Joseph Selasini: Mwaka 2020 Mbatia alitupeleka na Anthony Komu kwa Dkt. Bashiru Ally kufanya makubaliano na CCM

Joseph Selasini: Mwaka 2020 Mbatia alitupeleka na Anthony Komu kwa Dkt. Bashiru Ally kufanya makubaliano na CCM

Hiihii CHADEMA inayotumiwa na Samia atakavyo, au kuna nyingine?

Ndio hiyo CHADEMA ambayo Samiah alidai Mwenyekiti wake ni gaidi lakini leo kamwita ikulu. Kutoka ugaidi mpaka mazungumzo.
 
Kama mlikubali kwenda kikaoni basi inatosha kudhihirisha kuwa unanunulika na mlishindwana kiwango maana msingekubali kwenda kabla ya Mbatia kuwaelewesha mnaenda kufanya nini.

Ni bora hata ungeendelea kubaki kimya kama ulivyobaki huo muda wote.
 
Joseph selasini nadhani aliyoeleza yanakaribiana na ukweli kwani katika utawala wa mwendazake James mbatia alikuwa akifanya ziara mikoani kuimarisha chama chake huku akipokelewa na wakuu wa mikoa,. Mfano mzuri alipofanya ziara mkoa wa mbeya alipokelewa na mkuu wa mkoa wa wakati huo CHALAMILA
 
Mbatia ni mchumia tumbo tu. Hana uafisa wowote. Uchaguzi wa mwaka 2020 walipoitwa na Magufuli, waliahidiwa vyeo na fedha za kusaidia kampeni zao na wao wapewe baadhi ya nafasi za ubunge na kuwa chama cha upinzani kitiifu kwa mwendazake. Hali ilikuja kubadilika baada ya Chadema kumsimamisha Lissu na kuvutia umati mkubwa wa watu. Magufuli alipoona hali ni mbaya kwake akaamua kutumia dola kupora uchaguzi na akawatupilia mbali hawa wachumia tumbo kwani aliona hawana uwezo wa kupambana na Chadema.

Huu ndio ukweli wenyewe,Mzee wa Chato hakutegemea wala kujiandaa na ujio wa Lissu.
 
Yap, kula tano mkuu, hapa umesema ukweli wa wazi, na tulisema kabisa kuwa Magufuli alivunja makubaliano yake na kina Mbatia na Lipumba, baada ya kuona kura za CDM zingemuumiza hata yeye. Akaona isiwe tabu bora apore uchaguzi kabisa, maana hata kuiba bado ingekuwa ngumu kwani akina Mbatia hawakuwa na mvuto wowote. Akaagiza usalama wa taifa waende na karatasi za matokeo fake na hayo ndiyo yatangazwe.

Ilifika mpaka mahali Mbatia anapangiwa sehemu za kwenda kufanya kampeni, na ujumbe gani awe anatoa. Baada ya Mbatia kuacha hewani ndio imebidi awaunge mkono cdm kwani huko ccm hana support yoyote.

Pamoja na kuandika yote haya lakini ukweli ni kwamba ilikuwa ni ndoto Lissu kumshinda Magufuli kabisa hili jambo ni lazima sote tukubaliane japo ni gumu sana
 
Hapo ndio ugomvi unapoanzia, Mbatia akapewa shs. 500 miliion kuisaidia ccm kwenye uchaguzi 2020; Selasini na Komu hawakuambulia kitu!!! Lakini kwenye sakata hili Komu yuko na Mbatia!! Hawa wachaga wanachezea saccos yao!!!
Wazaramo hamkeni, wachaga wanajua kula na maccm
 
Pamoja na kuandika yote haya lakini ukweli ni kwamba ilikuwa ni ndoto Lissu kumshinda Magufuli kabisa hili jambo ni lazima sote tukubaliane japo ni gumu sana
Kumshinda kihalali sio tatizo, tulitaka tuone atamshinda kwa kura kiasi gani. Kwa taarifa yako Magufuli hukufikisha kura 5m, wala wapiga kura hawakufika 10m. Kilichomfanya anajisi uchaguzi ni kwasababu aliogopa ukweli kukaa hadharani.

