Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Naona umechanganya mambo au umekosa utulivu wakati wa kuandika:Hakuanza leo.
1. Kama nakumbuka sawa sawa Lissu aliwahi kusema kuwa Mbowe hakumshikia drip baada ya kupigwa risasi bali ni Msigwa. Inawezekana ni kweli lakini aliisema kama vile Mbowe alikuwa anajipendekeza. Nikadhani ni kuteleza tu na ni hulka ya msema kweli.
2. Akaanza kuzungumzia mapungufu ya chama chake jukwaani. Alipoulizwa, akasema akasemee wapi? Insinuation ni kuwa Boss wake anayakumbatia.
3. Zikaanza tuhuma za yeye na Msigwa kutaka kufanya mapinduzi, akakaa kimya. Msibwa akawa anamtukana Mbowe, yeye kimya. Msigwa kahamia CCM, yeye kimya. Msigwa akawa anashambulia CDM na Mwenyekiti wake, yeye kimya.
4. Chadema wakatangaza kikao cha Kamati Kuu. Yeye wala hakujisumbua kuhudhuria badala yake publically akahudhuria mazishi ya mpiganaji mmoja wa CDM. Hii ni dhahiri ilikuwa kuonyesha kuwa Mbowe hajali wanachama wake.
5. Akaibua hili la kuhongwa na Abdul. Hadithi ambayo haina kichwa wala miguu.
6. Akazungumzia watu kung'ang'ania madaraka. Wote tulijua anamsema Mbowe
Kinachonisikitisha ni kuwa haikupaswa kuwa hivi. Angeweza kugombea bila kumpaka matope Boss wake. Nadhani washauri wake walimwambia kuwa ukitaka kuhakikisha kuwa nyoka amekufa inabidi umkate kichwa. Hivyo shutuma, maneno ya ovyo n.k. vingemtisha Mbowe kutangaza nia. Big miscalculation. Badala yake anaonekana kama opportunist asiyekuwa na chembe cha loyalty.
Na sasa, kama atashindwa, nafasi ya kugombea urais itakuwa hati hati. Labda ahamie ACT-WAZALENDO. Akifanya hivyo atawasaidia kupata wabunge wengi pengine hata zaidi ya CDM. Lakini yeye heshima yake itakuwa zero.
Amandla...
Eti labda ahamie ACT, akihamia ACT atasababisha kupatikana wabunge wengi ACT kushinda CHADEMA, ila yeye atakosa heshima!! Aliyesababisha kupatikana wabunge wengi, atakosaje heshima? Atakosa heshima kwa nani? Aliosababisha wapate wabunge wengi kwa aliowasababishia wapate wabunge wachache?