Uchaguzi 2020 John Mnyika: CHADEMA haijakaa na Tume ya Uchaguzi(NEC) na haina mpango wa kuteua wabunge Viti Maalum

Uchaguzi 2020 John Mnyika: CHADEMA haijakaa na Tume ya Uchaguzi(NEC) na haina mpango wa kuteua wabunge Viti Maalum

Imefahamika kuwa hadi sasa hakuna kikao chochote kilichoketi kati ya Kamati Kuu ya Chadema na Tume ya uchaguzi, na hadi sasa hakuna majina yeyote ya viti maalumu yaliyopelekwa NEC.

Leo serikali ya CCM na NEC wanahaha kufoji saini ya Katibu Mkuu Chadema ili tu wawe na angalau wabunge wa upinzani bungeni, kama walijua hilo kwanini walikuwa wanawaengua.

CCM na serikali yake hawakujua kabla madhara ya kubaki peke yao bungeni kuwa hata wafadhili wa bajeti yetu WB, IMF, EU huangalia kwanza maoni ya kambi ya upinzani ndipo wachangie kiasi gani.

Jambo la msingi ni kuwa Chadema imeshalitambua hilo inasimamia msimamo wake wa kutoyatambua matokeo, na wote watakaoingia bungeni kwa tiketi ya Chadema iwe kwa kufoji au kuhongwa watambue watafutwa uanachama na watakuwa wabunge wa mahakama, na hilo halitakuwa tukio la kwanza kufanywa na Chadema.
WB, IMF ni wafanya biashara. Hawawezi sikiliza propaganda zetu hapa
 
Very stupid of yuh!
Kama mtateua ni kwa faida yenu, na kama hamtoteua ni kwa hasara yenu wenyewe full stop!
 
Yaani orodha igushiwe, halafu viongozi waseme hawajaiandaa itakuwa na uhalali gani?. Kama viongozi hawajaiandaa it means hakuna haja yakupeleka viti maalumu inatakiwa CDM ife ili tupate maendeleo, maana wao ndio wakwamisha maendelo kulingana na Wana ccm wanavyodai. Kwahio kama viongozi wakikataa hawajapeleka majina NEC, hapatakuwa nahaja yakupeleka viti maalum wa CDM . Wapeni hivyo viti URA,TADEA,CUF,NCCR ,UPDP,UDP,TLP.
Jamani mbonasijasikia.chauma.
 
Very stupid of yuh!
Kama mtateua ni kwa faida yenu, na kama hamtoteua ni kwa hasara yenu wenyewe full stop!
Faida inayotazamwa ni ya Tanzania siyo kununuliwa kupitia ruzuku.

"Upinzani ruzuku" ndiyo CCM inaoutaka na si "Upinzani wa kushika dola".

Chama chochote kuliko kubaki kuwa "chama ruzuku" ni bora hicho chama kife!, maana kitakuwa hakina faida kwa Wananchi
 
Ungejua nilichafua kidole changu kwa ule wino wenu, usingesema hivyo.
Kwani zile kura walizihifadhi police au kwenye kituo cha wapiga kura?

Halafu uchaguzi mwingine usikubali kushikiwa akili hapa JF na tweeter, uaendage field ukawe wakala ili kushuhudia mnavyoshindwa😁😁😁
Pole, hukuchafua kidole ila ulitimiza wajibu wako kikatiba ila kura hazikutosha kumpa ushindi uliyemchagua
Hawa wanaowadanganya na kuwaaminisha kwamba waliibiwa kura hawakua na nia ya dhati ya kufanya vitu sahihi ili kushinda uchaguzi. Waligeuka kufanya ujanja ujanja ambao unawagharimu sasa.
 
Je Chadema inaitambua ruzuku iliyotokana na uchaguzi inayoukataa?
Nikuulize uhai wa mtu ni sawa na ruzuku ya sh. ngapi.

Kuna wanachama wengi wameuawa na polisi wakipigania wabunge wao waingie bungeni kuna wengine wamepoteza viungo wengine wako mahospitalini wengine gerezani, hao wote unawalinganisha na ruzuku?
 
