chadema . Ni chama chenye uongozi ,vikao vyake ,slogano yake ,mikakati yake na malengo yake tofauti na Chadema .
Haraka sana utaratibu ufuatwe kipengele baada ya kipengele ili Mrema afukuzwe haraka sana . Atakua chama au watasababisha madhara makubwa sana ndani ya chama ikiwemo kutumika kuwaua baadhi ya watu ndani ya Chama. Yule mtu kwa wanaosoma saikolojia ni mtu mwovu sana hata kwa kuongea tu unaisoma sura yake. Ameweka pesa mbele kuliko kitu chochote . Ubunge anautaka kutimiza ndoto zake binafsi sio kulinda uhai wa watu na rasilimali za umma ili kuleta maendeleo endelevu .
Narudia tena Chadema Mfukuzeni John Mrema.