Na kwa kukusaidia vizuri, wabunge wa CCM hawakufika 55%, jambo ambalo kikatiba lingewanyima CCM kufanya maamuzi yoyote watakayo bungeni. Hivyo kwakuwa Magufuli alikuwa na mpango wa kuchezea katiba ili akae madarakani zaidi ya miaka 10, akawa hana jinsi zaidi ya kuagiza yatolewe matokeo ayatakayo. Hutaki jinyonge.
 
Pamoja na kuandika yote haya lakini ukweli ni kwamba ilikuwa ni ndoto Lissu kumshinda Magufuli kabisa hili jambo ni lazima sote tukubaliane japo ni gumu sana
Unatumia tundu gani kuongelea mkuu? Sio kwa viroja hivyo aisee.
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Tukisema kwamba upinzani ni Chadema peke yake nchi hii muwe munaelewa,Watu wanakokotwa kwenda kuisaidia CCM halafu mnategemea wawasemee
Hata mbowe alisaidia sana CCM 2015 kwa kumleta Lowassa fisadi na kutupa wapambanaji.Wapinzani wote njaa tupu ukiona mtu anapiga kelele jua hajapata furusa.
 
Lissu alivutia umati upi wa watu!!? Unajitekenya na kucheka.

Kwani umati wake ulikuwa siri? Tena alikuwa anapata umati bila kuruhusiwa kuweka hata bango moja la matangazo.

Umati aliokuwa anapata ndio chanzo cha dhalimu kuanza kuugua, na baada ya matokeo kisha dhalimu kuujua ukweli wa kwenye box la kura, alichanganyikiwa na kupata sonona ya hatari. Hadi dhalimu anaenda motoni hakuwahi kuwa na raha tena.
 
Ila siasa kweli ni unafiki na kuwahi.
Miaka ya mwanzoni ya 2000 Selasini alikuwa kama office boy wa Mbatia. Leo hii kamtimua kwenye chama.
 
na bado watatajana sana...walidhani jamaa ni mungu ataishi milele

Huwa nashangaa sana wanacdm wakimtetea Mbatia kwenye hili balaa analokutana nalo sasa. Kwa kiwango kikubwa alitumika na Magufuli kupunguza nguvu ya upinzani. Na kwa kiwango kikubwa alitumika kuihujumu cdm yeye na Lipumba. Hili tulilieza wazi na ushahidi wa matendo yake ulikuwa wazi. Wafuasi wa CDM wanatakiwa wamuache Mbatia ashinde mechi zake.
 
Joseph selasini nadhani aliyoeleza yanakaribiana na ukweli kwani katika utawala wa mwendazake James mbatia alikuwa akifanya ziara mikoani kuimarisha chama chake huku akipokelewa na wakuu wa mikoa,. Mfano mzuri alipofanya ziara mkoa wa mbeya alipokelewa na mkuu wa mkoa wa wakati huo CHALAMILA

Cha kuchekesha eti akawapokea madiwani waliohama CDM wakajiunga na NCCR. Hao madiwani ni wale walionunuliwa katika ile KUUNGA JUHUDI PROJECT. Wakati wanasubiri kutambulishwa ndani ya CCM, Mbatia ndio akachomekewa awapokee ili kuonyesha kuwa CDM inazidi kubomoka. Akatoka hapo akaenda Arusha akapokea wanacdm wengine.

Cha kushangaza kila alipoenda alikuwa anapewa ulinzi na polisi jambo ambalo kabla ya kikao cha ikulu ilikuwa haiwezekani kwa mpinzani kupata hizo huduma, na huko kote alikokuwa anapita alikuwa anapokea wanacdm tu! Halafu akawa kwenye kampeni zake anawasakama CDM zaidi kulingana na maagizo aliyopewa na Magufuli, na akawa anawaaminisha wananchi kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki kisa Magufuli aliahidi mbele ya mabalozi, sijui na dunia.

Maajabu ilikuwa hakuna dalili ya uchaguzi kuwa huru na haki, kwani dalili za dhuluma kama za uchaguzi wa SM zilikuwa wazi. Hayo yote Mbatia alikuwa anafanya kwa lengo la kuididimiza CDM, leo hii wafuasi wa CDM wanapata wapi dhamira ya kumtetea Mbatia?
 
Back
Top Bottom