John Heche: Walio Madarakani Wanatengeneza umasikini, Deni la taifa lafika Trilioni 94. Bandari ya Dar yazidiwa na Mombasa

Chama Cha demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Nyasa kimefanya kongamano la kisiasa lenye lengo la kutoa elimu kwa wanachi juu ya haki zao.

Mhe. Mchg. Peter Msigwa, mbunge Mstaafu wa Iringa Mjini, Joseph Mbilinyi, Mbunge Mstaafu wa Mbeya Mjini na Mbunge Mstaafu wa Tarime Mhe. Heche ni baadhi ya viongozi waliotoa salamu ambapo wameshauri serikali kutatua changamoto za wananchi ikiwemo Pembejeo za Wananchi.

John Heche akihutubia kwenye Kongamano la CHADEMA Mkoa wa Iringa miaka 61 ya Uhuru, haya ndo kayasema:

*Hatuwezi kutatua matatizo tuliyonayo kwa kujidanganya kwamba hayapo.

*Tatizo kubwa la Umasikini sio kwa sababu sisi hatuna Rasilimali. Umasikini wa Tanzania ni Umasikini wa Kutengenezwa na Viongozi wa chama cha Mapinduzi

* Tanzania tuna kila kitu. Sisi ni nchi ambayo Mungu ametujalia bandari.

*Bandari ndo Mpango Mkuu wa Mizigo wa biashara. Wakati wa wakoloni, Miji iliyokuwa ya kwanza ilikuwa miji kando kando ya bahari

*Tanzania Mungu ametupa Bandari 5. Bandari ya Dar, Tanga, Mtwara, Bagamoyo, Bandari ya Ziwa Victoria inaunganisha Kenya Uganda na Tanzania. Mungu akupe nini?

* Tuna Madini ya Nickel na uranium, Tuna Gesi Makaa ya Mawe, Misitu, dhahabu, Tanzanite nk

*Nchi yetu haina hata kipande cha jangwa. Tanzania ukubwa wake ni sawa uunganishe Kenya, Uganda Rwanda na Burundi . Tuna mbuga za Wanyama

*Mungu ni Mtanzania.

* Leo wakisema Mungu anakuja na kuingilio ni laki moja, wote wataenda Motoni.

*Tumejenga Bomba la Tazama kutoka Dar hadi Zambia lakini Dar eti haina maji wakati maji yaliyopo chini Kimbiji ni ¾ ya maji ya Ziwa Victoria. Tungejenga bomba la Maji tungesambaza Nchi nzima

* Tanzania tunaagiza ngano 90%. Tunaagiza ngano kutoka Jangwani Saudi Arabia

* Wanaona Watanzania wakipata hela wanataka hela wawe nazo wakina Ridhiwani Kikwete na Janwari Makamba wengine wawe ombaomba sababu ya roho mbaya zao.

*Kagema alisema "Akipewa bandari ya Dar peke yake hatochimba madini bali atakuwa na uwezo wa kuitumia afrika yote". Tanzania imezungukwa na nchi zisizo na bandari. Kupitisha gari bandarini tunalipwa. Gari kaagiza mtu wa Kongo na kanunua mwenyewe lakini anatulipa.

* Bandari ya Tanzania inapitisha Mzigo Tani Milioni 17 wakati Kenya bandari ya Mombasa wanapitisha Tani Milioni 34. Hii ni kwa Mwaka 2020/2021.

*Hapa ninapotaka kuzungumza bandari yetu haifanyi kazi kwa ufanisi nimehongwa na nani? Mimi nasema nyie Mlioko na wengine wote Mafisadi, na CCM inayowasimamia, imeshindwa kusimamia bandari ilete pesa kwenye Nchi yetu ili tusichangishe watu kwenye matozo tutumie hizo pesa za bandari kuwapa Wananchi wetu huduma. Kusema hivyo nimehongwa na nani?

*Yaani leo rais Samia Suluhu hawezi kuendesha Nchi hadi achangishe kitu kinaitwa TOZO.

*Nawaambia jamani, Tumieni bandari Vizuri ili msitoze Tozo. Wanasema nimehongwa, mimi na wao nani kahongwa? Wanaoteta huo ujinga na mimi ninayesema hamna uwezo wa kuongoza nchi. Nani amehongwa?

*Serikali ya CCM na Watu wengine waliopo CCM wamefika mwisho wa Kufikiri. Leo hatuna maji miaka 61 ya Uhuru. Tunajadili maji tena sio Vijijini bali Mjini Dar es Salaam, je Vijijini hali ipoje? Tumefikishwa hapa na kiwango cha chini cha fikra ambacho kimeshindwa kusimamia Mungu alichotupa.

* Deni la Taifa limefika Trilioni 91 kutoka Trilioni 71 alizoacha Hayati Magufuli. Mwigulu jana kakopa Korea Trilioni 2.4 hivyo sasa tunaenda Trilioni 94.

