Uchaguzi 2020 John John Mnyika kutogombea ubunge mwaka huu 2020

Uchaguzi 2020 John John Mnyika kutogombea ubunge mwaka huu 2020

Mnazungumzia upepo,upepo,mbona form za Urais mlificha mkabakisha moja,na bado hamtaki tume huru ya uchaguzi.
 
Kaogopa kudhalilishwa. Maana angeshindwa vibaya mno. Mnyika hawezi jimbo. Ubungo lilimshinda akakimbilia kimbamba. Sasa Chadema Ruzuku inakwenda kupungua ndo ajiandae kurudi CCM.
Nani kakuambia kaogopa....?
Kwanza mpaka hapo wale waliyokuwa wanatumia nguvu fedha ili kutaka asirudi hapo wameumbuka

Ova
 
Mnyika kweli yupo smart Sana kichwani.
Kachukua maamuzi sahihi Sana baada ya kusoma nyakati na pepo.

Kiukweli upepo wa kijani umetawala Sana kiasi kwamba Kama ukisafiri kwa upepo tofauti inatakiwa usitishe tu safari yako Maana hutafika final destination.
CCM wenyewe watanyukana we Ngoja uone

Ova
 
Kazaliwa kipindi cha CCM. Na primary school lazima aliimba "Naapa naahidi mbele ya chama,mapinduzi nitakulinda mpaka kufa "
goddamn that song!

mbona hatukuimba Uhuru ntakulinda?

Wanzanzibar wamepinduana huko baharini inatuhusu nini Watanganyika????

anyhow, Nyerere aliacha mshahara kuitumikia TANU bure.

Je mshahara/maslahi/maposho/maruzuku/mamikopo ya Katibu Mkuu CHADEMA ni shiiing ngapi ?

Mkoloni hakumpa TANU ruzuku
 
Nimeupenda sana msimamo wa bwana mdogo John Mnyika wa kufuata mfano wa Mwalimu Nyerere.

Mnyika ametangaza rasmi kuachana na ubunge ili apate fursa ya kukitumikia chama vizuri zaidi katika nafasi yake ya Katibu mkuu wa Chadema.

Mungu mbariki John Mnyika.

Maendeleo hayana vyama!
Hah hah kajua hana ubavu wa kutetea hilo jimbo,hana cha kuongea mbele ya wanajimbo lake,hayo mengine anayoyasema ni yale ya sizitaki mbichi hizi.
 
Nimeupenda sana msimamo wa bwana mdogo John Mnyika wa kufuata mfano wa Mwalimu Nyerere.

Mnyika ametangaza rasmi kuachana na ubunge ili apate fursa ya kukitumikia chama vizuri zaidi katika nafasi yake ya Katibu mkuu wa Chadema.

Mungu mbariki John Mnyika.

Maendeleo hayana vyama!
Mnyika na Nyerere wapi na wapi
Mnyika amesoma alama za nyakati,angeshindwa vibaya sana,watu wana hasira nae
 
Yuko sahihi, kwani Polepole na Bashiru huko CCM wanagombea Ubunge majimbo gani?
 
Maana kishausoma mchezo kuwa. Atabwagwa vibaya mno.

Sio kwa kura, bali ni kwa hizi chaguzi za kishenzi na kihayawani, ambapo kuna mtu anaagiza nani atangazwe mshindi.
 
Mnyika na Nyerere wapi na wapi
Mnyika amesoma alama za nyakati,angeshindwa vibaya sana,watu wana hasira nae

Chini ya awamu hii ya tano hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya kipimo halisi cha uhayawani, na ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Chini ya awamu hii ya tano hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya kipimo halisi cha uhayawani, na ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Nina matumaini, safari hii watakikwaa kisiki.

Naomba usinibane kwa kuleta ushahidi, lakini ni hisia nzito ambayo sijawahi kuwa nayo wakati wowote hadi sasa.

Safari hii watu watakataa kufanya kazi ya kupiga kura halafu atokee mpumbavu mmjoaja avuruge kazi yao hiyo.

Uzuri ni kwamba haitahitaji vurugu, watakaoanza vurugu (wezi wa kura) watadhibitiwa huko huko kituoni kwao kwa usalama wao.

Iliyobaki ni kwa CHADEMA kutoa somo tu lieleweke vizuri na watu watatimiza lengo.
 
Mnyika na Nyerere wapi na wapi
Mnyika amesoma alama za nyakati,angeshindwa vibaya sana,watu wana hasira nae
Ukiwa na akili fupi utadhani wewe ni mjanja.

Subiri atengeneze kiboko atakachowatandikia, hapo ndipo mtakapotambua anachofanya sasa.

Kazi ya kujenga chama ni ya muda mrefu, 2025 ukiwa bado upo utayapata matokeo ya kazi yake.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Back
Top Bottom