Joseph Mrindoko wa wachokonozi azichana vibaya shule za English Medium

Joseph Mrindoko wa wachokonozi azichana vibaya shule za English Medium

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Amezichana vibaya shule za English Mediums na kuwaita " mbumbumbu "Watanzania wanao jistress kusomesha watoto wao kwenye shule hizo.

Ameongea point nyingi sana nenda kamsikilize mwenyewe You Tube.

Moja kati ya nukuu yake anasema " Waafrika tunataka kuwa kama wazungu. Wazungu hawataki kuwa kama sisi.

Tumekuwa mbumbumbu kiasi cha kulipa pesa ili watoto wetu watengenezwe wawe kama wazungu.

Cha ajabu hao tunao taka wawatengeneze watoto wetu wawe kama wazungu sio wazungu wala hawajui chochote kuhusu wazungu na uzungu
 
Kumbuka Kenya na Uganda wametupita kielimu jwa sababu ya lugha ya malkia. Angalau na sisi tujikomboe, hii lugha ni ya kimataifa huwezi kuikwepa. Wewe anzisha viwanda vingi vyenye tija, andika kila kitu kwa kiswahili, ili ueneze kiswahili duniani. Hata terminology za kisayansi uandike kwa kiswahili. Utaweza? Whether you like or not you ought to lean English. Naomba tu waalimu wa hizi shule wapikwe vizuri.
 
English medium zinasaidia sana kwa usalama wa mtoto wako hata kama unakipato duni somesha hizi English medium mtoto wako atakuja na changamoto kwa rafiki zake waliofanikiwa hapo baadae hizo st kayumba watoto wanaomaliza huwa wanaishia kuja kushinda vilabuni na kuwa wavuta bangi
 
Ni wazazi limbukeni tu ndio wanaopeleka watoto wao huko wakiamini watapata elimu bora.

Cha ajabu watoto wanafundishwa kiingereza kibaya na walimu wa kuokoteza wao wenyewe hawajui lugha hiyo kwa ufasaha wanakaririsha watoto kiingereza kibovu.
 
Wazazi wengi wenyewe hata kiingereza cha kuombea maji hawakijui.

Wakisikia english medium wanajua kuna elimu bora kuliko kwingine.

Mwisho wa kozi mtoto anahitimu hajui kuongea kiingereza vema inabidi akimbizwe tena mitaani kupatiwa english course ya pre form one, huko nako anaenda kubabaishwa na vijana wa form six failure wasiojua vema kuongea kiingereza.

Mzazi anaishia kutapatapa asijue wapi kuna elimu bora kwa mtoto wake wakati naye ni dunya tu shule alikwenda lakini akaishia kusikojulikana kama alisoma au hakwenda hata darasa moja
 
Kumbuka Kenya na Uganda wametupita kielimu jwa sababu ya lugha ya malkia.
Acha uongo ndugu, hao unaowafagilia hawana lolote la kutuzidi, Mseveni mwenyewe alikuwa mkimbizi hapa bongo unalijua hilo?

Ruto mwenyewe huwa anaazima Zabron singers wakamburudishe ikulu, unalijua hilo?

Wabongo tupo vizuri sana kuliko Wakenya na Waganda
 
Amezichana vibaya shule za English Mediums na kuwaita " mbumbumbu" watanzania wanao jistress kusomesha watoto wao kwenye shule hizo.

Ameongea point nyingi sana nenda kamsikilize mwenyewe You Tube.

Moja kati ya nukuu yake anasema " Waafrika tunataka kuwa kama wazungu. Wazungu hawataki kuwa kama sisi. Tumekuwa mbumbumbu kiasi cha kulipa pesa ili watoto wetu watengemezwe wawe kama wazungu. Cha ajabu hao tunao taka wawatengeneze watoto wetu wawe kama wazungu sio wazungu wala hawajui chochote kuhusu wazungu na uzungu
Unataka wafunze kiarabu?

USSR
 
Wewe na Museveni nani anamaisha muda huu

USSR
Acha uongo ndugu, hao unaowafagilia hawana lolote la kutuzidi, Mseveni mwenyewe alikuwa mkimbizi hapa bongo unalijua hilo?

Ruto mwenyewe huwa anaazima Zabron singers wakamburudishe ikulu, unalijua hilo?

Wabongo tupo vizuri sana kuliko Wakenya na Waganda
na Museveni ba
 
Back
Top Bottom