* Kila mwezi Tanzania inalipa Bilioni 800 kulipa Mkopo. Mapato ni shilingi ngapi?
View attachment 2442561View attachment 2442563View attachment 2442564View attachment 2442571View attachment 2442579
Rose Mayemba Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Njombe
Mbona cdm ni wepesi kusahau kana kwamba hili ni jambo jipya. Yule baba aliyekuwa hana TOZO na aliyekuwa akiwaambia hii nchi ni tajiri mliishia kumtukana. Alipokuwa anajitahidi kufanya maendeleo ya vitu. Mkasema kwa sauti moja hatutaki maendeleo ya vitu tunataka maendeleo ya watu. Kulikoni leo!!!!????
 
Co wakati wa .kujadili habari za marehemu now
Mbona cdm ni wepesi kusahau kana kwamba hili ni jambo jipya. Yule baba aliyekuwa hana TOZO na aliyekuwa akiwaambia hii nchi ni tajiri mliishia kumtukana. Alipokuwa anajitahidi kufanya maendeleo ya vitu. Mkasema kwa sauti moja hatutaki maendeleo ya vitu tunataka maendeleo ya watu. Kulikoni leo!!!!????
 
Haya yote ni matunda ya mfumo mbovu alioujenga Nyerere
Marais wa nchi hii ni majalala ya muda wote. Kumbuka Nyerere kaipokea TZ ikiwa haina wasomi, haina miundo mbinu ni sawa na mtu anayepewa nyumba ya kuishi ikiwa tupu kabisa anaanza kununua makochi, mafriji na vitu vyote vya ndani.
 
Mlamba asali mmoja alisema mama atawale adi 2035 ili waendelee kuitafuna nchi. uyu mama adi atakapostaafu kuna wapuuzi watakuwa wamejitajirisha vibaya mno maana sidhani kama uyu bib anafahamu kuwa yey ni rais wa nchi
 
Hapo kwenye 'Mungu ni Mtanzania' hapo imebidi niweke kituo nivae miwani kwanza lakini bado sijaambulia nukta gani hasa mh. Heche alikusudia hadhira tuijue.
 
Marais wa nchi hii ni majalala ya muda wote. Kumbuka Nyerere kaipokea TZ ikiwa haina wasomi, haina miundo mbinu ni sawa na mtu anayepewa nyumba ya kuishi ikiwa tupu kabisa anaanza kununua makochi, mafriji na vitu v

Nyerere alirithi shule, hospitali, viwanda, na mambo mengine mengi kutoka kwa wakoloni
 
Chama Cha demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Nyasa kimefanya kongamano la kisiasa lenye lengo la kutoa elimu kwa wanachi juu ya haki zao.

Mhe. Mchg. Peter Msigwa, mbunge Mstaafu wa Iringa Mjini, Joseph Mbilinyi, Mbunge Mstaafu wa Mbeya Mjini na Mbunge Mstaafu wa Tarime Mhe. Heche ni baadhi ya viongozi waliotoa salamu ambapo wameshauri serikali kutatua changamoto za wananchi ikiwemo Pembejeo za Wananchi.

John Heche akihutubia kwenye Kongamano la CHADEMA Mkoa wa Iringa miaka 61 ya Uhuru, haya ndo kayasema:

*Hatuwezi kutatua matatizo tuliyonayo kwa kujidanganya kwamba hayapo.

*Tatizo kubwa la Umasikini sio kwa sababu sisi hatuna Rasilimali. Umasikini wa Tanzania ni Umasikini wa Kutengenezwa na Viongozi wa chama cha Mapinduzi

* Tanzania tuna kila kitu. Sisi ni nchi ambayo Mungu ametujalia bandari.

*Bandari ndo Mpango Mkuu wa Mizigo wa biashara. Wakati wa wakoloni, Miji iliyokuwa ya kwanza ilikuwa miji kando kando ya bahari

*Tanzania Mungu ametupa Bandari 5. Bandari ya Dar, Tanga, Mtwara, Bagamoyo, Bandari ya Ziwa Victoria inaunganisha Kenya Uganda na Tanzania. Mungu akupe nini?

* Tuna Madini ya Nickel na uranium, Tuna Gesi Makaa ya Mawe, Misitu, dhahabu, Tanzanite nk

*Nchi yetu haina hata kipande cha jangwa. Tanzania ukubwa wake ni sawa uunganishe Kenya, Uganda Rwanda na Burundi . Tuna mbuga za Wanyama

*Mungu ni Mtanzania.

* Leo wakisema Mungu anakuja na kuingilio ni laki moja, wote wataenda Motoni.

*Tumejenga Bomba la Tazama kutoka Dar hadi Zambia lakini Dar eti haina maji wakati maji yaliyopo chini Kimbiji ni ¾ ya maji ya Ziwa Victoria. Tungejenga bomba la Maji tungesambaza Nchi nzima

* Tanzania tunaagiza ngano 90%. Tunaagiza ngano kutoka Jangwani Saudi Arabia

* Wanaona Watanzania wakipata hela wanataka hela wawe nazo wakina Ridhiwani Kikwete na Janwari Makamba wengine wawe ombaomba sababu ya roho mbaya zao.

