Joyce Ndalichako na Kiingereza kibovu tena

Hata hayo matokeo mboa hayapo, au inatakiwa darubini kuweza kuyaona ?.
 
Hiyo Phd yake lugha aliyotumia kuipata ni kingereza, kushindwa kuzungumza kingereza vizuri ni lazima tuwe na mashaka research na thesis alizifanyaje?
Angekuwa Mrusi au mchina ingeeeweka lakini kaipata kwa Kingereza
Hata wewe hicho Kiswahili chako ukifuatiliwa bado utaonekana hukijui vizuti. Kukosea grammar haina maana kuwa mtu hawezi kufanya research au kuandika thesis/dissertation. Hiyo research kwanza kuna sehemu unaweza kulazimika kutumia kiswahili ili kukusanya data hasa ikiwa respondents hawajui English kisha unatafsiri mwenyewe katika English. Wewe una chuki binafsi na huyo mama sasa unatumia huko kuteleza kidogo kumshambulia. Voivyote vile huyo mama yuko vizuri kichwani kuliko wewe na ikitokea mkapewa mtihani wowote ule wewe na yeye atakubwaga mbali. Raha ya JF unajikficha nyuma ya keyboard unashambulia lakini ukiambiwa wewe unayejua umesoma hadi kiwango gani cha elimu huwezi taja humu. Kumbuka hakuna anayejipa vyeti bali hupewa baada ya jopo la wanazuoni wanaokubalika katika ngazi husika kuona fulani anastahili kutunukiwa. Elimu ya huyo mama inatambulika mpaka kimataifa hata wewe binafsi usipoitambua.
 
Wakenya hawasomi kwa kiswahili mpaka PhD, so kutokujua kiswahili siyo ishu

Sent using Jamii Forums mobile app
In kenya kiswahili ni lugha ya taifa na inatumika ktk shughuli za kiserikali na there probable kenyan 5th hayuko competent nacho na our JN sio kwamba hajui kabisa she is just not competent enough of which haidhuru sana na not only her many of our learned bro and sis wanatafsiri tu kingereza kwa lugha yao ya kwanza na haijaathir sana utendaji wao
 
Eti huyu alikuwa katibu mkuu wa baraza la mitihani Tanzania.

Huuu dr huu Uprofessa. mimi nina mashaka sana nao.

Hata wengine wakubwa kabisa ila kiingereza hawajui. sasa hizo insha zao (thesis) wali defend vipi? kama sio za kununua.
 
yaani unataka kushindana na phd?huyu mama kasoma hiyo ni lugha tu mbona wengine kiswahili nacho ni shida
 
Kuongea kiinglish ingekua rahisi zaidi kuliko hayo mahesabu mnayomsifia kuyajua!!

Sijui anakwama wapi!!

Yaani ku derive ma formula koote present continues, future tenses zinamzinguaje????

Hatumvui nguo, anajivua mwenyewe,

Mwacheni ajitetee mwenyewe kwa kiinglish.
 
Hapana sio kweli, kuanzia form one mpaka PhD unatumia English kusome, how come someone with PhD she is not be able speak a good English
 
kwamba kujua kingereza inatokana na uwezo wa mtu binafsi na mazingira aliyokulia na kusomea. Pia, haina uhusiano na uwezo wa kiakili wa mtu.
 
Lkn hili tatizo sidhani kama liko confined kwa huyu mama peke yake ni changamoto kubwa linalowakabili wasomi wengi ktk nchi hii.

Nchi hii pamoja na kuwa tunakitumia kiingereza kama Medium of Instruction ktk sekondari zetu na kuendelea lkn tatizo lipo kwa wakufunzi kwani wengi wao hawako vizuri kwa lugha hiyo.

Pia hatuna msingi mzuri wa hii lugha kwani ktk shule za msingi ambako pia hufundishwa kama somo walimu huko pia hawako vizuri ktk lugha hiyo, hivyo Joyce ni the end product of a poor manufacturing process, she should therefore not be very much vilified.
 
Hapana sio kweli, kuanzia form one mpaka PhD unatumia English kusome, how come someone with PhD she is not be able to speak a good English
Mara nyingi tunatumia English kwenye kuandika na sio kuongea...hivyo basi mfumo wetu wa elimu haumfanyi mtu awe mzuri kwenye kuongea English kwa ufasaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe mwenye kingereza kizuri mbona unashinda tu humu ndani pasipo msaada wowote kwa taifa lako.

Kingereza ni lugha yetu ya pili kumbuka sisi sio kama wakenya ambao wanakijua vyema kingereza wakibebwa na mazoezi ya maongezi ya kila siku na kila mahali.

Achana na mawazo ya kishamba na kitumwa.
 
Rudia kusoma ulichoandika mwanzo halafu linganisha na ulichoandika sasa baada ya hapo tuambie hoja yako ni nini.
Hoja yangu nilishaitoa ila ya kwako sijaiona badala ya swali....

Hebu sema unachokisimamia nami nipate kujifunza...

Angalizo:Tusibishane bali tuelimishane!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana sio kweli, kuanzia form one mpaka PhD unatumia English kusome, how come someone with PhD she is not be able to speak a good English
Lugha yoyote inahitaji practice, tatizo hapa Tanzania unaweza ukakaa mwaka mzima kwenye maeneo fulani usipate hata mtu moja wa kuongea naye hiyo lugha.

Ktk nchi kama Kenya, Uganda, Zambia, Zimbabwe, SA, Malawi, Botswana nk wanatuzidi mbali kwa sababu kiingereza ndio lugha yao ya pili na ndio inayotumika kufundishia ktk ngazi zote za elimu wakati sisi ni kiswahili hadi wengine hawawezi hata kuongea kilugha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…