Joseph Musukuma: Kikokotoo kinawaumiza wananchi, tunatengeneza taifa la wezi

Hizi ndio shida za kuwapa dhamana watu wasiojua wanaowaongoza. Eti unasave laki 5 Hadi 7 kwa mwezi. Unajua mshahara wa daktari, nesi, mfamasia, walimu?

Nyumba ya laki 6 wakati wengine hawapati hata take home ya laki 6.
 
Inaonekana wewe ni mnufaika wa kikokotoo. Haiwezekani pesa ya mtu ikuume kupewa yote.

Yaani una roho mbaya zaidi ya mchawi.
 
Vya bure kivipi wakati ni hela yake?
 
Katibu Mkuu wa CCM Dr. Nchimbi kalisemea vizuri sana hili la kikokotoo, kuwa ni kilio kikubwa cha watumishi wote, hivyo atalibeba na kulipeleka kwa Mh. Rais wetu Mama Samia, na Mama yetu alivyomsikivu na uhakika atarudisha kama zamani kikokotoo cha PSPF..!!
 
Mbunge anavuta 250M unaona kawaida?

Mke wa Rais mstaafu analipwa unaona kawaida? Rais mstaafu analipwa 70% na kujengewa nyumba.

Halafu unaongea upuuzi hapa. Halafu hizo hela ni za wafanyakazi, kinachofanyika hapo ni kubadili jina tu.

Ni sawa simu ya 700,000 ukaambiwa inauzwa laki 800,000 na vocha ya 100,000 BURE

Hizo ni kanuni tu za kuonekana serikali unafanya kitu kumbe hamna kitu kipya.
 
HAKUNA WATU WANAFIKI KM CCM NA WABUNGE WAKE, MAANA HAWA HAWA NDO WALIPITISHA KIKOKOTOO KWA BWEMBWE NA KEJELI WAMEONA UCJAGUZI UMEKARIBIA WANAANZS SARAKASI
 

Hujui maana ya haki za watumishi, sio Tz tu hata duniani kote hujui maana ya haki zao, ni sheria hiyo dunia nzima, sbb wewe huna ajira ndio unataka watu wasilipwe mchango wa mwajiri? Kisa huna ajira unataka watumishi wasichangiwe na mwajiri? Akili huna hata nukta, unajua maana ya uwizi? Sheria za haki za watumishi unazijua? Nosense
 
Tapeli mwengine.

Inaonekana upo mbali na biashara ndio maana unaanza kupiga hesabu za kwenye makaratasi.
 
Kifupi wafanyakazi wa serikali mumewaasha wananchi kupinga hiki kikokotoo kipya cha nyie hiki cha kulipwa ikiwemo asilimia 15 mnachangiwe na serikali you will be loosers timu za nawakili zimeshaanza kujipanga kuiburuza serikali mahakamani kwa niaba ya wananchi kupinga serikali kulipa wastaafu kwa kikokotoo kipya kama malipo yatahusisha na asilimia 15 ya serikali imechangia itakuwemo kwenye kikokotoo

Kuwa asiwepo wa kulipwa ikihusika hiyo asilimia hadi kesi ya msingi iamuliwe

Nyie wafanyakazi wa serikali ndio mliolianzisha mjiandae kulinywa kama lilivyo

Wajinga nyie serikali inawapendelea bado mnajitia ujuaji .Mtaliipwa asilimia 5 tu za mafao yenu ya mlichochangia kinachobaki subirini maamuzi ya mahakama
 
Hizi ndio shida za kuwapa dhamana watu wasiojua wanaowaongoza


Eti unasave laki 5 Hadi 7 kwa mwezi

Unajua mshahara wa daktari, nesi, mfamasia, walimu?


Nyumba ya laki 6 wakati wengine hawapati hata take home ya laki 6
Main post ya mada imeelezea msukuma kasema nini ndio kinachojibiwa. Sasa wewe unakurupuka tu, unasoma posts za watu with bias reading ukiona statement zisizokufurahisha unatoa povu.

Savings zinazoongelewa ni kwa watu wanaokaa rent free nyumba za serikali. Wewe unaniletea mambo ambayo mimi sijasema kabisa.
 
Hiyo hela inabidi izungushwe, binafsi sioni shida kwenye hiyo 33%.

Ningewaelewa watumishi wangekuwa wanalalamikia ‘replacement rate’ ya 1/580 ni ndogo mno. Hiyo rate airudishi hata 20% ya mchango wa mwezi malipo ya wastaafu ni kama 10.3% (kabla ya withdrawal) kwa mwezi kwa mtu aliefanya kazi miaka 30, inaendeshwa hovyo sana hiyo mifuko.

Replacement rate inatakiwa kuwa walau between 1 of 100 to 200 kwenye calculations, tena for life. Hiyo mifuko itakuwa na hali mbaya sana.
 
Kama ni hivyo kwa nini kuna double standard.? Mawazir na wabunge watumie Kikokotoo hicho hicho kama ni kizuri
Mawaziri wengi wakistaafu au hao wabunge wanakuwa masikini sana, sababu ni poor financial planning. Amini nakuambia elimu ya uwekezaji na fedha ya wachaga na wakinga ni muhimu sana kila mtanzania aipate. Bila elimu hata kama serikali itatoa hela yote ya kustaafu hakuna unafuu utakaopatikana kwa mtumishi zaidi ya kusababisha msongo zaidi wa mawazo na kuwafanya wafe mapema. Nasisitiza serikali isikurupuke kabisa iendeshe elimu ya fedha na financial planning in masses.
 
Serikali sijui kwanini haisikilizi wananchi ,kama hadi wabunge wa CCM wanaona kikokotoo kibaya kwanini bado tu wanaendelea kukitumia? Kodi 30% mmelamba na bado mnaichukua 20% yake huu si WIZI?
 
KUTOKA 22:18

Mithali 26:4-5
 
Hiyo hela inabidi izungushwe, binafsi sioni shida kwenye hiyo 33%.
Basi na hao wapitisha sheria(wabunge) na wao kwenye mafao yao kama yale ya kiinua mgongo baada ya miaka mitano ya ubunge wachukue 30% inayobaki izungushwe, hapa ndipo unaona hakuna usawa, mtu kamaliza muda wake mpe 100% zake akajambe mbele
Hapa nakubaliana na wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…