Joyce Ndalichako na Kiingereza kibovu tena

Amekaa darasani miaka zaidi ya 10,
humu tumeshaongea kuna eneo halitakiwi kucheza hasa elimu ya msingi.Shule za serkiali zote ziwe english medium.

Ndio maana wazazi wengine wanaonekana wabishi hawataki elimu bure lakini sio kweli wanakwepa aibu kama hizo mbeleni kwa watoto wao
 
Wajinga wenzio ndo walikubali hizo sifa za kuwa mbunge,hapana lazima tuukubali ukweli kwaamba kuna shida,haiwezekani kwa prof kuwa na kiingereza chakuokoteza vile.Inawezekana hujui vzr sifa ya kuwa prof.Visingizio kibao eti ooh wamesoma sayansi utafikir sayansi inafundishwa kwa kiswahili haina maneno ya kiingereza.
 

Kwani sayansi yote inasomwa kwa kiingereza kote duniani?
 
Mmh, mbona shida!!!???

"......to make sure that the children of Tanzania are get their......aaah they are achieve.....".....!!!!!!????
 
Haya tumeona utumbo wako ulioandika kuhusu PhD yako ya Kijerumani. Gambia kuwa kama una PhD kwa lugha ya Kijerumani na huwezi kuongea basi hiyo ni PhD fake kama ya Prof Ndalichako.
 
Basics free basic primary education ands the they decision was made make sure that all all tanzanian children of Tanzanian give aaaaah
Yaani hivyo😏😏😏😏😏
Halafu mijitu inataka kweli tukae kimya kwa broken hiyo kisa ana PhD ya mathematics?? Kwani PhD ya mathematics kutengeneza model gani tuone?
 
Acha kabisa hizo. Kiinglishi ni lugha yetu ya nne hivyo uelewe kuwa ipo hivi kama wazazi ni makabila tofauti basi:
1. Utamfahamu lugha ya baba
2. Utamfahamulugha ya mama
3. Kiswahili murua kila jona na primary yote usipokuwa somo la Kiinglish linalofundishwa na waalimu waliopata daraja la
4. Kiongozi cha mwisho na ni darasa ni tu.

Wewe ambaye nimesoma mjini na kuja yenu ya kikabila kufahamu ukiingia baby care mpaka university umetumia kiingereza huwezi jifananisha na sisi wa rika la Ndalichako tuliosoma na kukulipa huko moundombinu iliyokufa.

Kuna nchi hata English hawaongei anzia na nyingi za Asia,nhia Ufaranza, into a Kurudi, into a ujerumani n.k. Tuliokwisha tembelea hizo nchi nakuambia hata supermarket ni majanga huna msaada. Kama Uholanzi ya kusini kule Mastritcht usiombe kufika huko.

Hivyo acha Prof achape kazi Kiinglish ni lugha yake ya nne aliyojifunzia shuleni.
 
Huna akili ,aliyekwambia kujua English ndiyo ishara ya usomi ni nani?

Karne hii bado unaamini anyeongea kiingereza vizuri ndiyo msomi??

Hovyo kabisa ,shithole mind.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hebu tueleze maana na tafsiri ya msomi kwako ni IPI, maana binafsi nimeshindwa kuielewa dhana unayotaka kuijenga hapa hata kutetea hili.....

Ninavyoelewa mimi ni;

1. "Mtu msomi" ni yule mwenye ujuzi na maarifa katika kitu fulani, kwa hiyo mbobezi ktk fani hiyo

2. Lakini hiyo pekee haitoshi kumkamilisha mtu huyo hata kuitwa msomi isipokuwa awe na uwezo kuutumia ujuzi na maarifa yake kumletea yeye binafsi manufaa pamoja na watu wengine (jamii anayoishi kwayo)

3. Hata hiyo, bado hiyo pekee inakuwa haijatosha kuukamilisha "usomi" wa mtu fulani mpaka pale naye atakapoweza kuushirikisha kwa watu wengine huo usomi wake ktk njia rahisi zenye kueleweka...

Moja ya njia hizo ni uwezo wa namna ya kuwasilisha (kushea) kwa busara na hekima maarifa kwa kutumia lugha rahisi kwa ufasaha, yenye staha na isiyotweza utu wa watu wengine ili kutoa madini (maarifa ya usomi wako) uliyonayo ili kuwatajirisha wanaokusikiliza wawe kama wewe...!!

Ndiyo maana kuna msemo huu maarufu wa;

".....amesoma lakini HAJAELIMIKA" ....na yaweza pia kuwa ni; "....AMEELIMIKA lakini HAJASOMA....."

Je, unadhani Joyce na kaka yake Magufuli wanaweza kuwa ktk kundi gani hapa?

Aaah, obviously ni;- WAMESOMA LAKINI HAWAJAELIMIKA!!!
 
kwani kiingereza ndio elimu ya mtu au lugha tu kama kichaga,
natamini sana serikali itamke waziwazi kuwa kiswahili kitumike ktk shughuli zote za serikali na kiingereza kitumike tu kama lugha ya ziada maaana watanzania tumeleweshwa na kiingereza hadi mtu akikosea kwa bahati mbaya basi tayari unaaanza kuuliza juu ya elimu yake kama iko sawa!!

naiomba serikali yetu kupitia waziri wa habari tangazeni kiswahili kiwe ni lugha rasmi ya shughuli za serikali ikiwemo Mahakamani ambapo bado kinayumika zaidi kiingereza wakati wanao kijua wachache.tuache ukoloni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeeleza vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…