Uchaguzi 2020 John Mnyika: Kuongea na vyombo vya Habari, saa 8 mchana

Uchaguzi 2020 John Mnyika: Kuongea na vyombo vya Habari, saa 8 mchana

John Mnyika: Jitihada za mawasiliano na NEC juzi, jana na leo mpaka muda huu kudhibiti hujuma kwenye uapishaji wa mawakala zimekwama maeneo mengi. Nitazungumza vyombo vya habari HQ saa 8 mchana. Kwa sasa , #PeoplesPower itumike maeneo ambayo hujuma zinaendelea. #SasaBasi.

=====

MNYIKA: MAWAKALA WETU HAWAPEWI CHOCHOTE KUTHIBITISHA WAMEAPISHWA

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema wanaona kitendo cha asilimia kubwa ya Mawakala wao kutopewa uthibitisho kuwa wameapishwa kama tatizo litakaloleta tatizo kubwa zaidi siku ya kupiga kura

Amesema wanaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuelekeza Wasimamizi wa Uchaguzi kutoa nakala za barua kwa Mawakala, na wao kama Chama wapewe ili Wakala anapoenda Kituoni ajue tayari ameshatambulishwa na ana ushahidi wa hilo

Amesema, "Tume kwa nia njema kabisa isipoyafanya haya ya kurekebisha hili jambo la mawakala, tunawaomba wananchi waendelee kujiandaa kupiga kura tarehe 28 kumchagua Tundu Lissu kwa wingi, kwakuwa tutaungana pamoja kuhakikisha kwa namna yeyote ile Mawakala wetu wanaingia ndani ya Vituo"

Ameongeza, "Ikibidi kutumia falsafa yetu ya People's Power tutatumia, lakini tumeshasema Uchaguzi huu sasa basi. Hujuma tulizofanyiwa huko nyuma imetosha"
Viongozi wanaojiita wadini hii ndio amani mnayo hubiri sintowaheshimu daima madhalimu nyie anaeashiria kuvuruga amani hammambii chochote mnanjaa sana hivyo mnavyokula mtakula hadi kaburini siro viashiria vyakunja amani ndio hivyo shughulika sasa au niwaelewa tofauti kwenu haki ndio uvunjifu wa amani?
 
Back
Top Bottom