JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship

JPM, CCM wakishinda, Freeman Aikaeli Mbowe ni lazima ajiuzulu, amwachie Tundu Lissu. Lissu aache Uanaharakati, aonyeshe Statesmanship

Laana iambatane nawe milele yote

Eti Lissu aache uanaharakati ! Upo serious kweli?
Roho yako ni nyeusi kiasi hiki

Aliyepigwa risasi 16 ulitaka azungumze vipi afanye lipi mtambue 'kisaikolojia' mliyabadilisha maisha yake 360 degrees
Mgombea yupi mwingine amepitia aliyopitia Lissu

Angekuwa mjomba wako Baba yako Mtoto wako au wewe mwenyewe ungeandika huu urojo kweli?

Nachukia watu waliokosa utu huruma upole na upendo
Mungu akufunulie akuguse utambue 'hujafa hujaumbika'

Lissu ana kila sababu ya kuzungumza anavyozungumza hujui maumivu aliyopitia

Muombe Mungu akuzidishie miaka mingi ya kuishi ushuhudie Nguvu ya Mungu kwa wamchukizao
Wapandao kwa machozi watavuna kwa shangwe

Mungu halali wala hasinzi
Tunapiga magoti kumlilia na kuomba aliepushe Taifa na watesi

Roho yako kwatu kwa yanayotokea Zanzibar

**mods msifute comment yangu nimepata kibali kwa Mungu tafadhalini !
 
Mbona kuna vyeo vingi sio lazima uwe mwenyekiti kuna vyeo vingi. Pili wewe umeshasema ni kada wa CCM sasa kwanini wasikilize watu ambao wanaombea chama kife.
 
kwa hizo porojo zako yani hata asingekuwa lissu, ata ungeweka mawee ya gombea yange shinda asubuii kabisa.

afu tatizo lako una matatizo ya kiafya ya akili una kisukari nini?
 
Mbowe pamoja na mipaka ya elimu ya darasani ameweza kuwa proactive politicians, ni muanzishaji wa masuala ya kisiasa na muendelezaji.

Lissu ni reactive politician kwa maana ya hoja zake hutokana na hoja za wengine, ni fundi wa kujibu hoja lakini hana kipaji cha kuwa na hoja za mwanzo za kuanzisha wazo fulani la kisiasa.


Lissu hawezi kuacha kuwa mwanaharakati ndio alivyozaliwa.
 
Hilo la kwamba Tundu Lisu atashindwa hilo liondoeni kwenye akili zenu, labda tujadili kutangazwa. Kwa mwendo wa katiba yetu, ni rahisi rais aliye madarakani kushurutisha kutangazwa. Na huo ndio mpango uliopo, lakini ikiwa hilo litatokea bila ridhaa ya watu, basi tuendelee kuomba huu ukondoo uitwao amani utamalaki, kinyume na hapo tutajadili mengineyo.

Tuje hilo la uenyekiti wa Mbowe. Mimi sio muumini wa kiongozi yoyote yule, kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi kwenye nafasi moja ya utawala wa kisiasa. Mara nyingi kiongozi akikaa madarakani zaidi ya miaka kumi ubora wake hupungua, na mara nyingi hutawala kwa mizengwe. Mfano wa viongozi hao ni:
Nyerere
Moi
Ghaddaf
Mugabe
Museveni
Kagame nk

Katika mashabiki wa cdm tuliopinga Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti, hasa uchaguzi uliopita mimi ni mmoja wapo. Na sababu zangu ni kuwa sio muumini wa zaidi ya miaka 10, pia Mbowe kashuka ubora na sasa anatawala kwa mizengwe. Pia kosa la kumpokea Lowassa ndani ya chama na kumpa nafasi, linatosha kuwajibika kwa kiongozi muwajibikaji. Kitendo cha cdm kukosa ofisi yenye hadhi ya chama hilo, linatosha kumuweka Mbowe pembeni.

Toka Magufuli ameingia madarakani, ujasiri na uimara wa Mbowe kuongoza cdm kama taasisi umeondoka. Yeye na Mnyika kwa sasa wanaiendesha cdm kwa ubora duni. Nakubaliana na MMMK kuwa Lisu sasa anastahili kabisa kuwa mwenyekiti wa cdm, awe rais au asiwe, na katibu Mkuu anastahili kuwa John Heche au Marcus Albanie i.
 
Pascal Mayalla mbona hujasema gwajima aachane na siasa aendelee na harakati zake zakikanisa maana sadaka zinamtosha.

Nina swali hapa ivi ni lazima JPM agombee muhula 2 wakat hata huo unamtosha ... Unasiasa bado za karne 18 this is 21c mzee
 
Back
Top Bottom