..mimi nilipinga ununuzi wa ndege tangu wakati wa JK.
..nimejiridhisha kwamba shirika la ndege ni biashara isiyo na faida kwetu.
..ndege zetu kukamatwa ni kutokana na maamuzi ya kipumbavu na sio uzalendo kama unavyodai.
..tumeingia mikataba kipumbavu na kifisadi, na tumevunja mikataba kwa namna hiyohiyo.
..ndege zetu zimekamatwa kwasababu tumeshindwa mahakamani halafu serikali inafanya kiburi kulipa fidia.
Matokeo yake tunaingia hasara ya kulipa riba na aibu ya mali zetu kukamatwa. Sasa huo ni upumbavu sio uzalendo.
..Ndege iliyokamatwa Uholanzi waliosoma mwenendo wa shauri wanadai serikali haikutokea kujitetea ktk shauri hilo. Hayo ni makosa makubwa ya uzembe.
Serikali imekata rufaa na rufaa bado kusikilizwa. Pia mtu ukikata rufaa unaruhusiwa kuomba stay of execution.
Kuhusu hoja kuwa serikali haikutokea mahakamani kama ni kweli basi elewa kuwa mahakanani mmoja anaweza kucheza na wakili wa mpinzani wake ili asitokee mahaka.mani au wakati summons ikiletwa yule anayeipokea anaweza kuhongwa ili aikalie asitoe taarifa kunakohusika ili kesi isikilizwe upande mmoja huku Tanzania zamani mchezo huo umefanyika sana.
Pia elewa kwa sasa nchi iko katika wizi/ ufisadi wa kimfumo ambapo watu wenye mamlaka wizara/idara tofauti wanashirikiana kufanya ufisadi( yaani ufisadi haufanywi na mtu mmoja kana deal lake bali unafanywa kimkakati na kwa ushirikiano). Kesi hii huenda kuna watu ndani ya mamlaka wamesaidia kichinichini ili tushindwe.
Ndege zina faida isiyo ya moja kwa moja ingawa pia faida ya moja kwa ,moja inaweza kupatikana. Mnaopinga mnaimba tu lakini sio kwamba mnapinga economically. Pia uwekezaji unapofanyika haiangaliwi tu faida ya sasa bali potential iliyopo na long term aspects za uchumi. Mfano uwepo wa ndege unasaidia mazaa kama maua, samaki, dagaa na nyama yasombwe kwa haraka na kufika sokoni. Pia watalii wanabebwa kwa haraka sasa ukianalyse kwa kina utaona GDP inayozalishwa kutokana na uwepo wa ndege ni kubwa sana. Miundombinu ya usafirishaji ( ndege, viwanja vya ndegw, reli, bandari, barabara, meli, mabomba ya gesi) ni kichocheo kikubwa cha uchumi ndio maana nchi zote ziliizoendelea ziliwekeza sana katika vitu hivyo. Pia bila kusahau umeme mawasiliano ya simu,
Tatizo nchi hii hivyo vitu vinafanyika kwa kutanguliza ufisadi ambao nimekuambia unafanyiika kimfumo.
Umesikia juzi mkutano wa CCM mafisadi walikuwa na wagombea wao na wamefanikiwa kuwachomeka sasa unategemea nini.
Yule baba wa ufisadi asipokufa mapema watanzania tutaumia sana.
Nb: tupiganie mgombea binafsi Tume huru ya uchaguzi.