Pre GE2025 Joseph Oleshangay: Kuna watu wanataka Kuvunja Chama ili kumtengenezea Samia Njia Nyeupe Ya Ikulu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Naona umechanganya mambo au umekosa utulivu wakati wa kuandika:

Eti labda ahamie ACT, akihamia ACT atasababisha kupatikana wabunge wengi ACT kushinda CHADEMA, ila yeye atakosa heshima!! Aliyesababisha kupatikana wabunge wengi, atakosaje heshima? Atakosa heshima kwa nani? Aliosababisha wapate wabunge wengi kwa aliowasababishia wapate wabunge wachache?
 
Nimepoteza sana matumaini na Chadema, labda kama Lissu atashinda kitu ambacho sikioni maana Mbowe tayari atasaidiwa sana na Ccm kushinda kwa mbinu zao.

Kilichobaki tu nikuiomba Ccm ituletee mgombea yeyote wa kiume hata kama atakuwa January lakini si huyu mama.

Sikutegemea kabisa Mbowe aliyekipambania chama na watu wengi wamepoteza maisha wakikipambania chama kumbe mwenyekiti ni wa upande wa pili dah hii ni hatari sana. Bila Mungu kutupambania Ccm italitesa sana taifa hili.
Lissu pamoja na madhaifu yake lakini ni mpinzani wa kweli sana na hapendi kabisa rushwa ila haoni taabu kupambania kilicho haki yake.

Pamoja na maovu yote yaliyofanyika serikali za mitaa Mbowe haoni kama kuna shida. Natamani wanaopiga kura kumchagua mwenyekiti wakiweza wale pesa za Mbowe maana najua atatoa fungu kubwa sana kwa wajumbe wa mkutano mkuu ili ashinde na hizo pesa zitatoka kwa mama Abdul ila mwisho wa siku nilitamani wampigie kura Lissu.
 
Hahaaa bana ety kutunishiana tumbo dah OK msuli na give apparatus
 
Mbona uwezekano mkubwa mgonjwa na wewe!! Mleta mada ameweka analysis nzuri.
Analysis gani..maelezo yote tena kamilifu yametolewa, katiba ya chadema inamruhusu Mbowe kugombea na walipokubaliana kutoweka ukomo kulikuwa na sababu..vyama vya siasa na mbaya zaidi hapa Tanzania vinaoperata kwenye mazingira yanayohitaji mtu aina ya Mbowe..chama kikipata mtu wa aina hii hakiwezi kukubali hoja za kijinga ili kife! Mmeshindwa kupigia kelele katiba uwepo ukomo wa ubunge ambao wanaishi kwa kodi zenu mmepepesukia jambo dogo la chadema ambao wanajitoa kupigana kwa ajili yenu..mwenyekiti apate timu nzuri ya kumsaidia ili chama kiendelee kupigania maslahi ya nchi..na imeelezwa bayana mambo yote haamui mwenyekiti peke yake..yeye ni kamisaa tu mambo yote yanaamuliwa pamoja!
 
Mbona huyu lussi alipewa nafasi na Mbowe 2020 ashindane na jiwe, , kwani kuna shida gani kuwa na mwenyekiti na mgombea raisi ni mwingine kama huyu lussi alivyopewa?
Huyu mnyaturu hajielewi, anadhani akiwa mwenyekiti ndio atashinda uchaguzi, ni kama anasahau ilikuwaje yeye na jiwe 2020
Kiukweli tunajua na hata hawa chawa wa lissu mitandaoi wanajua kabisa 2025 hawataweza kumshinda mama
Lakini wanakaza fuvu
 
Kuna neno "pengine". Nitajie mtu mmoja aliyehama Chadema akabakia na heshima aliyokuwa nayo akiwa Chadema? Lissu akihamia ACT-Wazalendo atashutumiwa kuwa kuwa yeye ni mganga njaa. Hata kama sio kweli wako watakao amini. Na wako pia watakaoamini kuwa "amepewa" wabunge hao ili kupunguza nguvu ya CDM na kuifanya ACT-Wazalendo kuwa kambi rasmi ya upinzani.

Amandla...
 
Mbona kama unabwabwaja tu inshu apa chadema ilikataa uchaguzi halafu chini ya uwongozi wa mbowe wameenda kuchukuwa ruzuku bado kiongozi huyu anafaa kuongoza mapambano
 
Mbowe ni mwenyekiti wa maisha wa Chadema
 
Mbowe ni mwenyekiti wa maisha wa Chadema
..elewa na sababu za hali hiyo, hivi alipopatikana Mashinji kuwa katibu mkuu kuna mtu alitarajia huyu mtu ataishia kuwa DC wa ccm sawa na kina mchopanga? akili zenu haziko sawa, lkn mifano ipo..kwani Mbowe si binadamu? Kwa nini bado yupo chadema katikati ya misuko suko isiyoisha? Lisu hawezi kuwa km Mashinji? au Katambi, au Waitara..au Msigwa ana tofauti gani Lisu na hao..
 
Mbowe ni mwenyekiti wa maisha wa Chadema
Sio lazima. Anaweza hata kushindwa katika uchaguzi ujao. Kitu muhimu ni apewe heshima anayostahili na watu waheshimu haki yake ya kugombea.

Amandla...
 
Yaani unyimwe haki zako ambazo zipo kwa mujibu wa katiba..halafu ukipewa tena uanze kufurahia?
 
Tunamuomba FM atumie busura hajiondoe kwenye uchaguz kwa nia njema amuachie TL ili kukiokoa chama
 
Samia hagombei 2025.
Samia hatagombea ila anaitengenezea njia nyepesi ccm kushinda urais 2025 kwa kumpetimpeti mbowe na maridhiano-bandia.

Ila 2025 baada chuma kingine kutoka ccm kuingia ikulu , chadema itakuwa imeshajifia tayari wala hakuna atakaye hangaika na mbowe.
 
Tanzania hakuna upinzani me ndio mana siwaamin wanasiasa kabisa watajua na mambo yao
 
Kwamba Mbowe kwenda kudanganywa na Samia kwako ndiyo jambo la maana? Je na alipodanganywa hayo mambo ya utekaji yalikoma? Zaidi sana tumejua kuwa kumbe hata enzi hizi za Samia wale team Mbowe hawatapata madhila maana kamanda wao analamba miguu. Hakuna chama cha upinzani wa kweli cha aina hiyo.

Jana Mbowe alionyesha dhahiri kuwa ana jambo lake Chadema yeye pamoja na hao wafuasi wake ambalo ni tofauti kabisa na sisi tunavyoamini. Mbona Slaa tulikuwa tukimuunga mkono? Jinsi ambavyo tulifanya kwa Slaa basi vivyo hivyo tungefanya kwa kiongozi aina ya Lissu. Mbowe ameshajionyesha kwa kila mtu kuwa ni nani. Hafichiki tena wala hasafishiki. Ungekaa tu chini ukafikiri tunahitaji nini kwa kipindi hiki basi ungeona kabisa Mbowe siyo mtu sahihi kutupeleka. Kama huwezi kujua zaidi ya kutaka Mbowe aendelee kujilipa fadhila basi pole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…