Joyce Ndalichako na Kiingereza kibovu tena

Joyce Ndalichako na Kiingereza kibovu tena

Hiki unachokiongea kinathibitisha hujui lolote.

Mtu yoyote mwenye degree anapaswa kuwa na managerial skills maana mambo mengi atakayokutana nayo yatakuwa yanayohusu management.

Sasa unaposema phd holder alitakiwa huko benki anacrunch namba inamaana angekuwa nafanyi kazi za management??

Akili mbovu sana hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Managerial skills unazipata kwa either kusomea degrees zake ie. Business Management, Health and Social Care Management, Oil and Gas Management, etc Management.

Ama unazipata kazini through training and development; ndio maana kwenye vikao vya bunge majuzi mwenyekiti wa kamati ya serikari za mitaa akawa anashauri kutokana na walichokiona wakurugenzi wengi huko wilayani ni incompetent kwenye usimamizi kwa sababu ni untrained matokeo yake wanategemea msaada wa wafanyakazi wa halmashauri wenye experience ambao wamepanda madaraja kutokana na kupatiwa mafunzo ya usimamizi.

Hakuna degree isiyokuwa na neno management mwishoni ina cover wide scope areas of management; Mtu anaesoma business studies, Social Work, Oil and Gas exploration or any other degree ambayo aina neno management awezi kuwa na wider knowledge ya management anachofundishwa ni namna ya ku perform task for the most part; trust me.
 
Kwako wewe mtu mwenye "bonge la elimu"unampima kwa umahiri wake wa kuongea English?

Vp unadhani amepewa hiyo dhamana aliyonayo hivi sasa kwa uwezo wake katika kuongea English?

Kwanini usihoji anafanya jitihada gani kuhakikisha elimu ya Tanzania inawawezesha wahitimu kujitegemea katika kila nyanja?
badala yake unahoji uwezo wake wa kuongea English kwa ufasaha?
Huoni kama akiendelea kuwa hapo anaweza kutuletea wasomi dizaini yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usipaniki babu, hakuna aliyohoji utendaji wake, ishu ni kwa nini Waziri wa Elimu level ya PhD hajui lugha ya Malkia kwa ufasaha?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijapanic dogo na katika jibu la msingi ungekuwa na akili ya kusoma vitu between the line ungekuwa umeshaelewa. kiingereza ni somo miongoni mwa masomo mengi. Performance ya kwenye Science si lazima kujua English grammar. Na wewe ni kwa sababu tu uelewa wako ni mwembamba ndiyo maana unapata shida na hivi vitu. Naendelea kukusisitiza hata hiyo PhD yake haina uhusiano wowote ule na English grammer.
 
Punguza Ugoro.
Umewahi kumsikia Jose Mourinho akiongea broken English? Mourinho unaongea English fasaha,nenda karudie kusikiliza au kuangalia video zake mkiwa pamoja na Ras Simba.
Anazungumza lugha nyingine 5 kubwa duniani na hana hata masters katika elimu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Cha kwanza kabisa unachopaswa kufahamu,hakuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya mtu kuongea lugha hata kumi kwa ufasaha na elimu aliyonayo,na zaidi sio rahisi kwako wewe kuona makosa ya mwengine kwenye jambo ambalo huna ufahamu wa kutosha juu yake!!
 
Joyce Ndalichako anapenda kuongea Kiingereza lakini Kiingereza hakimpendi. Hebu aliyemuelewa hapa atuambie alikuwa anataka kusema nini?

Hii ni mara ya 2 ndani ya siku 60 kwa Waziri kuongea Kiingereza chenye uvunjifu wa sarufi na tafsiri ya neno kwa neno toka Kiswahili kuja Kiingereza. Ya kwanza ni pale alipokuwa anamtishia Mkandaarasi wa kichina kuwa nitakusweka ndani (You will stay inside)

USHAURI:
Namshauri Mh Waziri awe anaongea kwa Kiswahili tu au awe anasoma hotuba alizoandikiwa na wataalamu. Kinyume chake anadhalilisha PhD yake na Vyuo vilivyompa hizo shahada.

