Hivi Kuongea English ndio Ishara ya usomi!???
Watanzania English sio lugha yetu ya kwanza wala ya pili,mara nyingi tunaitumia tuwasilianapo na wageni na pia katika shughuli za kiofisi!!
English sio lugha yetu mama hivyo huwezi ukaiongea kama ambavyo inaongelewa America na Uingereza...Halafu tambua yeyote anayejifunza English ukubwani lazima akumbane na changamoto kwenye kuongea...
Kwa Mfano ili uwe mjuvi wa English lazima uwe mzuri kwenye" Pronunciation " hapa hubeba asilimia 60 kwenye uongeaji wa lugha hii..
"Stress" Mikazo ya maneno hapa napo ndipo shida hutokea kwa watu ambao English sio lugha mama na hapa hubeba asilimia zisizopungua 40.
Intonation,Rythm...kila lugha ina mfumo wake na mpangilio wake wengi kiswahili kimetuathiri sana na hzi lugha zetu za makabila...
Ni ngumu kuongea English yenye kupendeza masikio ya watu tusiongee kwa mihemko aisee
Sent using
Jamii Forums mobile app