Hata Mimi mwanzo nilifikiria kuwa huyu Mdada aliyeshinda asiende bungeni lakini nimetafakari naona aende tu,akakae zake Kimya akusanye tu hela zake Basi maisha yaendeleee,Ila hawa wa viti maalum hapo ndio mtego nadhani endapo watawateua watakuwa wameingia kwenye mtego
 
Very stupid of yuh!
Kama mtateua ni kwa faida yenu, na kama hamtoteua ni kwa hasara yenu wenyewe full stop!
Utopolo uliofanyika kwenye uchaguzi huu haukubaliki. Uchaguzi ufutwe, iundwe tume huru ya uchaguzi, kisha uchaguzi huru na wa haki ufanyike.
Vinginevyo, bunge liwe la kijani mtindo mmoja
 
Viti maalum mtavipataje wakati hamjapata 5% ya wabunge wa TZ au mimi sielewi wabunge wa viti maalum wanapatikanaje!!

Huna lolote ujualo zaidi ya kupiga Siasa mfu hapa jukwaani. Viti maalum vinatokana na kura za urais. Hata hivyo siwashauri cdm kupeleka viti maalum kutokana na uchaguzi uliokuwa wa kishenzi, kihayani, ukatili wa wazi na umwagaji damu.
 
Pole, hukuchafua kidole ila ulitimiza wajibu wako kikatiba ila kura hazikutosha kumpa ushindi uliyemchagua
Hawa wanaowadanganya na kuwaaminisha kwamba waliibiwa kura hawakua na nia ya dhati ya kufanya vitu sahihi ili kushinda uchaguzi. Waligeuka kufanya ujanja ujanja ambao unawagharimu sasa.

Hivi unadhani ule upuuzi uliokuwa unafanyika kwenye uchaguzi huu ilikuwa ni siri kufahamika? Achia mbali ule uhayawani wa wagombea wa ccm kupita bila kupingwa kwa mizengwe ya wazi.
 
Hata Mimi mwanzo nilifikiria kuwa huyu Mdada aliyeshinda asiende bungeni lakini nimetafakari naona aende tu,akakae zake Kimya akusanye tu hela zake Basi maisha yaendeleee,Ila hawa wa viti maalum hapo ndio mtego nadhani endapo watawateua watakuwa wameingia kwenye mtego
Hata huyo wa Nkasi lazima ajue ni chama kilichombeba, na msimamo wa chama ni kutoyatambua matokeo yote, kama hakithamini chama na wanachama waliokufa kwa ajili yake anathamini pesa kwanini asiunge juhudi aungane na watesi hatokuwa wa kwanza.
 
Sijui kama hamjui au mnafanya kusudi.
Viti maalum vinatokana na % ya kura zote za ubunge ambazo chama kimepata.
Mfano jumla ya kura za ubunge nchi nzima zilikuwa milioni 10, wataangalia chadema walipata kura ngapi katika hizo mil 10. Na hivyo itatafutwa % ya kura za chadema kama zimefika atleast 5%.
Hii inafanyika chaguzi zote, tuwe tunafatilia

Kura za ubunge au urais?
 
Imefahamika kuwa hadi sasa hakuna kikao chochote kilichoketi kati ya Kamati Kuu ya Chadema na Tume ya uchaguzi, na hadi sasa hakuna majina yeyote ya viti maalumu yaliyopelekwa NEC.

Leo serikali ya CCM na NEC wanahaha kufoji saini ya Katibu Mkuu Chadema ili tu wawe na angalau wabunge wa upinzani bungeni, kama walijua hilo kwanini walikuwa wanawaengua.

CCM na serikali yake hawakujua kabla madhara ya kubaki peke yao bungeni kuwa hata wafadhili wa bajeti yetu WB, IMF, EU huangalia kwanza maoni ya kambi ya upinzani ndipo wachangie kiasi gani.

Jambo la msingi ni kuwa Chadema imeshalitambua hilo inasimamia msimamo wake wa kutoyatambua matokeo, na wote watakaoingia bungeni kwa tiketi ya Chadema iwe kwa kufoji au kuhongwa watambue watafutwa uanachama na watakuwa wabunge wa mahakama, na hilo halitakuwa tukio la kwanza kufanywa na Chadema.
We nani kwanza unayesema hayo
,hebu jitambulishe tukujue
 
Chadema ilikufa baada ya Dr slaa kuondoka Hawa wengine wanafanya siasa za majitaka na matukio kwa style hii watabaki kuwa chama Cha upinzani muda wote Ikulu wasahau

Unaongea utoto gani dogo? Wakati wa Dr. Slaa cdm ikiwa hai mbona haikuchukua hiyo nchi?
 
Jipangeni na 2025, sasa hivi muwe wapole tu kwa mamlaka sababu hakuna chochote mtachofanya kikafanikiwa.
 
Back
Top Bottom