*Kagema alisema "Akipewa bandari ya Dar peke yake hatochimba madini bali atakuwa na uwezo wa kuitumia afrika yote". Tanzania imezungukwa na nchi zisizo na bandari. Kupitisha gari bandarini tunalipwa. Gari kaagiza mtu wa Kongo na kanunua mwenyewe lakini anatulipa.

* Bandari ya Tanzania inapitisha Mzigo Tani Milioni 17 wakati Kenya bandari ya Mombasa wanapitisha Tani Milioni 34. Hii ni kwa Mwaka 2020/2021.

*Hapa ninapotaka kuzungumza bandari yetu haifanyi kazi kwa ufanisi nimehongwa na nani? Mimi nasema nyie Mlioko na wengine wote Mafisadi, na CCM inayowasimamia, imeshindwa kusimamia bandari ilete pesa kwenye Nchi yetu ili tusichangishe watu kwenye matozo tutumie hizo pesa za bandari kuwapa Wananchi wetu huduma. Kusema hivyo nimehongwa na nani?

*Yaani leo rais Samia Suluhu hawezi kuendesha Nchi hadi achangishe kitu kinaitwa TOZO.

*Nawaambia jamani, Tumieni bandari Vizuri ili msitoze Tozo. Wanasema nimehongwa, mimi na wao nani kahongwa? Wanaoteta huo ujinga na mimi ninayesema hamna uwezo wa kuongoza nchi. Nani amehongwa?

*Serikali ya CCM na Watu wengine waliopo CCM wamefika mwisho wa Kufikiri. Leo hatuna maji miaka 61 ya Uhuru. Tunajadili maji tena sio Vijijini bali Mjini Dar es Salaam, je Vijijini hali ipoje? Tumefikishwa hapa na kiwango cha chini cha fikra ambacho kimeshindwa kusimamia Mungu alichotupa.

* Deni la Taifa limefika Trilioni 91 kutoka Trilioni 71 alizoacha Hayati Magufuli. Mwigulu jana kakopa Korea Trilioni 2.4 hivyo sasa tunaenda Trilioni 94.

* Kila mwezi Tanzania inalipa Bilioni 800 kulipa Mkopo. Mapato ni shilingi ngapi?
View attachment 2442561View attachment 2442563View attachment 2442564View attachment 2442571View attachment 2442579
Rose Mayemba Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Njombe
Hizi nondo zimeshiba
 
Nyerere alirithi shule, hospitali, viwanda, na mambo mengine mengi kutoka kwa wakoloni
Kazi aliyoifanya ni ngumu sana kumbuka alisomesha mainjinia wote waliokuja kuajiriwa baadae kina Hayati Mfugale.

Waliojenga miundo mbinu mingi nchi nzima na hayati JPM ni wasomi waliosomeshwa bure na Baba wa Taifa miaka hiyo ya 1960-70.
 
Msisahau pia nyinyi mlikuwa mnapiga kelele na kumlaumu Magufuli kuwa ananunua ndege kwa cash badala ya kununua kwa mkopo! Unafiki ulioje!

..tulipinga ununuzi wa ndege sio kwasababu zimenunuliwa cash, bali kwasababu biashara ya shirika la ndege ni ya hasara.

..tumenunua ndege 11 cash toka kwa mabeberu.

..halafu tuna kesi 19 ktk mahakama za mabeberu kwasababu Jpm amevunja mikataba nao kihuni.

..mabeberu wanazisaka hizo ndege wazikamate.
 
Tukubali tu Chadema ndo mkombozi wa hili Taifa

The others utilise matumbo yao na familia zao na marafiki zao na UJINGA ndo mtaji wao

RETHINK
Dah.....siyo chadema hii mkuu ya Mbowe na TL 🤣 🤣 🤣
 
Mbona cdm ni wepesi kusahau kana kwamba hili ni jambo jipya. Yule baba aliyekuwa hana TOZO na aliyekuwa akiwaambia hii nchi ni tajiri mliishia kumtukana. Alipokuwa anajitahidi kufanya maendeleo ya vitu. Mkasema kwa sauti moja hatutaki maendeleo ya vitu tunataka maendeleo ya watu. Kulikoni leo!!!!????

..maendeleo ya vitu ni kama tunato sadaka kwa mabeberu.

..tulinunua ndege 11 lakini tuna kesi 19 ktk mahakama kimataifa na wawekezaji.

..Na kila wakitushinda wanakamata ndege yetu.

..Ni afadhali fedha hizo zingewekezwa kwenye KILIMO au UFUGAJI umasikini ungepungua.
 
Usisahau ya kwamba maendeleo ya vitu yana jumlisha miundombinu kama barabara. So utasafirisha vipi mazao na mifugo kwenda kwenye masoko kama huna miundombinu safi.
 
Back
Top Bottom