Joyce Ndalichako na Kiingereza kibovu tena

Kama na Joyce kwa kizung hicho ni kichwa basi Tanzania haina wasomi
 
Sioni mantiki yoyote ya kumlaumu Professor kwenye lugha. Kujua lugha sio maarifa ni lugha tu kama kuhaya, kikorea, kachina n.k. Nauliza swali je mtoto wa miaka mitano aliyezaliwa UK ambapo lugha ya kiingereza ndio asili yao ana akili kuliko Rais wa China ambaye hajui kiingereza. Tuna fikra potofu sana watz haswa kuhusu lugha. Mie watoto wangu wanasoma shule za English medium na wanaongea kiingereza vizuri kushinda mimi lakini mimi nina elimu kubwa sana ambayo nimeipata kwenye vyuo vikubwa tu vya dunia ya kwanza na sio mtaalam kihivyo wa hiyo lugha na hayo wazungu nilikuwa nawagalagaza sana darasani
 
Wadau msimtetee huyu waziri wenu hata kama mna mapenzi nae, kwa nafasi aliyonayo, kwa level yake anayojitangaza (kwamba ni Profesa) hastahili kuongea ovyo ovyo hivyo, kama hawezi kunyoosha ulimi basi aache kuongea kingereza, umesema kweli kuhusu pronounce, lakini ni kutuaibisha sisi watanzania, nimegundua ndio maana yeye na bosi wake (rais) wanazichukia sana shule binafsi, kwa sababu kule wanatolewa wanafunzi ambao akiongea hapa kiingereza utadhani amezaliwa mjini Manchester, lakini pia amekaa muda mrefu sana huyo darasani, inaonesha ana kichwa kigumu, ndege wafananao huruka pamoja
 
Upuuzi mtupu! Mleta hoja unakuja na upumbavu kama huu? Kiingereza ndio cha kumsema nacho mama Ndalichako? wewe unakijua? Ulizaliwa nacho? Kiswahili tulichozaliwa nacho tunaharibu sembuse hii lugha iliyokuja na meli? Kwendaaaaaaaaaaaaa!
 
Jose Mourhino ni mcheza mpira au kocha wa mpira. Joyce ni PhD holder na mwalimu na sasa waziri. Acha kutetea ujinga
 
Mnategemea akajifunze wapi na hivi safari za nje zimekatazwa mpaka ukapate kibali maalumu kutoka kwa Boss ( RA-HISI)?
 
Najivunia kufundishwa communication skills na Dr Chi'panda serikal kwakweli hajanifanya nishwindwe kusoma compaund sentences kama huyo amenifundisha speech derivation techniques live long Dr sio hawa maprofessor wa kuunga unga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila sahaka utakua mtaalamu wa lugha wewe
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera Mag3 kwa kutoa msisitizo kwa kutumia English iliyosimama vyema
 
Mtu mwenye PHD ya hesabu kumuweka kwenye uwaziri sio sawa, huyu ilitakiwa awe kwenye kitengo cha hesabu anapanga mitaala ya hesabu huko. uwaziri angepewa watu wa history na kiswahili
 
Wakenya hawasomi kwa kiswahili mpaka PhD, so kutokujua kiswahili siyo ishu

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakenya hawasomi kwa kiswahili mpaka PhD, so kutokujua kiswahili siyo ishu

Sent using Jamii Forums mobile app
kiswahili in kenya ni lugha ya taifa na inatumika pia kwenye shughuli za kiserikali kama tu kingereza hapa kwetu na the predicted kenyan 5th hayuko competent nacho kutokuwa competent na kingereza kwa JN hakudhuru sana kama tunavyotaka kumaanisha
 
Other than the "ehs" and her thick African accent, (in my opinion) she did just fine grammatically.
 

Lugha rasmi ya kibiashara na kisheria (official business and legal language) ya Tanzania ni lugha gani?
 
Tuwe tunaelewa kitu kila lugha unayoongea inaathiriwa na lugha mama. Prof anaongea vizuri tu. Tusimlazimishe mirindimo yake ya sauti wakati anaongea iwe kama ya Muingereza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama na wewe unasema Profesa anaongea vizuri basi na wewe ni mburula mwingine wa Kiingereza. Rudi kwenye clip tena
 
Halafu utakuta Hugo ni mmoja wa wale wanafunzi kutoka shule za "mtakatifu..."
Na alikuwepo kwenye kumi bora kitaifa.
Yote ni ili upande flani uonekane una wasomi wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwanza kumfananisha Profesa wa Tanzania na mtoto aliyezaliwa UK inaonyesha hujaelewa mada. Pili kama mtoto wako anayesoma English medium anajuwa English kuliko wewe uliyesoma mpaka nje ya Tanzania basi wewe ni mburula na mwanao ni mkali. Ikifika jioni mwambie shikamoo mtoto
 
Kwani mkuu wewe gramatical English unataka ikusaidie nini katika maisha yako ya kawaida ya kila siku? Boutros Boutros-Ghali Mmisri mwanasiasa na mwanadiplomasia aliyetukuka aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa hakuwahi kuwa na Kiingereza kizuri hata siku moja lkn kaserve kwenye nafasi kubwa kabisa na kwa mafanikio makubwa. Hangaika na matokeo ya kazi anayofanya mama ndalichako achana na lugha anayozungumza hasa hizi zilizoletwa kwenye makontena.
 
Upuuzi mtupu! Mleta hoja unakuja na upumbavu kama huu? Kiingereza ndio cha kumsema nacho mama Ndalichako? wewe unakijua? Ulizaliwa nacho? Kiswahili tulichozaliwa nacho tunaharibu sembuse hii lugha iliyokuja na meli? Kwendaaaaaaaaaaaaa!
Usimjibu mpumbavu kadri ya upumbavu wake, usije kuwa sawa na yeye ... (Mithali 24:6)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…