John Mnyika: Mambo CHADEMA tuliyozungumza na wenzetu wa CCM

Tumependekeza iundwe Tume ya Ukweli na Upatanishi itakayoshughulikia madhara ya watu walioumizwa ndani ta miaka iliyopita 6, pia tulipendekeza madhara yaliyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 yashughulikiwe na kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa huru na haki[emoji1534]
 
chadema sasa ndiyo mwisho wao jpm alikuwa anatumia nguvi kuwatoa kwenye reli mama anatumia ulimi kuwatoa kwenye reli na tayari wameshaanza kuchochora pembeni kwisha habari ya chadema
 
Kwa miaka sita ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, imepandikiza migogoro kwenye vyama takribani vitano, natoa wito kwa mamlaka husika kuchunguza mwenendo wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na kumchukulia hatua msajili wa vyama vya siasa[emoji1534][emoji1545]
 
Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba Katika mazungumzo yote, tutatanguliza maslahi ya Taifa na si kitu kingine. BRAVO.[emoji1534][emoji1534][emoji1534][emoji1533]
 
hayo hayatekelezeki muangalie mambo mengine huwezi anza uchunguzi wa vitu kama hivyo ccm ikiwemo madarakani never
 
2012 Wassira alisema Chadema itakufa ndani ya mwaka mmoja, Magufuli akasema 2020 ataifuta Chadema wewe unasema mama ataifuta. Kesheni mkiomba hilo.
Na yule Mwandishi nguli kabaki anaweweseka tu ili kujiliwaza kajibanza kwa covi19.
 
Ukizisoma hizo hoja za maridhiano za chadema its as if baba anamwagiza mwana kwamba ninataka hivi fanya hivi. Hapa baba ni chadema na mwana sijui ndie atakuwa Rais Samia?

Nirudie tena kusema kwamba chadema kinaonekana hakina uwezo kabisa wa kujitathmini , kujirekebisha na kugeuka. Wapo stuck kwenye mazingira ya kisiasa ya 2005-2015 wanafikiri na sisi wananchi tumeziacha akili zetu kule. Hivi kwa akili za hata mbayuwayu unawezaje kusimama na kurusha lawama kwa msajiliwa vyama kuhusu migogoro yenu? Aaaargh!
 
chadema sasa ndiyo mwisho wao jpm alikuwa anatumia nguvi kuwatoa kwenye reli mama anatumia ulimi kuwatoa kwenye reli na tayari wameshaanza kuchochora pembeni kwisha habari ya chadema
Kaungane na Wassira kutabiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…