Zaidi soma: Hivi hiki ndicho Kiingereza cha Profesa Ndalichako?
View attachment 1355606
Like daughter like father
 
Hata mie niliyedrop masomo ya History; Geography na Biology nikiwa kidato cha pili namzidi

"Even me who dropped subjects of history, geography and biology while in form two I am better than her"
Duh... Hebu malizia na aya ya mwisho
 
Wewe ndiye mjinga. Elimu ya Tanzania tunajifunza English kama somo compulsory kuanzia Std 1 mpaka O-level, yaani miaka 11. Na ni language of instruction kwa masomo yote kasoro Kiswahili kuanzia Form 1 hadi University yaani miaka mingine 9. Kisha kama unafanya Masters na PhD una miaka mingine 5. Kwa ujumla ana minimum ya miaka 25 ambayo alikuwa involved au kujifunza lugha au kutumia lugha ya Kiingereza

Hakuna excuse ya kusema eti Watanzania lugha yetu tunayoongea sana ni Kiswahili ndiyo uongee English fyongo kama hiyo ya Joyce. Kulazimisha kuongea "broken English" ni more damaging kuliko kuongea Kiswahili then mkalimani akakusaidia kutafsiri.

Kubalini tu kuwa Kiingereza hakimpendi, abakie kwenye Kiswahili tu, otherwise anajiaibisha kama Waziri mwenye dhamana ya Elimu nchini.
Sasa kama lugha yetu ni Kiswahili kwa nini aongee lugha isiyo yake?
 
Upo uhusiano wa kuongea lugha hiyo kwa fasaha na kama lugha hiyo ilitumika kukufundushia kwa muda mrefu na ulifundishwa kwa ubora unaostahili.
Cha kwanza kabisa unachopaswa kufahamu,hakuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya mtu kuongea lugha hata kumi kwa ufasaha na elimu aliyonayo,na zaidi sio rahisi kwako wewe kuona makosa ya mwengine kwenye jambo ambalo huna ufahamu wa kutosha juu yake!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwako wewe mtu mwenye "bonge la elimu"unampima kwa umahiri wake wa kuongea English?

Vp unadhani amepewa hiyo dhamana aliyonayo hivi sasa kwa uwezo wake katika kuongea English?

Kwanini usihoji anafanya jitihada gani kuhakikisha elimu ya Tanzania inawawezesha wahitimu kujitegemea katika kila nyanja?
badala yake unahoji uwezo wake wa kuongea English kwa ufasaha?

Kwanza kabisa sijahoji. Nilikuwa namwambia mchangiaji asipotoshe mada.
Pili, suala la kuhoji kifanyike nini ili wahitimu wakitanzania waweze kujitegemea kwa kila nyanja ni mada nyingine ambayo hapa haihusiki, walakini waweza kuianzishia uzi ukiona vema. Watu wajifunze kubakia kwenye mada. Full stop.
 
Mkuu kumbuka kwamba,kwa mtu yeyote kuongea ama kutokuongea english fasaha hakuna uhusiana wa moja kwa moja na elimu aliyonayo!!!
Mkuu, kuna uhusiano mkubwa sana wa elimu na ufasaha wa lugha. Hata ukienda US, UK, Canada etc. watu ambao hawajasoma hawaongei lugha kwa ufasaha kama waliosoma. Nia utawajua kirahi tu. Same Tanzania, pamoja na kwamba Kiswahili ni lugha yetu bado pia tunajifunza Kiswahili mashuleni. Kuna watu wengi tu (asilimia kubwa) wamejifunzia kuongea Kiswahili mashuleni. Watu wengi (hata humu) kwa kufuatilia maandishi ya wengi utaona ni jinsi gani tunapishana kwa ufasaha wa Kiswahili.

Tatizo kubwa la Ndalichako siyo tu kwamba ameongea broken English bali ameshindwa kufikisha ujumbe kwa walengwa.Zaidi ya Watanzania sidhani kama wengine wamemuelewa alikuwa anataka kusema nini.....!!
 
Back
Top Bottom